"P
ascal Mayalla, post: 34462355, member: 17813"]
Kujua nani kamwaga damu ya nani on a line of duty na kutomtaja, hakupelekei karma yoyote na kujua huko hakumfanyi yeye kuwa responsible or an accessory before the fact or after the fact.
Mkuu P, somo la Karma ni pana sana.
Karma haijitokezi kama watu wanavyotarajia, hujitokeza kwa namna nyingi na tofauti sana.
Mfano 1: Marekani mtu aliua mkewe na kumzika uani. Imepita miaka zaidi ya 20 hakuna aliyejua nini kilitokea.
Nyumba imeuzwa, mnunuzi akaamua kuchimba uani katika kutengeneza na kuimarisha nyumba yake.
Alikutana na mabaki ya marehemu, uchunguzi ukabaini mumewe alimuua. Karma ikajitokeza jamaa kanaswa.
Mfano 2. Same Kilimanjaro kuna tukio la mtu aliyepotea baada ya kuchukua mafao yake.
Mkewe alipofariki akataka azikwe eneo X. Wakachimba pale pale mumewe alipozikwa.
Ikabainika aliyetenda unyama ni mwanae miaka zaidi ya 10.
Mama kutaka azikwe eneo X ilikuwa ni 'Karma' ili mwanae inamrudi leo hii.
Mfano 3; Marekani kuna wimbi la askari kupata matatizo wakiyaita PSTD(Post stress traumatic disorder)
Idadi ya askari wanaojiua kila siku inaongezeka na hata kuwa ''janga''. Je, hii si karma ?
Hata waliotekeleza uovu huo, kama wametekeleza kwa amri halali on the line of duty, pia wanakuwa hawana hatia yoyote kwasababu wao walikuwa wanatimiza wajibu wao, na kama wameajiriwa kumwaga damu na hiyo ndio kazi yao, wakimwaga damu yoyote kwa amri halali, huko ni kutimiza wajibu wao na damu hiyo haitakuwa juu yao, ni kama mnyongaji, au wanajeshi vitani, sheria ya vita inataka wa target military targets na kama ni kuua, waue wanajeshi na sio civilians, lakini vita haina macho, au kombora halichagui nani mwanajeshi na nani civilians kama Hiroshima na Nagasaki, hadi sisimizi hakusalia, sasa wanajeshi vitani wanapoua innocent civilians damu yao haiwi juu ya wanajeshi hao bali aliyeanzisha vita hiyo au aliyetoa amri hiyo.
Amri halali ndiyo subject hapa.Vitani ni amri halali.
Mnyongaji anatenda kwa amri halali tena mchana kweupe baada ya process nzima ya uhalali kufanyika.
Wanaokabiliwa na adhabu ya kunyongwa kamwe hawalaumu wanaotimiza wajibu.Ni amri halali.
Swali, amri halali mipaka yake ni ipi?
Kuna sababu inaitwa halali, kwa maana imepitia hatua halali, imeelezwa kihalali, imeidhinishwa kihalali.
Hata vitani kuna kitu kinaitwa ''rule of engagement' kwamba, kuna abcd za kufanya na kutofanya.
Uwepo wa 'rule of engagement' unalenga kuhakikisha askari wanatimiza amri halali kama ilivyoelezwa.
Kwahiyo amri halali ina namna zake na mipaka yake si ''open season''
Mkuu P huku mitaani watu hujitoa katika baadhi ya maamuzi ya Familia au Ndugu yenye utata.
Kauli kubwa unayoisikia ni moja '' wana nawa mikono yao'', kwa maana wanajiepusha na ''karma''
Hoja yangu hapa ni maoni tu ya jumla juu ya Karma. Hailengi kuhusu tukio au watu kwa namna yoyote