Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Pascal Mayalla, Mkuu Pasco,
Umemwaga nondo za ndani sana mkuu.

Ila ninawaza kwa sauti, mpaka leo nina mashaka makubwa sana kama waliohusika na tukio na TL ni vijana wa kitengo.

Maana kwa jinsi jamaa ambavyo hufanya kazi na once the job is done it's hard to trace the footprints, nina maswali risasi 30+; unless kama kazi hii ilifanywa amateurs; unless kama kulikuwa na motive ya kuifanya mission hii isifanikiwe.

Ila masuala ya clean-up yapo toka agano la kale. SAULI mfalme wa kwanzs Israel amewahi kutumwa kwa taifa la amaleki kufanya "ethnic cleansing". It happened hakutii.

Kwa kuwa ndiyo mifumo ya kazi na watu wamekula viapo, basi "let them do what they were sworn in to do"

Otherwise Paskali una ujasiri wa ajabu sana kufunguka mambo ambayo watu wengi huongea kwa mafumbo ila wewe bana unaita koreo ni koreo na sio kijiko kikubwa




Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Maskafu" ni ulimbukeni tu, hauongezei hadhi yoyote kwa anayeyavaa.

'In fact' inaweza onekana kama ishara ya udhaifu kwa anayeyavaa; kama jitihada za kuficha hayo madhaifu mengne aliyonayo.
 
URAIS SIO NDOTO ZA MTU BALI NI HITAJI LA WAKATI NA HITAJI LA WATU . HIVYO HII SIO AGENDA KWA SASA. NIULIZE KUHUSU IRAMBA
LOooh, mbona kauliza kuhusu Iramba hapo, na bado hukujibu lolote juu yake; na badala yake ukakimbilia kwenye urais?

Ishara mbaya hii!
 
Mwigulu sasa amejifunza kitu kipya hapa JF licha ya kuwa member muda mrefu. Maswali aliyoulizwa na tuhuma nzito nzito zilizoelekezwa kwake ambazo ni kama amehukumiwa tayari duniani na mbinguni. Hatakaa Hasau huenda pia akajitoa JF.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla,

Paskali, nakuheshimu sana kama mwandishi na kama binadamu mwenzangu. Lakini katika hii falsafa yako, nafikiri umepotoka. Post yako hii imefanya niitilie shaka "integrity" yako kuhusiana na concepts za "utu" na "haki". Elewa kwamba, thamani ya "utu" ni ile ile kati ya mtu na mtu, na wote wanastahili haki sawa, bila kujali suala la "hadhi". Haki ya utu na "hadhi ya mtu" ni vitu viwili tofauti; nashauri tusivichanganye hivi katika miktadha kinzani.

Haki ya utu huivuvia jamii (inspires), ilhali hadhi ya mtu huitabakisha jamii (classifies). Moja ya vitu hatari vinavyoisinyaisha jamii ni matabaka (classes). Nakushauri ukamsome kwa makini sana Carlo Focarelli, mhadhiri wa Oxford, kuhusiana na jambo hili. Tafuta kitabu chake kinachoitwa "International Law as Social Construct: The Struggle for Global Justice."

Kama unataka kuidhoofisha au hata kuiua kabisa jamii yoyote ile, mantiki ni kuhuisha falsafa yoyote inayohusiana na "hadhi" za watu. Lakini kama unataka kuistawisha jamii hiyo, mantiki ni kuithamini thamani ya utu, na kuihuisha "haki" ya mtu yeyote aliye katika jamii hiyo - awe alisoma "Ilboru" au mwokota makopo wa huko Makoroboi!

Na hapo ndipo tunapoipata definition isiyoghoshiwa ya "haki sawa kwa wote", au "binadamu wote ni sawa." Kwa hivi, nakusihi usichanganye maboya hapo tafadhali. Thamani ya utu wa mtu haipimwi kwa vyeo vyake, mali zake, au akili zake; inapimwa kwa "utu" wake, na wala hii siyo falsafa ya TANU peke yake kama ulivyosema, bali ni kanuni rijali, ya msingi, iliyokuwepo toka mifumo ya maisha ilipoanza, na inayotumika katika jamii nyingi zilizokomaa.

Nikupe mfano mmoja mdogo. Ni kwa nini unafikiri, jamii zenye viongozi wanaozishusha "hadhi" zao ili ziwe sambamba na hadhi za "waongozwaji" aghalabu ndizo zinazofanya vizuri kiuchumi na kimaendeleo kwa ujumla? Na hapa nazungumzia jamii zenye maendeleo ya kweli - maendeleo ya watu na siyo ya vitu - jamii kama za Waskandnavia, New Zealand na nyinginezo, ambazo hata kitakwimu zinaoneshwa kuwa ni "least corrupt" (WEF, 2019).

Kwa nini unafikiri Mark Rutte, Waziri Mkuu wa Uholanzi, au Jens Stoltenberg, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Norway, hutumia baiskeli ili tu wawe sawa na wale wanaowaongoza? Ukipata jibu la swali hili utanielewa vizuri zaidi.

Kipindi fulani nilikaa Norway na Denmark kwa miezi kadhaa nilipokwenda huko kikazi, nikavutiwa sana na tabia yao ya kujishusha. Nilikuwa nafanya kazi na madaktari wengi (PhD holders) lakini hata siku moja sikuwahi kuwasikia wakiitana "doctor so and so" au kuongelea "shule maalum" walizosoma walipokuwa katika darasa la upili.

Sasa ichukue taswira hiyo niliyokupa, kisha uilinganishe na taswira ya Mwigulu Nchemba, unayemtetea kwa kusema: "siyo wa kawaida, ni mtu muhimu, na ni mtu wa maana sana, siyo sawa na Pasco" - mwanasiasa ambaye kucha kutwa huongelea ukiranja wake wa "Ilboru" na "PhD" yake ya kinadharia isiyo na uhalisia kwa mwananchi wa kawaida aliyeko Ntuzu - kisha useme mwenyewe kipi ni chuya na kipi ni mchele halisi katika mtazamo wako kuhusiana na utu, usawa, haki na "hadhi."
 
Juzi Dkt. Mwigulu alianzisha thread ambayo aliitisha wanaJF kuuliza maswali na yeye alikuwa tayari kuyajibu. Nilipitia posts hizo na nilishindwa kuchangia kwa sababu nilikuwa mbali na sehemu ambayo ina mtandao stable - kwetu Simbalungwala Iramba kwa kule chini chini mtandao unasumbua sumbua kidogo. Hata hivyo nilipofika sehemu nzuri nikamwuliza maswali mawili kwenye thread aliyoanzisha kuwa mbona kishaanza Kampeni ndiyo ikawa mwisho wake kuchangia kwenye thread aliyoanzisha mwenyewe. Akatuacha hewani.


Kwa maana hiyo Moderator naomba hii thread au uzi kwa Kiswahili usiunganishwe kwenye ule alioanzisha yeye kwa sababu ukipelekwa kule atajifanya hajaona na anaweza kupotezea tu km ambavyo amekuwa akipotezea maswali ya wengi waliokuwa wana shauku ya kujua yale waliyouliza na hajayajibu. Kwa leo naona ninaleta ushahidi kdg tu kuwa katika Chama chetu -

utaratibu wa kuanza Kampeni za ndani ya Chama haujatangazwa. Dkt Mwigulu mbona tayari kishaanza Kampeni, kwa nini anacheza faulo - haoni anachofanya ni kama vile wachezaji wanaootea kufunga bao? Kwa nini anatangulia mbele kama sio kuwatisha wale ambao wanakusudia kugombea ili waogope?

Kwa kifupi naweka baadhi tu ya sms ambazo amekuwa akiwatumia watu ambazo kwa tafsiri zinaonesha wazi kuwa kishaanza Kampeni:

Tarehe 16 Januari alituma meseji ya hivi kwa watu:

Salama Kiongozi wangu, kuna mawakala wanapigapiga simu kutaka kupotosha. Usipate hofu ya kuwajibu. Wanauliza Uchaguzi ukifanyika leo unamchagua nani? Wajibu kwa kujiamini kuwa unamchagua Mwigulu Nchemba. Tunashinda mpk Fainali na Kombe tunabeba. Kazi tulizofanya haiwahi tokea.

Juzi Tarehe 21 Februari 2020 akatuma ya hivi:

Salam,
Asante kwa ushirikiano WAKO SIKU ya ziara ya Ndg Mangula. Tuendeleze mshikamano huu mpaka mwisho. Siku ya Uchaguzi tufanye kubwa zaidi Nitakuja ziara tuweke mkakati zaidi. Wapange na wenzako, Nakutegemea kwenye Tawi lako. Mwigulu.


Hapa ninaacha kuweka namba ya simu anayotumia meseji hizo ili kuona kama atakataa kwanza. Kwa kifupi sikatai kuwa anaweza akawa amewatumia watu wake wa karibu lakini ktk uchunguzi wangu ni wengi wamepata hizo sms hata wale ambao ni wanachama wa Opposition. Zimeenda kwa watu randomly ndiyo maana hata sisi wengine ambao sio wafuasi wake wa karibu tumezipata. Sasa tayari watu wanakusanya ushahidi tu ili na ubabe wake huko baadaye waje wammalize kwa tuhuma za kuanza kampeni mapema.

Kwa ujumla Dkt. Mwigulu mie bado namshauri akomae na ndoto yake ya Urais mwaka huu Ubunge kwake sio. Ili kujiandaa kwenye Urais 2025 bora hata aamue kugombea Ubunge wa Afrika Mashariki au apumzike siasa za ubunge abaki chamani tu mpaka 2025. Atakuwa kajijengea heshima na tutamkubali sana.

Kwa sasa Dkt. Mwigulu anapaswa awe mtulivu sana, aache kuanzisha threads ambazo mwishowe zinamdefeat mwenyewe. Aache kampeni ambazo kishazianza. Atafute mtu katika Timu yake iliyotajwa siku za nyuma hapa:


Kwa mfano tu kuonesha kuwa Dkt Mwigulu kachokwa hadi Jimboni kuna mgombea mtarajiwa mmoja ambaye hajajisema wazi ametuma kijana wake kaenda kijijini kwao Dkt Mwigulu - Makunda na kakusanya kuanzia historia ya kijiji hicho. Jina Makunda ni Vibanda vya kujificha - kwamba kijiji hicho kilikuwa maarufu kwa wahalifu kujificha na hasa wezi wa ng'ombe na majambazi.

Katika andiko lake anaonesha pia kuwa zamani kulikuwa na watu wanaogopwa sana Makunda kwa sababu kukutoa roho ilikuwa ni rahisi tu. Kijana amepata habari za wahalifu wakubwa kama kina Mzee Mdindio na watoto wake ambao hata vifo vyao vilikuwa vya kuchokwa na askari polisi. Mwandishi anaendelea kuelezea kuwa pamoja na watu wa Makunda kubadilika sana lkn bado utamaduni wa kibabe na hali ya uhalifu imewakaa kwa kiasi kwa sababu ya kuishi sana maporini.

Kwa maana hiyo hata Dkt. Mwigulu anavyoonekana na yale mavazi yake ya kibabe sio makosa bali ni utamaduni aliokuwa nao tangu akiwa mdogo na ndiyo maana hata mambo ya kurudia shule ya msingi hiyo hiyo uliyomaliza mwaka uliopita kwao haikuwa jambo la ajabu. Ilikuwa ni kijiji chenye mambo yao wenyewe. Ukitoka kijiji cha mbali kwenda kutafuta mifugo yako Makunda hata kama wanajua nani kaiba walikuwa hawasemi kamwe.

Kila le kheri Dkt. Mwigulu katika harakati zako. Ongeza umakini tu. Kama unagombea Mwaka huu hakikisha hukosi. Ukikosa ndiyo wewe kwishney tena.
 
Nietzsche, Mkuu Hongera Kwa Comment iliyoshiba nyama na Kisomi na Exposure,
Mi Nimeguswa sehemu Fulani ya Kujishusha.

Umesema huko Denmark,Norway Holland waziri wakuu,hujishusha na Watu PhD hawapendi kuitana PhDs,
Je Wahandishi hawajiiti Engineer flani!?

Namaanisha Hawaanzi na Utambulisho wa fani/Professional ya MTU kwanza?

Mfano
Eng.Stella Manyanya! Kama hafanyi hivyo na Elimu hizi zimetoka Kwao na Sisi tunafanya Unafikiri Tatizo ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ishu ya wasiojulikana imeshahiribu CV yake na image kwa jamii maana hawezi futa historia,kama angekuwa na ndoto ya uraisi angejiuzulu kuonyesha ana msimamo apelekeshwi na maagizo ili kulinda heshima yake. Wapinzani wake watatumia hoja ya wasiojulikana itabidi ajipange nao vya kutosha.
 
Kuna mtu ametupia uzi kuwa siku hizi sivai skafu, huu ni mkutano mkuu wa juzi tarehe 19/2/2020 wakati wa ziara ya mzee Mangula. Skafu nilikuwa navaa hata kabla ya kwenda Ilboru Sekondari haikuwa sare ya Uwaziri.

View attachment 1365715

Kama kuna maswali kunihusu, nitayajibu hapahapa
Baada ya kukusema ndo umevaa si ndio ili kuprove wrong si ndio?wewe kaa hapo usubirie anguko lako tu ulicheza mchezo mchafu sana na dhambi ya kunyanyasa upinzani ukiwa waziri wa mambo ya ndani hii dhambi haitokuacha hata kama ulitumika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nietzsche, Mkuu Hongera Kwa Comment iliyoshiba nyama na Kisomi na Exposure,
Mi Nimeguswa sehemu Fulani ya Kujishusha.

Umesema huko Denmark,Norway Holland waziri wakuu,hujishusha na Watu PhD hawapendi kuitana PhDs,
Je Wahandishi hawajiiti Engineer flani!?

Namaanisha Hawaanzi na Utambulisho wa fani/Professional ya MTU kwanza?

Mfano
Eng.Stella Manyanya! Kama hafanyi hivyo na Elimu hizi zimetoka Kwao na Sisi tunafanya Unafikiri Tatizo ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
True wenzetu wenye phd sababu ni mature huwa awapendi kujiita Doctor wanapenda uwaite Mr au madam yaani jina halisi na sio kwa elimu zao tofauti sie waswahili utaisikia Alhaji Shekh Dr mheshimiwa ...... Au Mchungaji dokta nabii ....
 
Huna taarifa hata kidogo, fuatilia upate ukweli ndio uje uandike. Kama kawaida nadhani unatamani niishi kama mbwa koko. nikuhaikikishie watafute wenye taarifa wakwambie nani aliwasaidia walipokuwa na matatizo
Mkuu, utajiexpose na huu uzi wako. Bora kukaa kimya....!!
 
Back
Top Bottom