Anachoweza kufanya Membe sasa na kikamletea heshima kubwa

Utaongozaje bila ya kuwa na cheo sehemu husika?,acha mbwembwe,nani atamtii ikiwa hana nyadhifa?

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
Nje ya ccm Membe hana nguvu wala ushawishi
Hilo unalijua wewe na wala huna ushahidi wa kuonyesha kuwa hivyo ndivyo kweli.

Kama ndani ya CCM anao ushawishi (maanake hivyo ndivyo unavyoonyesha), kwa nini ushawishi huo huo na hao anaowashawishi asiupeleke na kuuendeleza nje ya CCM?
 

Nadhani umeweka vizuri sana hii post yako.Ajue mazingira ya sasa na kumbukumbu mbaya ambayo wapinzani wanayo wanapotoa fursa hasa dakika za mwisho.Akilielewa hilo na kuunga mkono mapambano bila kutaka awe yeye litakuwa jambo jema.Walau aonyeshe anataka kweli mabadiliko anayojinadi kutaka kuyapigania.Karata hii ikichezwa vizuri tunaweza kushuhudia maajabu.
 
maneno hayo pia mwambie Lissu
 
 
Mada dhaifu
 
Maoni yako nimeyapenda sana , Na kwa maoni hayo hayo ya wananchi kuamini kiongozi alie jaribiwa anatosha, ndio maana wanachama wa CCM na wananchi wa Tanzania kwa ujumla wanapendekeza Magufuli aongezewa muda au miaka 10 au 20 zaidi baada ya kumaliza hii 10 ya kuanzia. Wananchi hutafuta Rais kwa kuwa anaitwa Rais laa hasha, tunatafuta kiongozi anaetufaa na kutuletea mabadiliko ya kutosha ambayo tumeyatamani muda mrefu. Kitaifa Magufuli nina tuu, Mbuga za wanyama, dhahabu, maziwa yetu, bahari, Tanzanite au resources ile ya kitaifa. Hatutaki kuweka kiongozi kwa vile katiba inapendekeza. Nchi duniani huendelea kwa kutumia resources walizo nazo. na resources zipo kuu tano( 5)
1) Watu
2) Fedha
3) Mali asili
4) Ubunifu wa kweli na wenye tija kwa Taifa.
5) Uongozi wa kutoa matokeo ( result oriented leadership)

Magufuli sio mtuu kitaifa ni resource, kwa hiyo lazima kwenye watu atumike kama kichicheo cha mabadiliko makubwa ya uchumi wetu. Akimaliza ndio hao waliberali ambao sifa kubwa ni kusema vizuri.
Kuonea huruma wahalifu.
Polisi kukubali kuwaacha watukutu wafanye mabaya watakayo na iwe ndio mtu wa kusifiwa na kupigiwa mfano.
Mashoga wafanye biashara zao za ukahaba na kujitangaza.
Wavuta bangi na ngada waingie bungeni na tuwapigie makofi ya kuwashangilia.
Watu wapate nafasi za uongozi wakiwa na vyeti feki na tuwavumilie na hata kuwatetea.
Wakianzisha kampeni za ukuta tuwaachie tuu na inapaswa tuwashangilia.
Tunatakiwa tuwe serious ndiyo tubadilike.
 
Nahisi akiwa msindikizaji hana relevance
 
Ndani ya mwili wa Nyalandu naiona roho ya Membe. Ingawa haitegemewi na walio wengi, bado napata ujasiri wa kumuona Nyalandu kuwa ndiye mpeperusha bendera wa CDM ili apate kukabiliana na Magufuli. Haya ndiyo yatukuwa maridhiano ya mwisho miongoni mwa makundi hasimu ndani na nje ya CDM.
 

Ww lazima utakuwa mzee kwa propaganda hizi, au kijana lakini unayeishi kwa kujipendekeza.
 
Nahisi akiwa msindikizaji hana relevance
Hili sio swala la usindikizaji, ni swala la kuchukizwa na hali iliyopo na kuamua kushiriki kuibadili. Huo sio usindikizaji, ni upambanaji.
 
Nyalandu amekwishaonyesha utofauti wake mkubwa na wengine wengi walioingia CHADEMA na wimbi la Lowassa. Nyalandu sio zao la Lowassa, yeye anajitegemea kivyake, tofauti kabisa na wengine. Anazo sababu zake za kumwondoa CCM, tofauti kabisa na wengine.

Alipoingia CHADEMA hakuingia kwa kugombea cheo, na amefanya kazi ndani ya CHADEMA matunda yake yanaonekana.
Kwa hiyo huyu ni sehemu kamili ya CHADEMA. Kama chama kitampima na kuridhika na sifa alizokijengea chama na yeye mwenyewe, bila shaka kitampa nafasi ya kupeperusha bendera. Hayo wanayajua wenyewe huko ndani ya chama chao.
 
Ww lazima utakuwa mzee kwa propaganda hizi, au kijana lakini unayeishi kwa kujipendekeza.
Mbona unampa heshima asiyoistahili mkuu tindo. Haya aliyoweka hapa zinakidhi mahitaji ya kuitwa 'propaganda' kweli?

Basi tuseme ni 'propaganda' kwa watu ambao hawana 'sophistication' ya aina yoyote kabisa! Hawana 'exposure' ya aina yoyote inayoweza kuwawezesha kujua ukweli na uongo.
 
Hakuna mpinzani bongo. Hiki ni kipindi Cha Hawa wahuni wa kisiasa kupiga hela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…