Anakorogea uji wa vitumbua na mkono wa mtoto aliyekufa

Hawa jamaa mjomba wangu aliwatoa baru. Enzi hizo watu wenye bunduki ni wachache. Kijijini huko.. Eti mvua imekataa kunyesha wanasema yeye ndiye anaizuia isinyeshe kwa uchawi wake. Wakamleta ''manyaunyau'' atoe uchafu. Ikapigwa risasi moja hewani pwaa.. watu wakakimbia kama wale nguruwe walioingiwa na mapepo kwenye biblia.
 

Wajinga Ni vipofu siku zote.
Sasa tuna kina lambalamba Huko makanisani
 

Buchani nyama sio halisi?
Hapo ndio patamu,
 

😂😂😂
Wabongo ukiwazidi Akili na Pesa utaitwa mchawi
 
Mkuu ile story ya utapeli ulimalizia kweli???
 
Ndio maana zikaitwa "imani" za kishirikina, maana yake hili ni suala la kuamini na wala siyo lazima iwe ni ukweli(facts). Madhara ya uchawi hayatokani na wachawi wanaodhaniwa kuloga hapana, bali madhara makubwa na hatari kabisa hutokana na wale wanaoamini kuwa kuna uchawi. Kwa mfano utakuta jitu likishaaminishwa kwamba kiungo cha albino kina uwezo wa kumfanya mtu awe tajiri, basi utakuta jitu hilo kwa ujinga wake kweli linakwenda kumtafuta albino wa watu maskini asiyekuwa na hatia yeyote na kumuua au kumkata kiungo.

Halikadhalika kwa vile mganga mpuuzi kamuaminisha mtu eti akiloweka nguo chafu ya ndani katika mchuzi wa ugali wateja watakuja lukuki, basi mtu huyo kwa ujinga wake kweli anakwenda kuwalisha watu uchafu wa ajabu usioelezeka. Waafrika nasisi tuache kushabikia mambo ya kishirikina yasiyokuwa na ushahidi wowote zaidi ya speculations tu sisizokuwa na kichwa wala miguu na mbaya zaidi si waganga tu wanaoshadidia mambo haya bali hata baadhi ya viongozi wa dini nao wamekuwa chanzo kikubwa cha kupandikiza imani hizi ndani ya waumini wenye uelewa mdogo kwa faida zao binafsi hasa za kiuchumi.
 
Wale mabwana walikuwa washenzi sana. Na akili za watanzania zilikuwa finyu katika kuchanganua mambo. Wale walikuwa wakiitwa lambalamba au rambaramba Kila nyumba lazima watoe chupa imefungwa vitambaa vyekundu na vyeupe Yan rangi mixer.

Kumbe ilikuwa janja janja tu mmoja anajifanya kapandisha mashetani anasema hapa Kuna kitu anachinjwa kuku au mbuzi ili kutoa hicho kitu.

Ila vile vitu walikuwa wanakuja navyo wanavizika hapo hapo na kuvitoa hapo hapo

Walikuwa wanakula Hela za Bure Kila nyumba 1,500/✓ au 2,000 tsh pamoja na kuku.

Walikuwa ni lazima Kijiji kizima waingie na Kila nyumba.

Na kwa mfano ukikataa nyumba yako wasifike basi pale kijijin wanakuona ww ni mchawi kwann hutaki nyumba yako ikaguliwe.!????


Kuna masheikh walikuwa wanakataa hawa washirikina wasifanye ushenzi wao katika nyumba zao ila wanakijiji wakawa wanaona masheikh ndio wachawi

Basi wale jamaa walinenepa kwa kuku WA dhuluma .ila kumbe ilikuwa ni mpango tu maalumu WA kuwapiga watu Hela .....


Ila jamaa hawakujulikana hata wamepotelea wapi na uzushi wao wale washirikina.

Ujinga mzigo!!!!!
 
Ila manyaunyau sikuwai muelewa na ile style yake ya kung’ata paka.
 
Dah ilo song lao kilikuag tamu sana "wachawi wanawanga wanga"
 

Hatari Sana.
Kwa sasa lambalamba wapo Kanisani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…