Anachokifanya Rais Magufuli kingefanywa na Rais muislam basi angekosolewa vikali

Status
Not open for further replies.
Wakristo ni wabinafsi sana, kipindi cha JK matamko toka kwa wachungaji yalikuwa mengi sana,lakini mkuu alikuwa hazungumzi chochote ,au wale wachungaji wa kipindi cha JK waliondoka?
Lakini wakati huu wa Jiwe waislam ndio hawalalamiki kabisa maana Jiwe alishawajulia shida yao ni ni kujengewa misikiti, pesa na ubwabwa.

Wako kimyaaaa kuliko hata hao wakristo.
 
Hayo yakumpenda Mungu na atwambie kila mwezi kupitia runinga ya taifa, mbona wenzake walikuwa wanalihutubia taifa kila mwezi live. Hakatazwi kwenda kanisani kusali na aende kila siku ila hakuna haja yakufanywa kama ni shughuli ya Serikali.
Udini unaozunguziwa unajidhihirisha wazi kwa hii tabia yake ya kila j2 kufanya siasa kanisani, huku ni kuwagawa watz.
Waraka wa shura ya maimamu ulizungumzia kwa evidence kabisa teuzi 70% kwa 30%.
 
Bado kampeni zikianza ataanza na zile salamu zake za kikabila huko mikoani atakakokuwa akipiga kampeni, kisha akifika kule kwao kanda ya ziwa hata Kiswahili atakisahau na kukampeni kwa kilugha cha kwao ili kuleta hisia za kikabila. Huu ni upuuzi usiomithilika.
 
Huu uzi mpaka Bi mkubwa Faiza foxy aingilie kati sijui kapotelea wapi siku hizi
 
Kwanza naomba nikupongeze kwa uzalendo wako kwa taifa lako. Udini ni changamoto ya kinadharia ambayo inaanza kushamiri vichwani mwa watanzania kutokana na kupungua kwa umakini kwa wale tunaowapa dhamana ya uongozi.

Kama hili unalolizilungumzia mimi pia huwa linanikera sana kwakweli. Sababu nikiwa kama mtanzania na ninatazama na kuweka mbele masilahi ya taifa langu ni vema tukajifunza kanuni na misingi ya kuishi kwa umoja bila kuwafedhehesha wengine.

Jamii yetu ni mchanganyiko wa tamaduni, imani, fikra, umri, kada, status, jinsia, na tofauti zingine nyingi zaidi. Tukiishi kwa mipaka ndio kuheshimiana kwenyewe.

Hii kitu huwa inanikwaza sana, utaona viongozi wanatumia madhabahu na nyumba za ibada kama sehemu ya kuvuta hisia za wanainchi ili wawaaimini bila kujua wanajenga hisia za ukakasi juu ya uadilifu wao.

Baba wa taifa, J. K. NYERERE, alishawahi kuweka bayana katika moja ya hotuba zake kuwa, ukiona kiongozi anatumia chama, udini, ukabila, au kundi /makundi kuwasilisha na kuwakilisha hoja zake jua huyo kiongozi amefilisika sera na sasa anatafuta uhalali wa kisiasa ili aweze kupata sapoti ya wale anaowalenga.


Kimsingi viongozi wa CCM wanafahamu maovu yao wazi wazi na hivyo wamekwisha jua kuna gharama kubwa sana kwa upande wao kuyarekebisha ndio maana wameamua kama mbwai iwe mbwai wanaendelea kuishi na sisi kibabe na kwa sera cheap na zisizo na mashiko kama hizo za kiimani.
 
SIna nia ya kupinga ulichoandika lakini naamini haujaelewa maana halisi ya maandiko matakatifu uliyoyanukuu.
Ukweli au truth unaoengelewa hapo ni kuhusu Kristu ni nani na dhana nzima ya Gospel/ Injili.
Kwa kifupi ulichokipinga umemalizia kwa kukiunga mkono.
 

Matthew 28: 19-20
Therefore go and make disciples of all nations...

Nakukumbusha tu apa ilimaanishwa ni Yale mataifa kumi na mbili ya Israel na sio ulimwengu (world).

Al Takwir ( 81:27 ) Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.

Soma uelewe sio unameza tuu
 
Wewe hujaelewa hoja kabisa.
Umedandia hoja na kuandika hisia zako.

Mleta mada hana tatizo na imani ya kidini aliyonayo Magufuli, bali ana tatizo kuona imani ya kidini ya Magufuli (ukristo) kutumika kirejareja kama imani rasmi ya kiserikali, wakati Tanzania tuna dini tofauti tofauti.

Nchi yetu haina dini, na katiba inatamka hivyo, sasa rais wa Tanzania hapaswi kulazimisha watu wote waamini katika Mungu wakati kuna watanzania wengi hawaamini kuhusu Mungu, ama wana mtazamo tofauti kuhusu Mungu.

Embu waza tu, Rais angekuwa muislamu halafu awe anafanya mambo ya imani ya kiislamu kama ndio msimamo wa kiimani wa Tanzania. Wewe kama mkristo ungefurahia?

Vipi Rais angekuwa mpagani au muumini wa ushirikina, halafu jambo hilo alifanye la kitaifa?
 
Absolutely mkuu.
 

Eeh eeh hebu rudia tena sijasikia. Mbona Mwl ndiye anaye laumiwa sana na wasomi wa kiislamu wa miaka ya 1950-1980s kuwa aliwaonea Waislamu kwa ubaguzi wa elimu. Ziko maada hapa JF zenye hizo lawama.
 
Tutafute pesa, tuzaane, tuzeeke, tufe kisha tusahaulike katika uso wa dunia.

Hizo dini zenu za kuletwa na wakoloni bado zinawatala kifikra.
 
Uliona matangazo ya SGR ama Meli ziwa Nyasa, Victoria, Tanganyika, au Treni ya mizigo ikiwasili Arusha enzi za Mh Kikwete.? Kila jambo na wakati wake na kusudi katika kila majira.
Umetoa utetezi mfu. Matangazo ya SGR, treni ya mizigo Arusha na meli yasingetolewa na Kikwete wakati sio rais wa awamu hii. Yani unataka Obama atoe matangazo juu ya mapambano ya covid-19 Marekani wakati POTUS wa sasa ni Trump?

Kwa hiyo unalinganisha kutangaza miundombinu na kutangaza dini.
Rais wa nchi akitangaza miundombinu itatumika na watu wote na wale wasio na dini, na wasio amini kama dini ipo. Rais akitangaza dini tena kurugenzi ya ikulu na TBC wanatangaza haya ni matumizi mabaya ya vyombo vya umma. Ni sawa na jeshi kuimba nyimbo za CCM as if nchi ina chama kimoja.

Wanaokubaliana na hili ni washamba wakubwa. Na wale mnaosema sijui mcha Mungu sijui ana hofu ya Mungu mnatumia SI Unit gani? Kwani Charles Taylor na Pierre Nkurunziza nao si walikuwa wakesha kanisani tena wanahubiri, achana na huyu anayeenda kusali tu.
 
Hapa kama ni kumlaumu ni Kurugenzi ya mawasiliano ikulu kwani sidhani kila anachofanya Rias au kila anapokuwepo rais ni yeye moja kwa moja anawataka wampe covarage.
Kwa upande mwingine, sio aibu kuwa muumini wa dini iwayo yote maadam mtu hajavunja sheria.
Tunakuwa watu wa ajabu sana pale ambapo mtu ameingia kanisani kuomwomba Mungu alimuumba halafu mtu mwingine aone ni kero.
Mara ngapi nyakati za ijumaa au nyakati za Idd El Fitir TV zinaonesha swala au maidha ya Kiislamu na hatupati kero?

Kumheshimu mtu anaekwenda kumwomba Mungu aliemuumba ni jambo kubwa sana na hata wimbo wa taifa una mstari unasema "Mungu Ibariki Afrika.... Mungu Ibariki Tanzania"

Nampongeza Rais kwa kumtegemea Mungu na kumwomba Mungu na imani yake kwa Mungu na ujasiri wake kumtegemea Mungu, Tanzania tumevushwa kwenye janga la Covid19 na majanga mengi.

Naendelea kuamini, Rais hajakosea kwenda kanisani, na kwa mtu kuona picha/taarifa anakereka kwa Rais kwenda kanisani kwa kuwa ni Mkisto na hakuwa anahubiri injili ili watu wageuzwe kuwa wakristo, basi ninazidi kushangaa
 
Tatizo hata BAKWATA yenyewe haijitambui imekuwa kama shina la CCM

BAKWATA ndicho chombo kikuu kitumikacho kuwagawa waislamu. Kipo pale kimkakati
Waislamu wakipaza sauti zao kupinga jambo, baada ya siku chache BAKWATA wanatoa tamko la kuipongeza serikali kwenye jambo jingine, Ilimradi tu kukwamisha juhudi za waislamu kupata haki na usawa

Kwa mfano Sheikh Ponda alisoma waraka majuzi, lakini Kesho Shehe Mkuu wa Dar es salaam kaandaa kongamano la viongozi wa dini kumpongeza Magufuli anavyotawala. Kwa hiyo unaweza kuona jinsi BAKWATA ilivyo pandikizi kwenye jamii ya waislamu nchini ili iwe nyapara w watawala kuwakeep incheck waislamu wasifurukute!
 
Mie ni Mkristo Mkatoliki siyo wa kuzaliwa tu bila wa imani. Naipenda sana dini yangu, na ninaamini ni sahihi kuliko zote, na nina hakika na wenzangu wengine wa imani tofauti ndivyo wanavyoamini kuhusu dini zao.

Kama muumini wa mafundisho ya dini yangu, bila ya kujali tofauti yoyote ile, ninaamini kila mwanadamu ameumbwa kwa mfano na sura ya Mungu. Nikitaka kumwona Mungu natakiwa kumwangalia aliye karibu yangu bila ya kujali huyo aliyepo karibu yangu ni muislam, mhindu au awaye yeyote.

Kutomtendea haki mwanadamu yeyote hata kama ni wa dini gani ni dhambi. Kuwa mnafiki ni dhambi mbaya zaidi.

Kuna mambo ya msingi ambayo mleta hoja ameyasema, na ninayakubali kwa asilimia kubwa. Kwa ujumla, mambo mengi yaliyopo nchini mwetu na katika mataifa mengi yameegemea kwenye desturi za Kikristo. Waislam wamekuwa na subira sana katika hilo. Lakini sisi tumekuwa sensitive sana kwa mambo madogo yakifanywa na kiongozi muislam.

Nakumbuka wakati wa Kikwete, akiteua viongozi 6, waislam wakawa 4 na wakristo 2, lazima minong'ono, miguno na hata lawama zitoke kuwa anawapendelea waislam. Lakini leo Rais mkristo, hata akiteua viongozi 8, muislam akawa 1, waislam wanavuta subira.

Leo, Rais Magufuli anaenda kutoa ujumbe kwaajili ya Taifa akiwa ndani ya kanisa, mbele madhabahuni. Waislam wanavuta subira. Jambo hilo siyo mara 1 au mara 2.

Kuna mambo makubwa tunatakiwa kujifunza:

1) Taifa huwa salama na mshikamano kunapokuwepo na subira ambayo ni sehemu ya hekima

2) Viongozi wanatakiwa wawe na hekima ya kujitahidi kutoamsha hisia za udini, ukabila, uchama na ukanda. Kauli nyingi za Rais Magufuli (kama zile za wa Mwanza wasivunjiwe nyumba, wapinzani watavunja madaraja, huu ni wakati wa kujenga maeneo mengine, wenzetu wa kaskazini wasubiri, n.k.) ni za kupalilia chuki na utengano

3) Ukipenda kuvumiliwa ujitahidi kuvumilia

4) Makuzi, malezi vina mchango mkubwa sana wa kumtengeneza mtu. Ndivyo vitu huchangia mtu kuwa wa namna gani hapo mbeleni. Viongozi waislam inaonekana wanakuwa na utu sana, wanathamini zaidi ustawi wa watu. Sijui jambo hili ni kwa bahati mbaya au linatokana na malezi wanayoyapata kwenye dini na jamii zao!

Ukiwaangalia viongozi wetu kwa kipimo cha uvumilivu, kama utataka kuwa mkweli wa nafsi yako, ni viongozi waislam ndiyo wanaoongoza kwa uvumilivu. Walinganishe Mwalimu, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli.

Uvumilivu ni utayari wa kusamehe. Mafundisho ya kikristo, tunafundishwa sana juu ya upendo, msamaha na kusaidiana LAKINI kwenye uhalisia kuna mashaka makubwa kama tunayaishi.

Wakati wa Kikwete, nyaraka za Kanisa na matamko ya Kanisa havikuwa haba, japo kiuhalisia hakukuwa na uvunjwaji mkubwa wa haki za binadamu kama awamu hii au awamu ya Mkapa. Unajiuliza, je, viongozi wetu wa dini huwa wana mahaba makubwa ya dini kuliko mahaba ya upendo wa kweli kama Mungu alivyoagiza?

Ni nje ya mada midogo - lakini inatafakarisha!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza, "Wewe ni mujahidin"
Pili umejawa na Chuki,

Tatu, Kikwete na Mwinyi wote walikuwa waislamu.
Nne, Magufuli alishasema hapangiwi, sasa kama unatka rais wa kupangiwa, subiri ucvhaguzi oktoba uchague huyo umtakaye, kuna waislamu wengi tu wanagombea.

Tano, Swala za msikiti haziruhusu kuzungumza tu, maana huwa ni za muda mfupi mfupi.

Si kweli kwamba kuna mfumo kristo, hizo ni hadithi zako, na inferiority complex yako, hakuna sensa iliyofanyika kutaka kujua idadi ya waislamu na wakristo walioajiriwa kwenye ofisi za umma.
Mbona hujagusia Bharesa kuajiri waislamu tu karibu kila idara kwenye makampuni yake?
 
Waislamu wanatakiwa waanze na BAKWATA kwanza
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…