Ana miaka 46 anataka kunioa, je hii ni sawa kwa umri wangu?

Kinachooa ni umri? Tafuta umpendaye muishi kwa furaha. Linda moyo wako kuliko chochote
 
Ukibaki mjane utalia hadi unagalagala na kuongea kilugha??

Au utalia umevaa miwani nyeusi huku unajifuta na tissue.

Kama jibu ni la kwanza achana nae huyo ni mzee, kama jibu ni la pili olewa mdogo angu age is just a number.

binti kiziwi Atoto muongezeeni neno la kujenga.
 

Kama ni kuolewa usikatae, kataa UZINZI usikatae ndoa kwani mapenzi haya UMRI.
Unaweza kuolewa na kijana ukajuta kuolewa na unaweza kuolewa na mzee ukafurahia ndoa.
 
Kama ni kuolewa usikatae, kataa UZINZI usikatae ndoa kwani mapenzi haya UMRI.
Unaweza kuolewa na kijana ukajuta kuolewa na unaweza kuolewa na mzee ukafurahia ndoa.
Ni kweli mkuu lakini huyu mbaba naona hadi aibu ikifika huo muda wa kwenda kumtambulisha kwa ndugu na wazazi
 
Kwahiyo niolewe kwasababu pesa zipo
 
Husiogope watu kukushangaa. Fanya kitu ambacho nafsi yako imeridhia. Ila chondechonde husiolewe naye kwa sababu ya kitu fulani nje ya upendo. Itakusumbua sana.
Asante sana mkuu, nitatafakari kwa kina kabla ya kuchukua hatua
 
Hata ndugu zangu watanishangaa
Husiogope watu kukushangaa. Fanya kitu ambacho nafsi yako imeridhia. Ila chondechonde husiolewe naye kwa sababu ya kitu fulani nje ya upendo. Itakusumbua sana.
Asante sana mkuu, nitatafakari kwa kina kabla ya kuchukua hatua
Vizuri. Amini katika maamuzi unayoyafanya. Kama yanakupa amani ya moyo go ahead. La hasha hayakupi amani ya moyo achanana nayo. Kwa umri ulionao bado una nafasi kubwa yakuamua mustakabari wa maisha yako.
 
Ingekuwa ni yeye ameomba ushauri ningemwambia asikuoe maana kama umempenda usingekuja hapa kuhoji
 
Asante sana mkuu kwa ushauri wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…