Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Pasco. Tunajua unaumia sana pale wafadhili wa Lowassa wanapokamatiwa mali zao za kifisadi. Tulia, dawa ikuingie.
Good Governance wakati mafisadi wanaua nchi? Nyumbu acheni ulofa
 
Pasco umeongea kwa hasira sana ila umesahau watanzania wameteseka na kudhalilishwa sana na leo walau wanaiona nuru ya mabadiliko na matumaini....

wameteswa na hao unaowatetea hapa tena kwa uchungu...unasahau ni wahujumu uchumi hawa...kodi ingesaidia mama mjamzito anayefariki sasa kwa kukosa gari la kumpeleka hospitali ili afanyiwe opereshen ajifungue ila kodi hio imepotea kwa makusudi au uzembe wa hao waliopewa dhamana...

adhabu ya watu hao ilikuwa ni kuwafunga kifungo cha maisha ila wanapewa adhabu ndogo tu ya kuhojiwa mbele za vimada wao waliowajengea majumba kwa pesa zetu...its time for revenge...its time for change...its time to get our revenue to build our nation

aluta continua...hakuna kurudi nyuma.
 
Last edited by a moderator:
Suala Ni Unafiki Wako Mkuu Haujui Unachosimamia,sasa Kama Haupendi Kazi Zake Na Hauzichukii Kazi Zake Unataka Tukuitaje, May Be Fungu La Kukosa Ndio Upande Wako

Huyo Mpuuzi yuko USA kila siku anatusema tunakula vumbi huku alafu bado eti hii nchi anayoitukana inamkosesha usingizi..

Mpuuzi wa Karne... USA Baby :usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2:
 
Hakuna cha ustaarabu tuna kosa kodi kwa uzembe wao na hatimae tunakosa huduma za kimsing
 
Ukiona mtu anamkosoa Rais Dr Magufuli kwa haya yanayofanyika kwenye serikali hii basi ujue ameguswa na huu utumbuaji majipu.
Mfano mdogo tu, unaona watu wanalalamika eti Rais Hataki kusafiri nje ya nchi....watu wa aina hii ni wale wanufaika wa hizo safari. Wamejaa ubinafsi kwa kujali maslahi yao tu bila kujali kama hizo safari je Zina manufaa kwenye nchi.
Poleni sana, vumilieni kwa muda baadaye mtaweza Kupata hizo safari......MLIZOEA VYA KUNYONGA .....PIA MSIZOEE KUSHUKA TU,FAHAMU KUNA KUPANDA PIA , JIANDAENI PUMZI.....
MHE RAIS NA PM PIGENI KAZI NCHI ISONGE MBELE....
 
Pasco. Tunajua unaumia sana pale wafadhili wa Lowassa wanapokamatiwa mali zao za kifisadi. Tulia, dawa ikuingie.
Good Governance wakati mafisadi wanaua nchi? Nyumbu acheni ulofa

Pasco Amelala Anachungulia Chungulia Huu Uzi Kimachale, Nadhan Amewatuma Nyani Babu Na The Boshi Waje Wapime Upepo
 
Ninatamani adhabu ya viboko ingekuwepo pia maana PM angekuwa anawatandika mbele ya waandishi wa habari... Haya mambo ya kuitana faragha na kubembelezana ndiyo yaliendekezwa awamu ya 4 na kutufikisha hapa
 
Mparaganyiko mkubwa
kaenda kwanza kagundua makontena 300
karudi tena kagundua mengine zaidi ya 2000

so inawezekana yakafika hata elfu 10 hajagundua bado
na hakuna namna ya kugundua hadi waziri mkuu aende mwenyewe..
ni kama system ime fail kabisa....waziri mkuu anafanya ukaguzi wa kontena
sio kujenga system mpya yasitokee haya tena

Mkuu ile ni ripoti ya mkaguz mkuu wa serikal ambayo alipewa jk ila hakuifanyia kaz ndo maana serikal hii imeamua kufanyia kaz ripot zote za CAG.

Narudia uchaguzi umeisha,usiyempenda ndo kashinda.
Maguful kasema ye hajasaidiwa hata na mfanyabiashara mmoja kwahyo hana pakulipa fadhira.kuwen wazalendo na mgombea wenu
 
Pasco kwa mfano hao wanaoshtukizwa wangesema ukweli hio karatasi aliokuja nayo ingewadhalilisha?? Wamesema uongo ndio maana anatoa data ili kuthibitisha uongo wao.

Msihangaike na mtoa mada ni moja kati ya jipu lilotumbuliwa so hapo alipo anaskilizia maumivu
 
Last edited by a moderator:
Nimeyafurahia majibu ya wanajukwaa kwabmleta hoja.Hata nyumbani ni baba dhaifu tu anayeweza kuendekeza upuuzi wa wanawe eti kisa utawala bora. Unamkamata mwizi na mali zako unasubiri mahakama ikathibitishe. Moja ya vitu vya hovyo sana tulivyoiga bila kuangalia kasoro sake vilikotoka ni kuondoa viboko hata kwa watoto wetu shuleni. Kisa utawala bora. Mtumishi wa Serikali anaibuka na utajiri wa ajabu kama mafuriko ya mvua haulizwi kapataje,ukihoji unaambiwa una wivu. Au thibitisha kaiba wapi. Yeye athibitishe kavipataje. Umekopa ili uwekeze na kulipa unaulizwa wanatetea utawala bora. Upi? Wa kulinda wezi ? Usipunguze kasi Mh.Majaliwa,wajitetee wakiwa nje ya of is I.
 
Nakuunga mkono huu ni mchezo wa kuigiza, kwanini kama wana ushahidi wasichukue hatua directly kwa hao wakwepa kodi? Hii show yote ni ya nini? Wanawadhalilisha hao watendaji wakati wnajua kabisa order zilikuwa zinatoka kwa nani kupisha baadhi ya hiyo mizigo.
 
Halafu, hao wote si walikuwa kwenye serikali iliyopita?

Manake wanachofanya sasa ni kama kuivua nguo hiyo serikali.

Ina maana walikuwa wanatumikia serikali iliyokuwa imefeli?

Nakuonea huruma sana mkuu unavyojitahidi kukosoa!

Hebu toa mwongozo basi unaoujua wewe selikari hii iongozeje ili wote tujue kwamba wanvyofanya sio!
 
Watu wanataka uchumi wa nchi ukae sawa, tupunguze utegemezi wa kiuchumi, nyie BAADHI mnalilia safari za nje????!!!!. Mlishazoea malipo$$$$ ya safari tu...........poleni sana.
Tulieni kwanza majipu yatumbuliwe kwanza.
 
Huyo Mpuuzi yuko USA kila siku anatusema tunakula vumbi huku alafu bado eti hii nchi anayoitukana inamkosesha usingizi..

Mpuuzi wa Karne... USA Baby :usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2:

Ama Kweli USA inawaaribu hawa watu ukute macheni makali,amesuka minywele eti naye anamshauri Mh Waziri Mkuu,hawa Ndio Hata Vibanda Hawajajenga Vijijini Kwao
 
Hata mimi nilikuwa najiuliza...hivi ni kipi tulichokuwa hatukijui ambacho wao wamekifunua?

Sijapata jibu.

Cheap popularity...
washawachota watu wenye upeo mdogo...
usishanga after two to three years waziri mkuu
akawa 'anavamia' ghafla bandarini na watu wakasifia tena
 
Ni kweli sio good governance kuuliza maswali mfululizo bila kutoa nafasi ya majibu. Ni sawa na mwalimu anamchapa mwanafunzi bila kumpa nafasi ya kujitetea and then anamwambia jitetee sasa halafu mwanafunzi anaonekana hana hatia lakini keshapigwa/dhalilishwa.
 
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomngoa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco

Mkuu umeongea vizuri sana lakini Nafikiri tofauti kidogo na wewe kwa hatua tuliyofikia Tanzanian inafaa waziri Mkuu aende mbali ya hapo haiwezekani wakope pesa nyingi waandike ni kwa ajili ya kufanyia mradi fulani alafu from no where leo unaulizwa unasema ulilipia wafanyakazi mshahara hii hali inatakiwa ibadilike ndo maana viongozi wakuu wanakuwa wakali pili yule anaenda pale Ana fact zote kashaletewa na pale kwenye mkusanyiko wa watu unakuta kuna watu wanaojua iyo issue husika so wakisikiliza majibu ya huku na huko I mean before wanalinganisha wanachuja wanaongeza na zakwao ripoti zinazidi kwenda
 
Mm naomba hata hizo ofisi watu wanajiita haki za binaadam zifungwe kwanza haawa wahishimiwa Rais na Pm wake watutie adabu mpaka turudi kuwa binaadam maana tulijisahau mpaka tukatoka ktk ibinaadam.
Hawezekani mtumishi wa umma anamiliki mijengo mpaka mingine anaisau achilia mbali vimada.
Acha waturudishe ktk ubinaadam tukisha rudi kuwa binaadam ndio ofisi zifunguliwe.
Hivi sasa wazifunge na wakiulizwa kwanini wamezifunga wajibu kiwa tuna rekebishana kutoka kutoka tulipo kwenda kuwa binaadam.
Haiwezekani binaadam akakojoa barabarani haiwezekani binaadam akatupa taka ovyo haiwezekani binaadam akapewa mamlaka ya kusimamia shirika halafu akashirikiana na anaowaongoza kuliibia shirika.
Haiwezekani kiongozi wa taasisi ya umma watumishi wanaliba yeye asijue au ajue asichukuwe hatua hapo hapana binaadam ni wanyama tu.
Mh majaliwa funga ofisi za huyi haki ya binaadam ufanye kazi kwa raha zaidu.
 
Tatzo.watz ni wanafiki mtu akitekeleza majukum.yke eti hana good governance mlitaka,afanyeje hawa wanaiopinga huu utendaji ni wale waliokuwa,wakifaid keki ya,taifa peke yao sasa vitumbua vnaingia mchanga wamezoea kuchezea kodi za wananchi kwa kubadili magari yakifahari kila mwezi sasa mirija inakatwa ndo mana mnalalamija na bdo mtahama nchi.
 
Back
Top Bottom