Anachoweza kufanya Membe sasa na kikamletea heshima kubwa

Akubali kuongoza mapambano dhidi ya CCM bila ya kudai malipo mbele.

Uhitaji wa Tanzania wa mwelekeo mpya, kuiondoa katika utekwaji chini ya mtu mmoja ni mkubwa zaidi kuliko mahitaji ya cheo kwa mtu anayeweza kuchangia kuiokoa Tanzania kutoka kwenye utekwaji huo.
Nimependa hicho unachodai cha Uhitaji wa Tanzania wa mwelekeo mpya, kuiondoa katika utekwaji chini ya mtu mmoja. Hakika mmefikirishwa kuwa kuna utekaji nchi hii. Poleni sana kwa kulishwa matanga.

Ebu, basi, tunapoelekea Uchaguzi Mkuu, kujeni na hoja mpya za kujenga IMANI ya wapiga kura kuliko kuendelea na hoja kama hizo zisizokuwa na mbele wala nyuma. Hazina ushahidi wowote kwani mnaotaka waamini hivyo, wako kwenye nchi huru wakiendesha maisha yao bila kubughuziwa kwa kufuata sheria bila shurti.
Babati
Chakaza
 
Akubali kuongoza mapambano dhidi ya CCM bila ya kudai malipo mbele.

Uhitaji wa Tanzania wa mwelekeo mpya, kuiondoa katika utekwaji chini ya mtu mmoja ni mkubwa zaidi kuliko mahitaji ya cheo kwa mtu anayeweza kuchangia kuiokoa Tanzania kutoka kwenye utekwaji huo.

Membe akubali kuwa mstari wa mbele katika mapambano haya bila ya kudai cheo chochote. Juhudi zake katika kuyaendeleza mapambano haya ndiko kutakakompa malipo ya juhudi zake za ukombozi.

Ni makosa kwake kuamini kuwa ni lazima apewe nafasi ya kugombea urais pekee ndio ashiriki kikamilifu kwenye mapambano.

Kazi Mbele, Malipo Baadae. Hii ndio iwe 'clarion call' ya yeyote anayetaka kushiriki katika mapambano haya.
2025 atagombea tena kwenye mchakato wa CCM. Iwapo mwaka huu atagombea chama cha upinzani na kukakuwepo na utitiri wa vyama baasi upinzani hawatashinda.

Membe alishindwa kuishi na kipofu kwa miaka hii mitano since 2015,alitakiwa awasuprise kwa kuchukua form CCM, sema jamaa wakamuintercept na kumfukuza.
 
2025 atagombea tena kwenye mchakato wa CCM. Iwapo mwaka huu atagombea chama cha upinzani na kukakuwepo na utitiri wa vyama baasi upinzani hawatashinda.

Membe alishindwa kuishi na kipofu kwa miaka hii mitano since 2015, alitakiwa awasuprise kwa kuchukua form CCM, sema jamaa wakamuintercept na kumfukuza.
Mkuu huwa nakukubali sana michango yako hasa katika siasa huwa upo neutral.

Kitu ambacho wengi hawana, uchama umewazidi.
 
Membe anawasumbua sana ccm tunakukaribisha CHADEMA tusukume juhudi za kuleta mabadiliko nchini.
 
Vipi, mnaiogopa mada. Mbona mnasoma tu na kujiendea zenu?

Kwa mtu yeyote anayejali maslahi ya Tanzania zaidi, kujitoa mbele na kudai haki kabla ya kutanguliza maslahi binafsi ya kunufaika hicho ndio kipimo sahihi cha kuwa kiongozi anayependa nchi yake.

Lowassa alikuja kutafuta maslahi yake, alipoyakosa, na kuwekewa masharti ikambidi arudi alikotoka. Lowassa hakuweka maslahi ya Tanzania mbele.

Kwa hiyo, kutokana na uzoefu huo, Membe atuonyeshe alivyochukizwa na CCM na kutaka kuiondoa, hata kama hatapata cheo chochote ndani ya serikali itakayofuata. Hicho ndicho kipimo sahihi cha uongozi wa kuipenda nchi zaidi ya maslahi binafsi.

Hapana, binafsi sijaiogopa. Ni saa za kazi boss . Ndo tu niko break na naiona mada....

Ulichokisema ni sahihi na ndivyo inayopaswa kuwa kwa Membe kama tu kweli ana nia ya kuikomboa Tanzania hii...

Haiingii akilini hata kidogo mtu kutoka chama kingine cha siasa na dakika chache anajiunga na chama kingine na hapo hapo anaomba kupewa madaraka makubwa...

Hii moja kwa moja ina - define nia ya mtu huyo inakuwa ni OVU kwa 100%....

Chama chochote kinachoweza kumpokea huyu bwana, kimpe sharti hili na yeye akubali. Akikataa aachwe aanzishe chama chake...!!
 
Sidhani kama Mbowe kukaa miaka 20 akiwa kama Mwenyekiti wa Chama ni tatizo kama demokrasia inafuatwa kwa ukamilifu kumhalalisha yeye kuendelea kukalia nafasi hiyo

Kupata kiongozi mkuu wa Chama chochote kunahitaji umakini wa hali ya juu. Kama vile tunavyoona kwenye CCM demokrasia lazima iwekewe kanuni na taratibu makini za ndani ya taasisi husika ili isiwe chanzo cha kuibomoa taasisi yenyewe kwa jina la demokrasia

Hebu chukulia mfano huu. Mnamchagua mtu kua kiongozi wa juu kabisa wa Chama halafu siku ya siku anatangaza kuunga mkono juhudi!!!

"....Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani mwisho wa siku eti anaacha chama na kutangaza kuunga juhudi..."

This is too bad....
 
Kaka chama ni Taasisi siyo mtu, kama taasisi imewekewa misingi mizuri haiwezi kutegemea mtu eti awaongoze kuwa threat kwa Serikali kwa muda wa miaka 20. Kwani lengo la chama cha siasa ni kuwa threat kwa Serikali au kushika dola?

Pia huwezi kufananisha mazingira waliyokua nayo kina Nyerere na ya sasa. Kipindi hicho hata watu wasomi wenye weledi walikua ni wachache. Na wengi walikua hawapendi kujihusisha na siasa walikua wanalinda vibarua vyao. Lakini sasa hivi, watu wenye uwezo ni wengi lakini wakitaka uongozi wanaondolewa kwa mabavu.

Lengo la chama chochote cha siasa ni yote mawili....

1. Kwamba, ni kuichachafya serikali iliyoko madarakani kwa kuikosoa na

2. Kutumia makosa ya chama kilichoshika dola kujiimarisha ili kupitia uchaguzi halali kikitoe chama hicho madarakani...

Wakati huo huo, Huyu ndugu hapa chini 👇👇👇kakupa majibu mazuri sana
Sidhani kama Mbowe kukaa miaka 20 akiwa kama Mwenyekiti wa Chama ni tatizo kama demokrasia inafuatwa kwa ukamilifu kumhalalisha yeye kuendelea kukalia nafasi hiyo

Kupata kiongozi mkuu wa Chama chochote kunahitaji umakini wa hali ya juu. Kama vile tunavyoona kwenye CCM demokrasia lazima iwekewe kanuni na taratibu makini za ndani ya taasisi husika ili isiwe chanzo cha kuibomoa taasisi yenyewe kwa jina la demokrasia

Hebu chukulia mfano huu. Mnamchagua mtu kua kiongozi wa juu kabisa wa Chama halafu siku ya siku anatangaza kuunga mkono juhudi!!!
 
Haukuwa ushauri mzuri, malengo yake ni kugombea urais ndani ya CCM au nje ya CCM. Wewe ulikuwa unamshauri kinyume na ndoto zake.
"Ndoto zake," na sio ndoto za kuitumikia Tanzania yenye mafanikio... ataishi na kufa nazo mwenyewe.
 
Vipi, mnaiogopa mada. Mbona mnasoma tu na kujiendea zenu?

Kwa mtu yeyote anayejali maslahi ya Tanzania zaidi, kujitoa mbele na kudai haki kabla ya kutanguliza maslahi binafsi ya kunufaika hicho ndio kipimo sahihi cha kuwa kiongozi anayependa nchi yake.

Lowassa alikuja kutafuta maslahi yake, alipoyakosa, na kuwekewa masharti ikambidi arudi alikotoka. Lowassa hakuweka maslahi ya Tanzania mbele.

Kwa hiyo, kutokana na uzoefu huo, Membe atuonyeshe alivyochukizwa na CCM na kutaka kuiondoa, hata kama hatapata cheo chochote ndani ya serikali itakayofuata. Hicho ndicho kipimo sahihi cha uongozi wa kuipenda nchi zaidi ya maslahi binafsi.

Hapa umezungumza jambo la msingi sana. Kama kweli anakuja upinzani kwa nia njema ya kupambana na ccm, basi cheo isiwe kipaombele chake kwa sasa. Yeye atoe mchango wako, mambo ya madaraka ni baada ya watu kujiridhisha na mchango wake.
 
Tindo viongozi wako watakuangusha sana wakimpitisha maana hoja zako zote nazokutana nazo ni kulaani hilo.
 
Na sidhani kuwa CHADEMA wana uthubutu wa kumpitisha Membe kuwa mgombea wao.

Linalowezekana, kwa maoni yangu; kama italazimu Membe awe mgombea urais, basi ni kupitia ACT-Wazalendo, na CHADEMA wakimpa ushirikiano kama hawatakuwa na mgombea wao toka ndani ya chama.
 
Msimamo wa kuwa Membe hafai kuwa mgombea wa urais kupitia cdm wala hauna kificho, uko wazi peupe, na ninaweza kuutetea msimamo wangu huu.
Membe amefanikiwa, mfumo umefanikiwa. Kama ni soka mchezo haujaanza lakini kuna timu ishapoteana kisaikolojia

Kwa ujio wa Membe upinzani uta/umeshaanza kigawanyika! Akienda CHADEMA na wakatokea watu wamsapoti kupeperusha bendera ya Urais, CHADEMA itameguka mapende matatu

Pande la kwanza ni hao wanaomuunga mkono, pande la pili ni wanaopinga asiwe mgombea wa Urais kama wewe Ndugu Tindo, na pande la tatu ni la wagombea wengine wanaoomba nafasi hiyo ikiwemo wale waliomwaga damu, machozi na jasho kuijenga Chadema hadi hapo ilipo sasa hivi ambao wataona wameuzwa na kusalitiwa

Ikiwa Membe ataenda ACT basi wapinzani watagawa kura! Hapa nawapa kongole watu wa mfumo, wamecheza kama wale mahodarinwa mchezo wa chess
 
Vipi, mnaiogopa mada. Mbona mnasoma tu na kujiendea zenu?

Kwa mtu yeyote anayejali maslahi ya Tanzania zaidi, kujitoa mbele na kudai haki kabla ya kutanguliza maslahi binafsi ya kunufaika hicho ndio kipimo sahihi cha kuwa kiongozi anayependa nchi yake.

Lowassa alikuja kutafuta maslahi yake, alipoyakosa, na kuwekewa masharti ikambidi arudi alikotoka. Lowassa hakuweka maslahi ya Tanzania mbele.

Kwa hiyo, kutokana na uzoefu huo, Membe atuonyeshe alivyochukizwa na CCM na kutaka kuiondoa, hata kama hatapata cheo chochote ndani ya serikali itakayofuata. Hicho ndicho kipimo sahihi cha uongozi wa kuipenda nchi zaidi ya maslahi binafsi.
Hatuogopi chochote !
 
Membe amefanikiwa, mfumo umefanikiwa. Kama ni soka mchezo haujaanza lakini kuna timu ishapoteana kisaikolojia

Kwa ujio wa Membe upinzani uta/umeshaanza kigawanyika! Akienda CHADEMA na wakatokea watu wamsapoti kupeperusha bendera ya Urais, CHADEMA itameguka mapende matatu

Pande la kwanza ni hao wanaomuunga mkono, pande la pili ni wanaopinga asiwe mgombea wa Urais kama wewe Ndugu Tindo, na pande la tatu ni la wagombea wengine wanaoomba nafasi hiyo ikiwemo wale waliomwaga damu, machozi na jasho kuijenga Chadema hadi hapo ilipo sasa hivi ambao wataona wameuzwa na kusalitiwa

Ikiwa Membe ataenda ACT basi wapinzani watagawa kura! Hapa nawapa kongole watu wa mfumo, wamecheza kama wale mahodarinwa mchezo wa chess

Cdm kama chama wanaweza kubaki wamoja hiyo ni juu yao kama chama, lakini mimi mfuasi sina haja ya kuendekeza jambo nisiloliamini.
 
Back
Top Bottom