Wewe ukiwa huru kujieleza alafu wenzako hawana uhuru wa kufanya hivyo. Je utasema kuna uhuru wa kujieleza?
Embu amka kwenye ndoto za kijinga hizo. unaandika kama mwendawazimu bhana.
Wewe kama unaona kuwa kuna uhuru wa kujieleza. Nawe kaimbe na uende kila chombo cha habari ukaipe promo. Kisha Ukale bata Fiesta au Wasafi Festival. Kwani nani alikukataza?
Lakini wewe unataka kumkataza ROMA ambaye kwa upande wake anaona hakuna uhuru wa kujieleza. Huoni kitendo tuu cha kutaka kumzuia ROMA asiende kuelezea hayo maoni yake ni Udikteta na sio Demokrasia.
Sina uhakika kama unajua maana ya Demokrasia. Sina uhakika kama unajua principles za demokrasia.
Ungezijua Principle za Demokrasia ungeelewa huyo ROMA anazungumzia nini. Hata hivyo sikukatazi kuwa Mjinga ikiwa umeamua kuwa hivyo. Maana nayo ni Demokrasia.
Kwa kukusaidia tuu.
Demokrasia ni mfumo wa serikali ambapo watu ndio huchagua serikali itakayowaongoza. Kwa hiyo watu ndio huamua nini kiwe na kipi kisiwe kwenye serikali walioichagua.
Tuje kwenye Principles za Demokrasia
● CITZEN PARTICIPATION (USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI AU RAIA)
Mwananchi au raia katika nchi zenye demokrasia anapaswa kushiriki na kushirikishwa katika masuala mbalimbali ya kitaifa kama uchaguzi, Upigagi wa kampeni na mambo ya kisiasa, Kulipa kodi, Kupewa taarifa ya mambo yanayoendelea katika nchi n.k.
Sasa kama Wapinzani hawapewi ruhusa ya kufanya siasa wakati demokrasia inawaruhusu kufanya shughuli hizo huoni kwamba tayari demokrasia imesiginwa. Hilo huoni.
Kama mtu anataka kugombea uongozi lakini anawekewa figisu figisu bado useme kuna demokrasia. Labda uwe mwendawazimu wa kuzaliwa ndio unaweza kufikiri kwa namna hiyo.
● EQUALITY (USAWA)
Kwenye demokrasia raia wote ni sawa. Na wanapaswa kutendewa kwa usawa kabisa bila uonevu.
Lakin taifa letu lipo kundi linayoruhusa ya kufanya siasa wakati kundi jingine halina haki ya kufanya hivyo.
Suala la vyeti feki tuu. Wapo walioondolewa kwa kuwa na vyeti Feki hilo ni jambo jema lakini kitendo cha kuwaacha wengine kama akina Bashite kumeifanya Demokrasia kusiginwa. Hakuna usawa.
Suala la kubomolewa nyumba. Kama utakumbuka Jpm alisema wazi kabisa watu wa Mwanza wasibomolewe nyumba kwa kuwa walimpigia kura. Wakati huo watu wa DSM wakilia na kusaga meno. Wewe Bado unamuona ROMA haimbi anachokiamini.
● POLITICAL TOLERANCE (USTAHIMILIVU/ UVUMILIVU WA KISIASA)
Demokrasia inawataka watu wawe wastahimilivu kwenye siasa. Ukisikia mwenzako anakupiga kijembe au anatoa hoja ziwe za msingi au ziwe za hovyo unapaswa uvumilie tuu maana nawe anakuvumilia.
Lakini hili kwenye nchi yetu halipo kama ulikuwa hujui. Mhe. Rais kila mara ameshuhudiwa akitukana watu na kuwaita majina yasiyo na stara kwa mfano Wapumbavu, Vilaza, majizi(wakati hajapeleka hata mmoja jela) n.k. Yeye watu wanamvumilia lakini yeye akiitwa Dikteta Uchwara anahaha. Akitajwa kwa majina yasiyo yaheshima anahaha. Hana ustahimilivu wa kisiasa.
Matokeo yake ndio utasikia Lema kawekwa ndani, utasikia Tundu Lisu kapigwa Risasi, Utasikia Mbowe Kawekwa ndani, akina Halima Mdee na wenzake.
Utasikia Nani katekwa, Sijui fulani kakutwa kwenye Kiroba.
Alafu useme ROMA hajui akiimbacho. Sema wewe ndio umeshindwa kuelewa maudhui ya wimbo huo na kuyaoanisha na Mazingira.
● ACCOUNTABILITY AND TRANSPARENCY (UWAJIBIKAJI NA UWAZI)
Nchi isiyo na Demokrasia huwezi kuona watu wakieajibika au kuwajibishwa. Au kuwa na uwazi. Ishu tuu utekaji na mauaji yaliyokuwa yanaendelea katika nchi hii. Viongozi kadhaa walipaswa wawajibike mathalani Kangi Lugola. Waziri wa mambo ya ndani asingepaswa kubaki madarakani ikiwa anajitambua kazi yake.
Masuala ya Korosho, Sijui Upotevu wa 1.5T ni mambo ambayo yangepaswa kuwekwa wazi lakini hayo hayapo. Na ukiyaongea upo katika hatari ya maisha.
● ACCEPTING THE RESULTS OF ELECTION
(KUKUBALIANA NA MATOKEO YA UCHAGUZI)
CCM mara kadhaa wamekuwa wakitumia mabavu kutangaza matokeo ambayo ni ya uongo. CCM wakishindwa kwenye uchaguzi mara nyingi huiba au kutumia nguvu kumtangaza Mgombea wao. Usijesema sina mifano; Kule Zanzibar hakuna asiyejua kilichotokea. Seif alishinda lakini CCM wakatumia Mabavu kufanya uchaguzi urudiwe. Kule kwa Kafulila na Wasira walitumia figisu figisu nyingi.
Bado useme ROMA hana chakuimba. Kama wewe sio mwendawazimu utakuwa ni nani?
Sishangai kusikia wewe ni mtu mzima tena huenda unashahada ya fani fulani. Demokrasia pia ni pamoja na kuchagua kuwa mjinga hivyo ni haki yako.
Zipo Principles nyingi sana za demokrasia. Nimekupa kwa uchache sana.
Hivyo ukisikia mtu akisema habari za demokrasia usifikiri anaongelea jambo moja au mawili kama miguu ya ndege. Hapo yanazungumziwa masuala mbalimbali.
Wewe umekalia Fiesta sijui uhuru wa kujieleza. Angekuwa na uhuru wa Kujieleza angetekwa? Mbona hilo hulizungumzii.
Hivi hii nchi ingekuwa na demokrasia unafikiri mpaka sasa watumishi wangekuwa hawajaongezwa mishahara?
Hivi hii nchi ingekuwa na demokrasia leo hii watu wangetekwa na kuuawa?
Hivi hii nchi ingekuwa na demokrasia unafikiri Akwilina angeuawa?
Hivi hii nchi ingekuwa na demokrasia unafikiri JPM angekuwa madarakani?
Hivi nchi hii ingekuwa na Demokrasia unafikiri Polisi kama Yule wa Dodoma angeongea sijui watapigwa Wachakae ilhali familia yake inategemea mshahara anaopewa na hao hao watu?
Niishie hapo maana mjinga naye anauhuru wake.