Mkuu Rose Mzalendo, nadhani wewe ni kada mwenzangu wa chama chetu, uzalendo wa kweli sio kujiita mzalendo bali kuwa ni mzalendo wa ukweli. Mzalendo wa ukweli kwanza yeye mwenyewe atakuwa ni mkweli, na ataibua hoja za ukweli anaoujua.
Japo mimi ni kada lakini nakiri Lissu ni maarufu na zile pingamizi zake ni valid kisheria ila ni voidable na sio void. Ili kujua kuwa kweli ni voidable subiria picha za mgombea urais kwenye karatasi ya kura if it's the same.
Ombi kwa Tume yetu ya Taifa ya Uchaguzi, naomba makosa mengine yote madogo madogo kwenye ujazaji fomu ambayo sio void bali ni voidable kwa wagombea wote, yawe tolerated na waruhusiwe kurekebisha wapitishwe!
P