Anaitwa Roma: Wimbo mpya wa Roma Mkatoliki

Anaitwa Roma: Wimbo mpya wa Roma Mkatoliki

Roma kauaaaaaaaaaa...Daaaah huyu jamaa Karudi sasa kwakweli
 
Wanauliza Roma siku hizi huimbi za kiharakati huku wakisema ununio ndio kumbukumbu iliyobaki. Aaaaah.

Eeh kwa unitaki
Mbona hamkumsapoti Mange na ninyi mtakuwa wanafiki, Sijui mlikwama wapi.

Walinivunja dole la Mwisho waliacha Dole la kati. Eeh hii si ni nchi ya Democracy mkimaindi basi mnawajua sasa mbona hamuwakamati. Tuache hayo

Vipi korosho za Mtwara, Maana wapiga kura wengi ni Wakulima na Wafanya biashara.

Kumnyima mpinzani Ajenda, mtendee tu yaliyo mema.
Sio kumpelekea Difenda, mtaani tutie vilema.

Machozi ya Watanganyika hayatowaacha salama. Damu zilizomwagika milele zitawaandama.

Mwanangu akiwauliza wale waliyoniteka ni nani aliwatuma, Mjibuni nimemzaa Mpare ila simchukii Msukuma.

Nchi inaangamia viongozi hawana maarifa na hawataki wakosolewe wanafanya kazi kwa sifa
 

Hakika nimeshindwa kujizuia usiku huu kuwaletea wimbo huu wa Roma Mkatoliki ambao kwa maoni yangu hakuna kwa sasa wimbo uliojaa hamasa za Kisiasa katika wakati huu mgumu wa siasa za kishamba.
Ndani ya mashairi yake amefunguka kisanii kumtaja mtekaji wake na mambo mengi ya hovyo ya utawala huu.
Tuusikilize na kuuchambua mstari baada ya mstari.
Natamani colabo ya Roma,Stamina na Sugu na Prof J siku moja.

Mungu mbariki Roma
 
Huyu ndiye Roma nimjuaye miye. Sema naye mjanja huu wimbo angeutoa wakati yuko Bongo saivi angekua mikononi mwa wasiojulikana. Naona kawapa 'dole la kati' walilosahau kulivunja.

'mnapiga bomu mochwari mnajisifu mmeua'
'nimemzaa mpare ila siwachukii wasukuma'
da mistari konzi sana kweli fasihi Roma kaitendea haki.
 
Mungu mbariki Roma
Kaimba "WIMBO WA TAIFA" huu. Ila kesho asubuhi na mapema utapigwa marufuku, tena watatangaza ukikutwa nao hata kwenye simu unakula "KESI YA UHUJUMU UCHUMI" au "KESI YA UHAINI" dadeki.

Halafu lazima basata "VAR" itumike, kumwita na kumfungia "ROMA" kujihusisha na sanaa kwa muda usijojulikana. Utawasikia basata wakisema "MAUDHUI YA WIMBO" sio ya kistaarabu wasanii wote wanatakiwa waige kwa "HARMONIZE na NANDY".

#HASHtag #MWIMBOwaTAIFA
 
Back
Top Bottom