Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Ile ni public office ina public responsibilities na public wanahitajika kujuwa. Kama kulikuwa na kitu confidential alikuwa amjibu kuwa jawabu la hili suala ni nyeti kwa hiyo nitakujibu tukiwa faragha.

My take: Hii ni kuonesha namna gani hizi nafasi watu wanapeana kwa kujuana. Mtu mwenye elimu yake na aliyobobea kwenye fani yake hakosi jawabu ya kukupa. Inakuwaje Mkurugenzi mzima anamuogopa Waziri Mkuu au Raisi, wakati unajuwa nini unafanya. Kama hawawezi kazi, wajiuzulu kabla ya kaudhirika kama watoto wadogo. Ukimuona mtoto wako karegea regea, unamkamata mabega unamtikisha mwili unamwambia ajikaze.
 
mwaka 2010 walitutukana kuwa elimu bure haiwezekani Leo wanasema inawezekana bado cement na bati kushuka bei....waendelee kuchimba huko kwenye .adini Luna makontene ya madini husafirishwa kinyemela...bado TANAPA
kaka hii nchi unaweza kujiuliza hivi ilikuwa na mtawala kweli? mi nafikiri tupewe credit watanzania kwa kujiongoza wenyewe kwa kipindi hiki chote cha miaka takribani 10.

CHADEMA walikuwa sahihi na bado wapo sahihi kisera - na hizo ndizo hizo JPM anazitumia.
 
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomngoa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco
Kaka nikweli lakini naona acha afanye tu maana hakuna namna nchi hii wenye dhamana walijisahau!pili yote unayoyaona waliyajua kuwa wanafanya vitu ambavyo nakinyume cha utumishi wa umma ila kwakuendekeza matumbo yao binafsi ndo wakaamua kufanya hivyo!!Mh Majaliwa anavyofanya ni sawa kwani hawa siwatu wakuchekea walipolifikisha taifa ni pabaya tena mimi ningewacharaza viboko!!Kuonyesha utawala huu unachukizwa na vitendo vya rushwa!Acha tu mkuu waonyeshwe ili atakayekuja kukaimu ajue cheo chake ni dhamana basi!Na hii nchi ilitakiwa kuongozwa na dikiteta kwa misingi ya sheria baadae!Ila kweli hawa ni manyan'gau walipandisha hata bei za madada wewe unahonga bia yeye anaonga vogue!shenzy type!sasa tutakaa nao mstari mmoja.
 
Mkuu Pasco hayo ni maonyesho. PM angeweza kumwita mtu ofisini na kumweleza aliyogundua, kumpa muda wa kujieleza akishindwa chukua hatua. Sio lazima uite waandishi wa habari ili uonekane unafanya kazi.

Ukweli ni kuwa JPM anajua kuwa hakuchaguliwa na watanzania, na anajua watanzania waliikataa CCM sasa ili ku win watu ni lazima afanye hivyo, ili hata wale ambao hawakumpigia kura wamuunge mkono.

Jana nilimhurumia sana alipokuwa anaongea na wafanyabiashara, maneno "naomba mniunge mkono" ameyarudia kama mara 20 hivi na akahitimisha kwa maneno "yalitopita si ndwele tugange yajayo." Anajua aliokuwa anazungumza nao hawakumuunga mkono wala hawakumpigia kura, anajua jinsi alivyoupata huo urais ndiyo maana ni lazima a - plead huruma ya watu.

Harakati za PM ni jitihada hizo hizo za kutaka support ya wananchi. Anyway tuwape muda tuone jinsi watakavyotuvusha kutoka hapa tulipo.
Yaano watu kama wewe natamani nikupe penseli ya jichoni, chubwiiiiiiiiiii.
Mnatetea ujinga.
 
Wizi wa wachache ndo umesababisha yote haya. Hacha mkuu afanye kazi yake.
 
Kwa kweli kwa hali tuliyonayo, mimi namsamehe Waziri mkuu. ndhani lengo la kufanya hivi ni kutoa ujumbe kwa wakuu wote wa mashirika na idara, kwamba wawe makini. waelewe details za mambo yanavyokwenda katika maeneo yao. tunatoka katika mfumo wa ulegelege, na tunapenda kuwa katika mfumo wa kuchapa kazi. sasa tunakwendaje? kama akifanya "kikao cha management" kama unavyosema, itabidi wapite mashirika yote kufanya hayo hayo. lakini hii wanayofanya ni sawa na kwenye gwaride afande ananyoosha mstari kwa kutumia risasi. atafanya hivyo mara moja tu. mara nyingine risasi haitampata mtu! kila mtu atajipanga usawa kulia na mstari utanyooka nyuzi tisini ndani ya sekunde tu. tuna matatizo mengi sana kwa hiyo tukubali maumivu ya operesheni na kuuguza majeraha ya upasuaji. lengo letu ni kupona
 
Ndugu naona unatupa lawama pekee kwa hii serikali bila kusema badala yake ilitakiwa kufanya nini kwa ilichokikuta kinaendelea kwenye bandari. Ok let's say wamesuka mfumo mpya wa kuiendesha bandari na kuisimamia kwenye mapato ila bado wanasubiri sheria maybe ipitishwe na bunge au vipi labda. Je wakati wanashughulikia uundwaji wa huo mfumo, ilitakiwa waache hizo pesa zinazopotea ziendelee kupotea mpaka huo mfumo uwe tayari ? Ilitakiwa waache kilichokuwa kinafanyika kiendelee au mimi ndio siwaelewi nyie mnaokosoa kila atachofanya?

Raia Mwema - Hapa kazi tu na utendaji kazi wa staili ya jeshi la mtu mmoja
 
Mleta mada mambo ya michakato ndio yaliyotufikisha hapa tulipo hivi sasa ni ubandidu tu Ili mambo yaende
 
Wao wamewadhalilisha kiasi gani watanzania kwa kuwaibia.Mangapi yameharibika katika maisha ya watanzania kwa wizi huu.Hawastahili heshima watu hawa hata kidogo.Na bado.Magufuli and Majaliwa keep it up.Asiyetaka kudhalilishwa aache kuiba.It is as simple as that.
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomngoa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco
 
Si kweli kama unavyotaka kuudanganya Umma,usifikiri walioshiriki vitendo hivyo vya kihalifu ni watu wepesi,vitendo hivyo vimefanywa na vigogo wa Serikali kupitia Kampuni zao.Kama sheria ingefuata mkondo wake,sakata hili lingeiacha uchi serikali yenyewe.

Kitendo cha kuwapa muda wakalipe kodi ni kusalimu amri baada ya kugundua wahusika wa sakata hilo ni watu wazito wasiogusika.Mh Pinda alishawahi kukiri hadharani kuwa wanaofanya vitendo vya ufisadi ni watu wazito ambao ukiwagusa nchi itayumba.

Zilikuwa ni kelele tu,wenye nchi wamempa onyo la kuacha kufukua "makaburi ya ufisadi" kuendelea kufukua makaburi hayo kungeweza kusababisha uchafu wa watangulizi wake ujulikane na kushusha kuaminika kwao.

Zipo wapi bilioni za EPA tulizoambiwa zilirudishwa na wezi?Tuliishia kuambiwa tu kuwa zilirejeshwa bila kuambiwa zilirejeshwa ngapi.
Mkuu ZILLAHENDER, tuneno twako tumesimama wima na vizuri sana. Sijui ni wadanganyika wangapi watakuelewa kwa sasa!

Acha kutetea upuuzi...
Good governance kitu gani bwanaa..ukishakuwa top wa sehemu, u should have all the info at your fingertips..
Go Magufuli go, Go Majaliwa go.
 
Hakuna namna nyingine ya kuwakomesha watanzania wavivu wazembe na wala rushwa kuliko wanavyofanya wakuu sana. Tena wanapaswa kuongeza kasi zaidi.

Wewe umenyanyasika kutokana na uzembe wa watu hawa halafu leo unawaonea huruma?! au ni baba yako yule? Hapa kazi tu.
 
Anachokifanya PM Majaliwa My Mate UD ni sahihi kwa muktadha wa nchi ilipofikia. Ustaaarabu hakuna, sheria zipo mifukoni, ni ubabe, unyanyasaji na kila aina ya udhia , dawa ni kama wanachokifanya , vile vile ni kuweka pace ya watakaowatweua ili waone namna ya kufanya kazi.
Je mbaona walimu kule sekondari na msingi wanakaguliwa pasipo kuambiwa kuwa wakaguzi waja?
 
Mkuu pasco siyo good governance sawa,lakini na hawa watendaji ni kama hawajielewi hivi,yaani libaba lizima linaulizwa maswali linaanza kutetemeka ,,lol
Sio libaba. Ungekuwa wewe nadhani ungejinyea moja kwa moja. Katika utawala bora huwezi kumuuliza mtu maswali tena ya skendo ya siku nyingi ukategemea akupe majibu hapo kwa hapo. Huo ni uonevu. Anapewa muda nae aangalie makabrasha yake atoe majibu. Kwani huyo PM si alijiandaa? Tuache ushabiki
 
Kwaaaaanza, Mh. Waziri Mkuu anawafanyia ustaarabu mkubwa sana; ningekuwa mimi, ningewanyoosha zaidi ya wafanyiwavyo. Mh. Waziri Mkuu na Mh. Rais wanapiga kazi halafu wewe, The Boss na wengine mnaofanana nao kimtazamo mnatuletea Theory za Management za kipuuzi kabisa!!! Hizo Theory hazitekelezeki kwa Africans tuliojaaa ulaghai mwingi na kuzungumza yale ambayo hayapo mioyoni mwetu: waachieni Wazungu huko watekeleze ma-theory yao huko huko kwao, sisi Hapa ni Kazi Tu. Nasema, wanabahati mimi siyo PM wala Rais; ningewanyoosha zaidi. Hivyo vi-theory vyenu vya Management pelekeni Msoga.
 
Na wewe naye

Umekumbuka maisha ya ndoa leo kumekucha, hii ni kwamba vijibahasha haviji.

Wengi michepuko hawana muda nao pesa hakuna na wanaishia kukumbuka nina mke na nimwekee heshima leo nimtaje ajulukane maana michepuko yote imeyoyoma

Yaani ni shida haswa, pole nimekuwa nikiona nguvu yako ya kumponda muheshimiwa na makamu ila umekuwa kama unapewa pembeni kuja kuchafua.

Pole yenu na hao wawili humu na wale wachache

Sie furaha, hadi huku Tand./Mbaga. tunasherekea

Wakiulizwa wanauma meno, y kuwapa muda. Eeh waunde bodi sijui nini hakuna hiyo wakiona vipi waache kazi.
 
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomngoa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco

Aisee wewe unaishi nchi gani? Kama ni Tanzania basi una lako jambo. Baada ya miaka hamsini ya tabia hatari ya watendaji wetu unathubutu kusema waziri mkuu awashughulikie kistaarabu? Nadhani wewe ni moja ya wale watanzania ambao hawajayaonja kabisa machungu ya halaiki ya watanzania ambao wameishi kama wafu kwenye nchi yao. Unaandika sana pasco lakini kwa hili umebuma. Watu walisali apatikane kiongozi wa kuwachapa kabisa halifu wewe unamlaumu waziri mkuu ambaye anawahoji wazi ili kwa mara ya kwanza watz wafahamu nani alikua shetani wao? Bro hutaeleweka.
 
Back
Top Bottom