Ukitafakari sana, bila kuwa na utando wa kishabiki kichwani, Lissu anaongea kitu cha maana na hapa tayari ameonyesha ku-compromise na CCM.
Pendekezo lake la "No Reforms na Elections" kwa alivyofafanua na nikamuelewa, anasema kwamba, Chadema wako tayari CCM iendelee kuwa madarakani kwa muda ulioongezwa, yaani Samia na Wabunge waendelee kuwa madarakani, hadi Reforms zikamilishwe. Zikishakamilishwa basi ndipo sasa ipangwe Bunge livunjwe lini na Uchaguzi Mkuu ufanyike lini, labda October 2026 badala ya October 2025, au hata October 2027. Yaani Wabunge na Raisi waongezewe kipindi cha mwaka mmoja, hadi miwili ikibidi, ili kufanya Reforms.
Sasa mimi nadhani kwa mtu mwenye kufikiri, hili si wazo baya, ni wazo la mtu mwenye akili na alie tayari kutafakari. Amesha-compromise.
Kwa upande wa pili ina make sense. Kwa nini uingie kwenye uchaguzi ambao unajua unafanyika katika misingi mibovu? Ni vema uahirishe uchaguzi ili urekebishe hiyo misingi mibovu kwanza.
Na hii ni lojiki ya kawaida ya maisha ya kila siku. Nikitaka kusafiri kesho, huku nikitambua gari nitakayotumia ni mbovu itanikwamisha njiani, basi ni vema nicheleweshe safari ili gari irekebishwe kuliko kusema ngoja niende tu nitafanya cha kufanya huko mbele. Unaweza ukafia njiani.
Sasa CCM msipoelewa hili nyie ni wakorofi na mnafanya makusudi kwa sababu hamtaki Reforms
Hebu Wasira katika busara za uzee wake atuambie ubaya wa hili wazo ni nini?
[/QUOTE
Tena kweupe pee jamani.