Anachosema Lissu ni kwamba, Bunge lisivunjwe mwezi wa sita, Rais na Wabunge waendelee hadi Reforms zikamilishwe, ndio uchaguzi mkuu ufanyike

Anachosema Lissu ni kwamba, Bunge lisivunjwe mwezi wa sita, Rais na Wabunge waendelee hadi Reforms zikamilishwe, ndio uchaguzi mkuu ufanyike

Ukitafakari sana, bila kuwa na utando wa kishabiki kichwani, Lissu anaongea kitu cha maana na hapa tayari ameonyesha ku-compromise na CCM. Nimesikiliza mahojiano yake kwa makini sana.

Pendekezo lake la "No Reforms na Elections" kwa alivyofafanua na nikamuelewa, anasema kwamba, Chadema wako tayari CCM iendelee kuwa madarakani kwa muda ulioongezwa, yaani Samia na Wabunge waendelee kuwa madarakani, hadi Reforms zikamilishwe. Zikishakamilishwa basi ndipo sasa ipangwe Bunge livunjwe lini na Uchaguzi Mkuu ufanyike lini, labda October 2026 badala ya October 2025, au hata October 2027. Yaani Wabunge na Raisi waongezewe vipindi vyao vya sasa, labda mwaka mmoja, hadi miwili ikibidi, ili kufanya Reforms.

Sasa mimi nadhani kwa mtu mwenye kufikiri, hili si wazo baya, ni wazo la mtu mwenye akili na alie tayari kutafakari. Amesha-compromise.

Kwa upande wa pili ina make sense. Kwa nini uingie kwenye uchaguzi ambao unajua unafanyika katika misingi mibovu? Ni vema uahirishe uchaguzi ili urekebishe hiyo misingi mibovu kwanza.

Na hii ni lojiki ya kawaida ya maisha ya kila siku. Nikitaka kusafiri kesho, huku nikitambua gari nitakayotumia ni mbovu itanikwamisha njiani, basi ni vema nicheleweshe safari ili gari irekebishwe kuliko kusema ngoja niende tu nitafanya cha kufanya huko mbele. Unaweza ukafia njiani.

Sasa CCM msipoelewa hili nyie ni wakorofi na mnafanya makusudi kwa sababu hamtaki Reforms

Hebu Wasira katika busara za uzee wake atuambie ubaya wa hili wazo ni nini?

Angalia pia: https://www.jamiiforums.com/data/video/5939/5939319-d39f72b02cc4e8f343ca921586c9ac51.mp4
Asilimia kubwa ya watanzania hawawezi kuelewa lojik hii ya lisu Kwa sbb ya uwezo mdogo wa kutafakari, lkn Kwa upande wa CCM pia, wao jambo wazo lolote linalotoka Kwa lisu hata kama linaenda kufuta umaskini wa nchi Kwa haraka, haliwezi kupokelewa, na ni wazo baya kuliko mawazo yote! Ukiachilia mbali kwamba hawako tayari kwa reforms ya aina yoyote ambayo itatengeneza mazingira ya usawa kiushindani kwenye CHAGUZI
 
Asilimia kubwa ya watanzania hawawezi kuelewa lojik hii ya lisu Kwa sbb ya uwezo mdogo wa kutafakari, lkn Kwa upande wa CCM pia, wao jambo wazo lolote linalotoka Kwa lisu hata kama linaenda kufuta umaskini wa nchi Kwa haraka, haliwezi kupokelewa, na ni wazo baya kuliko mawazo yote! Ukiachilia mbali kwamba hawako tayari kwa reforms ya aina yoyote ambayo itatengeneza mazingira ya usawa kiushindani kwenye CHAGUZI
Well
 
Jibu la tundu Lissu ni kwa wale wanaodai wako Tayari kwa Katiba Mpya ispokuwa muda ndio kikwazo.

Lakini kwa wanafiki hilo bado litakuwa gumu kwao
Kwani hujui kuwa hiyo habari ya "muda ndiyo kikwazo" ni geresha tu?

Lissu naye hajui hilo?
 
CCM wakigima kufanya reforms katika huo mwaka mmoja au miwili napo itakuwaje?

Waongezewe miaka miwili mingine bila uchaguzi?

Na hapo napo wakikataa tena?
Vilio vitasikika kila kona ya nchi.
 
Kwani hujui kuwa hiyo habari ya "muda ndiyo kikwazo" ni geresha tu?

Lissu naye hajui hilo?
Ndio maana amewapa another alternative ili kikwako hicho kipungue.

Since 2022 it has been same song. Time time time
 
Ndio maana amewapa another alternative ili kikwako hicho kipungue.

Since 2022 it has been same song. Time time time
Another alternative ipi? Na unafikiri kwa nini wataifuata? Na wasipoifuata atafanya nini?
 
Lissu anataka Samia aongezewe muda?

Hii mbona kama sio bahati mbaya, kuna nini nyuma ya pazia?
Nmefuatilia hii video na kwa hakika hakufatwa kuhojiwa tu bali waandishi hawa walitumwa. Kwsbb maswali yote aliyohojiwa ni swaala hilo tu lilichokua takriban dkk 40 na kuwekwa swali la mwisho na kwanini mwandishi akamhoji sana na kusisitiza zaidi hapa.

Kwa ujumla kauli ya lissu n kuwa chadema na wanachadema hawatashiriki uchaguzi mpaka reform (mabadiriko ya katiba) yafanyike. Na akaulizwa yuko tyr kukutana na ccm akagoma, mwenyekiti wa chama cha ccm akagoma, wasila akagoma na maelezo yake ni anahitaji kukutana na raisi mana ndio mwenye nguvu na kauli ya kusema reform ifanyike. Na reform sio maelezo n katika ifumuliwe au mchakato mzima, utaratibu, upatikanaji na uundwaji wa tume sio ubadirishwe ni uunde upya.

Kwa ujumla n kwamba yeye anataka kubadirishwe namna ya kuundwa kwa tume ya uchaguzi na jinsi wajumbe wake wanavyopatikana lkn iwe kwa maandishi ndani katiba.
Na hivyo yuko radhi muda wa raisi uongezwe ila bunge lisivunjwe libakie kurekebisha katiba hasa kipengele hiko cha uchaguzi. Simple

Najua watakuja wapotoshaji baada ya hili
Link ya mahojiano ni
View: https://www.youtube.com/live/upsvyyFMpu8?si=4yURPwNy-f4wn5gl
 
Mambo sio magumu kama unavyofikiria. Kusogeza mbele uchaguzi ni jambo linalofanyika kirahisi sana, linapitishwa na Bunge na kunakuwa hakuna ukiukwaji wa Katiba. Hata kwa tamko la Raisi uchaguzi unaweza kuahirishwa, kwa mfano akitangaza hali ya hatari kwa sababu nchi iko vitani au kuna Covid nk. Kwa hiyo usiwaze mambo ambayo hayapo

..Naunga mkono 100% maoni yako.

..Mabadiliko ya Katiba yatakayowezesha kuunda Tume Huru yanaweza kufanyika ndani ya mwaka mmoja na uchaguzi ukafanyika 2026.

..Uchaguzi wa Zanzibar umewahi kuharibiwa, na kulazimishwa kurudiwa 2016, hivyo hoja kwamba uchaguzi hauwezi kuahirishwa haina mashiko hata kidogo.

..Tunaweza kuamua uchaguzi ufanyike 2026 lakini awamu ijayo iishie 2030, na tuendelee na kalenda yetu ya uchaguzi iliyopo sasa hivi.
 
Natamani kushiriki maandamano yatakaoongozwa na Lissu siku hiyo takwa lake litakaposhindikana
 
Reforms sio lazima mabadiliko ya katiba.
 
Natamani kushiriki maandamano yatakaoongozwa na Lissu siku hiyo takwa lake litakaposhindikana
Ikishindikana watu waandamane JWTZ wapindue nchi kwa miaka miwili ya kutengeneza Katiba!
 
Nimelisoma. Nachoona Lissu anataka Samia n bunge la CCM waongezewe muda ili tupate katiba mpya. Sielewi kwa nini anataka utawala wa CCM uongezewe muda.

..kuna hoja kwamba muda hautoshi kuunda Tume Huru ya uchaguzi kabla ya October 2025.

..sasa Lissu ndio ametoa wazo kwamba tunaweza kuahirisha uchaguzi ili tupate muda wa kufanya mabadiliko ktk Tume ya uchaguzi.

..kinachopaswa kufanyika ni kumhoji zaidi anapendekeza mabadiliko yapi katika Tume.

..pia aulizwe anapendekeza uchaguzi uahirishwe kwa muda gani?

..Nadhani Mama Samia anapaswa kulichukua wazo hili. Kwa maoni yangu atakuwa ameuwa ndege wawili kwa jiwe moja.

..Hakuna atakayemlaumu kuwa ana tamaa ya madaraka kwasababu wazo limetoka kwa mpinzani wake. Pia atajijengea heshima kama mwanademokrasia wa kweli na mpenda mabadiliko. Vilevile atapata muda wa kujiiimarisha na kujiandaa zaidi kwa ajili ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom