Anachosema Lissu ni kwamba, Bunge lisivunjwe mwezi wa sita, Rais na Wabunge waendelee hadi Reforms zikamilishwe, ndio uchaguzi mkuu ufanyike

..kuna hoja kwamba muda hautoshi kuunda Tume Huru ya uchaguzi kabla ya October 2025.

..sasa Lissu ndio ametoa wazo kwamba tunaweza kuahirisha uchaguzi ili tupate muda wa kufanya mabadiliko ktk Tume ya uchaguzi.

..kinachopaswa kufanyika ni kumhoji zaidi anapendekeza mabadiliko yapi katika Tume.

..pia aulizwe anapendekeza uchaguzi uahirishwe kwa muda gani?

..Nadhani Mama Samia anapaswa kulichukua wazo hili. Kwa maoni yangu atakuwa ameuwa ndege wawili kwa jiwe moja.

..Hakuna atakayemlaumu kuwa ana tamaa ya madaraka kwasababu wazo limetoka kwa mpinzani wake. Pia atajijengea heshima kama mwanademokrasia wa kweli na mpenda mabadiliko. Vilevile atapata muda wa kujiiimarisha na kujiandaa zaidi kwa ajili ya uchaguzi.
Mkuu umejibu kwa lojiki ambayo sidhani kuna wengi ndani ya CCM wanaweza kuielewa. Hapo ndio tatizo. Mie ndio maana nasema, dawa ni JWTZ kuchukua nchi na kuamrisha Reforms zifanyike, na baada ya miaka miwili kurudisha nchi kwenye utawala wa kiraia. Kwisha. Hawa wazee wa CCM bila viboko hawawezi kusikia wala kwenda. JWTZ wamuulize Traole wa Burkina Faso atawaelimisha nini cha kufanya kwa viziwi na watu wenye shingo ngumu kama CCM.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 CCM wakubali maridhiano ambayo yatawaondoa wao meza kuu😄???
Sidhani kama litakuwa jambo rahisi.

..utawaondoaje CCM meza kuu?

..hawa watu wanapokea 3.2 BILLION kila mwezi kama ruzuku toka kwa msajili.

..wakati huohuo washindani wao wa karibu hata kulipa posho ya wajumbe wa mkutano mkuu hawawezi.

..binafsi sielewi kwanini CCM wanaogopa mabadiliko wakati wana advantage za kila aina dhidi ya washindani wao.
 
Swa kabisa - hizi ni sheria, taratibu na kanuni zinazohusu uchaguzi. Ndani ya mwaka mmoja zinaweza kuwa tayari. Kubadili Katiba ni sualala muda mrefu zaidi. TAL anaongelea Reforms za uchaguzi, sio Katiba mpya
Wengi hawajui kwamba suala la Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia uchaguzi na kura za urais kutohesabiwa katika kituo zilipopigwa kura sio hata matakwa ya katiba. Ni mambo yanayowezwa kubadilishwa wakati wowote.
 
..kuna hoja kwamba muda hautoshi kuunda Tume Huru ya uchaguzi kabla ya October 2025.

..sasa Lissu ndio ametoa wazo kwamba tunaweza kuahirisha uchaguzi ili tupate muda wa kufanya mabadiliko ktk Tume ya uchaguzi.

..kinachopaswa kufanyika ni kumhoji zaidi anapendekeza mabadiliko yapi katika Tume.

..pia aulizwe anapendekeza uchaguzi uahirishwe kwa muda gani?

..Nadhani Mama Samia anapaswa kulichukua wazo hili. Kwa maoni yangu atakuwa ameuwa ndege wawili kwa jiwe moja.

..Hakuna atakayemlaumu kuwa ana tamaa ya madaraka kwasababu wazo limetoka kwa mpinzani wake. Pia atajijengea heshima kama mwanademokrasia wa kweli na mpenda mabadiliko. Vilevile atapata muda wa kujiiimarisha na kujiandaa zaidi kwa ajili ya uchaguzi.
Kuna mabadiliko yanayoweza kufanyika bila hata bunge kuhusika mfano kuwaondoa Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia uchaguzi.
 
Sifa za Tume huru ni zipi?

..Sifa za Tume Huru kwa uchache zipo ktk namna wajumbe wake wanavyopatikana, namna bajeti yake inavyopatikana, na namna maamuzi yake yanavyolindwa na Katiba.

..hivi unafahamu kwamba Wenyeviti wa Tume za uchaguzi za Kenya, na Afrika Kusini, wamewahi kuitwa na wadau kutoa ufafanuzi kuhusu muundo na utendaji wa Tume zao?

..Jitihada zote hizo zimekataliwa na CCM na wakatuletea Tume Huru bandia.
 
huyo mpumbavu wenu mwambieni awaambie hao mabwana zake kule Ulaya nchi hii inaongozwa kwa mujibu wa sheria na taratibu siyo kwa upuuzi wake huo.
Acha kugha chafu ww, mkifanyiwa nyie mnasema watu hawana adabu, kuheshimiana ni two way traffic.
 
Kuna mabadiliko yanayoweza kufanyika bila hata bunge kuhusika mfano kuwaondoa Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia uchaguzi.
CCM wanasema itachukua zaidi ya miezi sita kubadilisha vitu kama hivyo, maana lazima muswaada wa kuwabadilisha uandaliwe, ujadiliwe na vikao, urekebishwe, uende kwa raisi, atoe maelekezo, upitiwe tena, kisha urudi kwa raisi, akubali arudishe kwa waziri, uwe drafted kama muswaada, wabunge wa CCM aitwe kukubaliana nao, ndio uende Bungeni kujadiliwa. Hapo si miaka mitano tayari?
 
Acha kugha chafu ww, mkifanyiwa nyie mnasema watu hawana adabu, kuheshimiana ni two way traffic.
Unajibinaza na mtu mwenye mtindio wa ubongo Mkuu? Huyu lazima ana shemeji yake anamtuma kuosha gari la kimulimuli cha taa za blue na anamruhusu akiwashe anapopeleka gari car wash. Unafikiri ataelewa maoni ya Lisu yanayotishia shemeji yake kupoteza nafasi yake?
 
CCM wanasema itachukua zaidi ya miezi sita kubadilisha vitu kama hivyo, maana lazima muswaada wa kuwabadilisha uandaliwe, ujadiliwe na vikao, urekebishwe, uende kwa raisi, atoe maelekezo, upitiwe tena, kisha urudi kwa raisi, akubali arudishe kwa waziri, uwe drafted kama muswaada, wabunge wa CCM aitwe kukubaliana nao, ndio uende Bungeni kujadiliwa. Hapo si miaka mitano tayari?

..Steven Wassira alitakiwa awe amejibu hoja hii, but he is spent, sluggish, and stuck in his old ways and ideas.
 
CCM wanasema itachukua zaidi ya miezi sita kubadilisha vitu kama hivyo, maana lazima muswaada wa kuwabadilisha uandaliwe, ujadiliwe na vikao, urekebishwe, uende kwa raisi, atoe maelekezo, upitiwe tena, kisha urudi kwa raisi, akubali arudishe kwa waziri, uwe drafted kama muswaada, wabunge wa CCM aitwe kukubaliana nao, ndio uende Bungeni kujadiliwa. Hapo si miaka mitano tayari?
Kama ni miezi sita ina maana kufikia mwezi wa saba mabadiliko yatakuwa yamekamilika na uchaguzi unaweza kufanyika October kama kawaida.
 
..Lissu aliwahi kusema kwamba mapendekezo ya Chadema wakati wa Maridhiano yalikuwa mpaka na ratiba ya namna ya kuyatekeleza.
 
Kwa hiyo atafanya nini?
Jaribu kuwauliza wana ccm wenzio kuanzia viongozi wako, hadi machawa wenzio kina lucas mwashambwa and co, kwanini wamechukia Lissu kushinda uenyekiti na walitamani Mbowe aendelee
 
Anatoa mawazo yasiyowezekana kufanikika anadhani CCM ni wajinga kiasi hicho yy kama hawez uchaguzi 2925 aususie wengine wale
Kiburi ndio kitawamaliza ccm. Hoja aliyokuja nayo Lisu itakuwa na mashiko kwa umma kupita maelezo.
 
Back
Top Bottom