Anaitwa Roma: Wimbo mpya wa Roma Mkatoliki

Anaitwa Roma: Wimbo mpya wa Roma Mkatoliki

Namkubali Fid ila kwa Roma aiseeee jamaa anajua sana
Hata mimi sisemi roma mbovu, ni kati ya wanahip hop wakali hapa tz ninaowakubali mimi.

Tusimuangalie huyu fid wa ole ole, tuanze na yule fid wa huyu na yule, fid.com. mwanza mwanza, albamu ya vina mwanzo kati na mwisho, i am professional, ielewe mitaa, neno na kuendelea.
 
Roma Mkatoliki ni ameamua kujilipua ama? Binafsi sijamuelewa au labda amepewa go ahead na system.

Wimbo mzima ukiusikiliza kwa umakini ni kama ameamua kumnanga "prince".

Pale anaposema "mjibuni mmemzaa Mpare ila siwachukii Wasukuma."

Naendelea kuamini, aidha Roma ameamua potelea mbali liwalo na liwe ama amepewa kinga na wasiojulikana.
Kwani hajawahi kuimba nyimbo za Aina hiyo ?
 
Kila mtu na mtazamo wake.. Francesc fabregas alikuwa mchezaji mzuri mnoo kwenye ubora wake lakink bado xavi na iniesta walikuwa mbele yake, xavi kuwa bora haimaanishi fabregas kuwa mbovu.

Roma ni mwanahipop mkali ana ngoma kali, na mistari mikali, anajua jinsi ya kucheza na maneno, hakuna mtu atakaetokea na kukwambia roma ni msanii mbovu, ila ukweli ni kuwa super marioo fid q atabaki kuwa fid q.
"Hawaamini kuwa na kiba au diamond WAWILI, wanachotaka nikumshusha mmoja na mwingine awe DILI"


Mkuu wabongo ndivyo walivyo, ni roho mbaya zimewajaa. Kwani hatuwezi kutambua ubora wa watu bila kutaka mmoja awe chini ya mwingine.

Kuna watu sijui wakoje.
 
Roma Mkatoliki amerudi upya jamani.
Ametoa wimbo mpya unaitwa "Anaitwa Roma".

Ni Roma yule tuliyemzoea enzi za Mrisho akitamba na vibao vyake matata. Je Basata watauacha huu wimbo? Utafute mapema kabla hawajauchukulia hatua.

Katika wimbo huo mimi nimependa mstari fulani hivi unasema;
"Kwetu bima ya afya ni bora kuliko ndege"
"Albino wa Moroco" anamaanisha nini......ni nani huyo?
 
We kamatiaaa chini,
Mi nakamatiaaa ndinga,
Na ukikamatiaa mpini,
Si utakamatiaaa mimba.
mtasahau tu kuhusu sekeseke la "nanhii" za mtaa la juz'kati......hata kwa lazima [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1544]
 
Kwa wenzetu huko majuu fid q wangemuweka katika level ya pekee yake, historia yake katika muziki, kudumu kwake katika gemu.. Na tukubali tu fid na roma wana mistari mikali ila fid yuko hatua kadhaa mbele ya roma.
Fid q.com
August 13
Usinikubali haraka
Propaganda
Ielewe mitaa

Kwangu mimi Roma hana ngoma inayozizidi hizo ngoma apo
 
Back
Top Bottom