Anahitajika msichana/mwanamke kwa ajili ya IVF

unaonaje ukimlipa mtu mwingine kwa ajili ya kutoa yai na mbebaji mimba awe mtu mwingine akijifingua tuu chukua watoto walelewe na mtu mwingine special tena awe mtu mzima anaejielewa, maziwa ya watoto jaribu kutafuta kwenye bank za maziwa ya watoto yaliyokamuliwa kutoka kwa wamama wanaonyonyesha watoto wapatiwe hayo maziwa kwa miezi 6 , tena maziwa wapewe kwa kikombe sio chupa .
 
Wazo zuri sana ndugu, bado sijafanya hitimisho la utekelezaji hivyo wazo lolote bora linaweza kutekelezeka.
 
Yaani wewe uchukue damu yake ( yai lake) ila wewe kumwachia damu yako hutaki huoni kama ur selfish mkuu?? Au unafikiri mama atakuwa hana damu yake wala connection na huyo mtoto??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenichekesha sana, kwako itakua ngumu sababu ni damu yako lakini yai langu litakua rahisi kukuachia sababu...sio damu yangu au?

Haya siku ukiwa tayari utanicheki msimamo wangu utaendelea kua huo.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mkuu njaa ...mkuu njaa zinatoa watu fahamu
Na ni kweli nakubali siyo yeye,hayo ni maamuzi ya njaa! Waswahili wanasema,adui yako muwombee njaa,sijui walikua na maana gani vile!!?[emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787]
 
Umenichekesha sana, kwako itakua ngumu sababu ni damu yako lakini yai langu litakua rahisi kukuachia sababu...sio damu yangu au?

Haya siku ukiwa tayari utanicheki msimamo wangu utaendelea kua huo.
Siwezi kukucheki ndugu sababu wazo lako haliwezi kutekelezeka kwangu,
Pia kumbuka hiyo ni hiari, hivyo hakuna kitu cha ajabu au kushangaza ninapotoa mtazamo wangu.
 

Wajameni sasa sisi short chassis tumeingiaje hapa,
hapo ni deal la kutupa mtoto tu ukipata u world's embassador si tutakufaz
We achana na hizi mbilikimo kwa comments
Tantalila zetu ndo zimesaidia nyie twiga wa Tanzania muuone uzi

Fanya kuwahi PM utume picha unaona dirisha la usahili limeongezwa maana maombi ni mengi
 
Me nilijua ma single maza tuna kazi lakini masingle faza mna kazi zaidi
Mungu awasaide
Uende huku uombe yai
Urudi huku uombe uterus
Uende kule uombe nyonyo
Urudi tena uombe wa kuvalisha diapers

Bado hujaenda kazini
 
Me nilijua ma single maza tuna kazi lakini masingle faza mna kazi zaidi
Mungu awasaide
Uende huku uombe yai
Urudi huku uombe uterus
Uende kule uombe nyonyo
Urudi tena uombe wa kuvalisha diapers

Bado hujaenda kazini
View attachment 2456839
Mimi ni mwanamke 🙏, nimetoa tuu ushauri kwa mtazamo wangu na pia hilo swala kwa nchi zilizoendelea ni rahisi zaidi kwasababu hao surrogate mother wapo na wanauelewa wa kutosha na hayo maziwa halisi ya mama yanapatikana kwa urahisi zaidi. Hata tanzania pia yapo ndo huwa wanapewa watoto njiti.
 
Asante sana ndugu kwa hizo link, ingawa tayari kuna watu kadhaa wameshajitokeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…