sam alladayce
Member
- Apr 17, 2022
- 5
- 5
maa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwendraaaa 25mil ni kidogo, mimi bado niko fresh sijazaa huwezi nipanua tumbo kw pesa ndogo hivyo.
Ahaaaaaa ati mtoto akizaliwa ndo mwisho kumuona baada ya mwaka? Hakuna mzazi wa vile.
Ahaaaaaa ati kipindi cha mimba awe anaishi kwa baba watoto? Ahaa watafanya tu labda baba huyo kama hana nguvu za kiume.wendo ndo sababu anataka kupandikiza.
Ni kwakuwa ni chai hakuna mbongo wa kukubali kuchukuliwa mtoto.
All the the best dadazi.
Huu msemo umenikumbusha mbali.. Mazaa alipenda kutuambia hivi ni baada ya maneno kua mengi kutoka kwa ndugu zake kua anazaa hovyo kwetu tupo 7 tumebaba kwenye kijumba chetu hadi tumekua.Tajiri na mali zake maskini na wanae
Hakuna wa kumfata piem hata 10 hawezi zipata. Hakuna wa kukodisha tumbo lake kwa muda.
Kiki za kijingaIVF kirefu chake ni In Vitro Fertilization.
IVF ni jambo la kurutubisha kwa kuunganisha mbegu za uzazi za mwanamme na yai la uzazi la mwanamke maabara, baada ya hapo zoezi linalofatia ni kupandikiza ujauzito kwa mwanamke kwa njia ya sindano kisha ujauzito utaendelea kukua kama kawaida kwa mda wa miezi tisa kisha mwanamke atajifungua kawaida.
IVF haihusishi kukutana kimwili kati ya mwanamke na mwanaume bali mwanaume anatoa mbegu kwa kujichua au punyeto na mwanamke anatolewa yai lililopevuka maabara na wataalamu baada ya hapo ndio ujauzito unapandikizwa kwa mwanamke,
Ni njia safi na salama na haihusishi operation kubwa na haina hatari yeyote kwa mwanamke.
Sasa anahitajika mwanamke au msichana katika zoezi hilo,
MALIPO
Moja malipo ni milioni 25 ambayo yatasainiwa kisheria mahakamani na ustawi wa jamii.
Pili kila mwezi atalipwa milioni moja kama malipo ya motisha kwa mda wa miezi tisa ya ujauzito, malipo hayo ni nje ya ile milioni 25.
Tatu kila siku atalipwa elfu ishirini kama gharama ya chakula kulea mimba kwa mda wa miezi tisa ya ujauzito.
Nne atalipwa shilingi elfu hamsini kila siku kama gharama ya chakula baada ya kujifungua kwa mda wa mwaka mmoja kipindi ananyonyesha.
Tano gharama zote za hospital kwa mama kipindi cha ujauzito, mama na mtoto baada ya kujifungua zitagharamiwa na baba wa mtoto/watoto
MASHARTI
Moja ujauzito utalelewa sehemu aliyopo baba wa watoto.
Mbili hauruhusiwi kisheria kutangaza kwa mtu yeyote kama una ujauzito labda wazazi wako tu, na wazazi wakiambiwa nao wataelimisha kuhusu hili sharti.
Tatu baada ya kujifungua, mtoto/watoto wakifikisha mwaka mmoja utawakabidhi kwa baba yao.
Nne baada ya kukabidhi mtoto/watoto hautoruhusiwa kisheria na kibinadam wewe ndugu zako au rafiki zako kuwaona mtoto/watoto kwa namna yeyote kipindi chote cha maisha yenu hapa duniani.
Tano hautoruhusiwa kuwa na mahusiano ya aina yoyote na baba wa watoto kabla na baada ya kujifungua mtoto/watoto.
Sita awe tayari kulea ujauzito akiwa jijini dar es salaam.
SIFA ZA MWANAMKE/MSICHANA ANAEHITAJIKA.
Moja awe na afya nzuri, asiwe na magonjwa ya akili, pili asiwe na magonjwa ya zinaa ikiwemo ukimwi.
Pili awe mtanzania kutoka kabila na dini yeyote.
Tatu awe mrefu, mrefu sana atapewa upendeleo.
Nne awe mwembamba, akiwa mnene isiwe unene mkubwa sana.
Tano awe na umri wa kati ya miaka 25 hadi 35.
Sita awe mweupe au maji ya kunde asiwe mweusi sana.
Asanteni.
Pia kwa mwana Jamii Forum mwenye ndugu, rafiki au jirani mwenye hizo sifa naomba mnisaidie kusambaza hili tangazo.
Asante tena.
Vigezo na masharti kuzingatiwa
Asante kwa maoni ndugu, ila hii sio kiki ni jambo serious.Kiki za kijinga
Hiyo pesa kwanini usiwekeze kwenye kilimo cha karanga nachingwea shamba ekari moja kukodi shilingi elfu 60.
Kama ni jambo serious kwanini utumie njia isiyo kubalikia kitamaduni na kidini?Asante kwa maoni ndugu, ila hii sio kiki ni jambo serious.
Asante kwa maoni nduguKama ni jambo serious kwanini utumie njia isiyo kubalikia kitamaduni na kidini?
Acha uhuni,wewe mbona hukuzaliwa kwa hiyo Moet?Asante kwa maoni ndugu
Ila naomba ujue kwamba si kila mtu duniani anaamini dini na utamaduni.
Watu wengine wanaamini katika Technolojia kama suluhisho la matatizo yao
Watoto watatoka mafala mafala kama ma broiler yanatotoleshwa kwa mashine 😂😂Ectolife ndio unahitaji wala usihangaike na mwanamke akuzalie bali subiri kuna artificial womb na wanafyatua watoto 30,000 kwa mwaka kwenye laboratory moja
Wanasema watu hawaongezeki sana na itafika kipindi tutakosa wafanyakazi
Sijui China atatengeneza machine cheap kidogo na mimi ninunue?
Elon Musk mwenyewe ana lea watoto 9 ambao hajawazaa yeye
View attachment 2454774View attachment 2454775
Asante kwa maoni ndugu, ila mimi sio muhuniAcha uhuni,wewe mbona hukuzaliwa kwa hiyo Moet?
Nature can't change!, Nyie ndy wale vijana wa hovyo umarekani mwingi kumbe kwenu Nanyumbu kisa tu Umefika chicago
I tell you heshimu utamaduni wako na nature yako acha kujifanya msomi uchwara wakati ww ni pure mdendeule wa mbinga
Mayai ninayo mengi sana tena ya kuzaa vidume vya mbegu.
Ila asee siwezi...kama kuzaa rahisi mbona yeye hawezi??
Mwisho yanakuwa juma lokoleWatoto watatoka mafala mafala kama ma broiler yanatotoleshwa kwa mashine 😂😂
Why utumie ivf?Asante kwa maoni ndugu, ila mimi sio muhuni
Hakika mkuu... hata ile uchungu wa mwana aujuae mzazi haitakuepo tena..Mwisho yanakuwa juma lokole
Umeanza kwa kunishutumu, hivyo sidhani kama unaweza kunielewa.Why utumie ivf?
Ila jamani hawa watoto wa hivi sijui itakuaje
Si kutukani nakueleza ukweli, mwanaume rijali hawezi akafanya mambo ya hovyo kama hayaAsante kwa maoni ndugu, ila sipo hapa kushindana au kutukanana na mtu
Asante kwa maoni ndugu, ila ukweli naujua mimi na hilo jambo sio la hovyoSi kutukani nakueleza ukweli, mwanaume rijali hawezi akafanya mambo ya hovyo kama haya