Anaomba ushauri: Akubali kuwa mke wa pili au asubiri atapata mume wake?

Anatakiwa atambue kwamba mtu wa kwanza wa kumuomba ushauri ni yeye mwenyewe asije kujidanganya.

Alafu akumbuke tu kwamba kuolewa/kuoa sio jambo la lazima iwe kwa mwanaume ama mwanamke wa kiislamu maadamu hafanyi zinaa.

Tatu aelewe kwamba ana uhuru wa kuchagua aolewe na nani kisheria ya dini na anaweza kuamua kukataa kwa sababu zake binafsi na wala hakuna wa kumzuia.

Miaka 25 sio umri wa kuharakia ndoa TENA NA MTU AMBAE hujui uamue nini kama akuoe ama laa,tena unaomba ushauri kwa watu.

Kama watu anaowaomba ushauri watamsaidia kukaa na huyo mume basi aendelee kuwaomba ushauri na kuwasikiliza lakini atambue kwamba ndoa ni jambo binafsi,ukishaolewa tu kila jukumu utabeba mwenyewe hakuna kwamaba alinishauri fulani,wewe hukuwa na ubongo wa kuchakata ?

Lakini mwisho ana uhuru wa kuamua kama ataolewa na mtu mkubwa zaidi yake ama mtu ambaye wanatofautiana miaka michache,muhimu asijifananishe na wengine.

Asijifananishe na wengine kwamba fulani na fulani wameolewa yeye bado,hiyo ni sumu kwa sababu everyone ana story personal,so kujifananisha na fulani kwamba yeye tayari wewe bado unataka kulazimisha story yako iwe kama yake
 
Umemaliza
 
Watakuwa wanaringia uzuri wao...wako tayari kuolewa na machinga wa kilimo? Nipe namba zao
Hawaringi ila aina ya maisha wanayotaka ndo haipo, hakuna wa kumpeleka shamba pale we jitafutie bi kilimo tu,
 
Kama Nani anatamani awe mwanamke
 
Na ni pisi kali kweli kweli lakini sijui nini kimewakuta haya mambo yanachanganya kinoma
Kibaya ni kwamba huenda walikuwa ma slay queen wa mitandaon kama wale wanaojiuza,,,mwanamke anapochagua kuwa slay queen ndo jinsi anavyojipunguzia nafasi ya kuolewa hakuna mwanaume hufikiria kumuoa slay queen na kumuweka ndani kwanza wazaz watakushangaa ila kupita naye au kuwa mchepuko na haya ndo malipo ya maslay queen
 
Hapo kwenye mzigo mimi huwa nawashangaa sana, na ndipo ninapoona dini ni unafiki tu.

Kulikuwa na dada wa Kiislamu analazimisha nile mzigo, wakati wa Ramadhani, huku yeye kafunga.

Mpaka aibu nikawa naona mimi.
Kwani si yeye kama binadamu ila uislami hautaki.

Huyo ni binadamu anatenda dhambi na wote tunatenda dhambi hakuna mkamilifu.

Nia yakoπŸ‘‰unataka kuleta hoja zako hazina mashiko kama huwezi kufuata dini na huamini kwamba hamna Mungu ni sawa ,ujinga ni pale unatumia nguvu kulazimisha maoni yako dhaifu watu waamini.

Kama una lifestyle ya uzinzi, ulevi ni sawa hata uwe muislamu ila uislami hautaki ni wewe tu utajua ufaute lip?

Hakuna dini inaweza kuharibiwa na matendo ya mtu mmoja na pia binadamu wote tunatenda dhambi,ila Imani ya mtu ipo pale pale.
 
Tupo nyakati ngumu sana inaonekana km story tu ila ndo uhalisia wanawake ndo wanatafuta kuolewa kwa mbinu zile zilizotumiwa na wanaume
Yaani zama hizi ndo unakuta magroup ya kutafuta uchumba yamejaa kibao yaani.

Kifupi maisha yamebadilika sana.
 
jamani at 25 unataka kuolewa mke wa pili?!,

Nini kilichomfanya awe desperate?

Au she is not confident with her looks, anaona atadoda?

Rejected na boyfriends?? ndio unaona safety net ni mume wa mtu?!

Either way pole zake,

Mimi ni kibibi,sijaolewa ila kuwa mke wa pili, NO. 😁😳😳😳
 
Sikuzote mwanamke akiwa mtiifu na mwenye maadili hata akiwa 29-31 years wanaolewa, hilo nimeliona, wenye viburi ndo huwa hawalambi kitu.
Exactly πŸ’― miongoni mwa wasichana walikuwa bora na misimamo wengi wameolewa miaka hiyo baada ya kupata Masters.

Adabu ina sehemu kubwa hata uwe 40 ila utoto kibao ,hakika utasanda.
 
Huu ndo ukweli maana kwenye kuslay maigizo ni mengi imepelekea sasa wanaume wanawaogopa inawagharimu pakubwa mabinti wazuri lakini wanalia kwa kukosa wachumba sio waume yani hata wa kuposa tu hakuna
 
Anahisi atadoda baadae ila mungu yupo mume atapata tu.
Ujue ukiwa huna mtu anaeonyesha muelekeo inaleta stress hiyo hali.
Kwa uzuri mzuri tu kishape anacho anajistiri vizuri
 
Anahisi atadoda baadae ila mungu yupo mume atapata tu.
Ujue ukiwa huna mtu anaeonyesha muelekeo inaleta stress hiyo hali.
Kwa uzuri mzuri tu kishape anacho anajistiri vizuri
Kwa nini uhisi utadoda baadae kama hujadoda sasa hivi...?

Kama hakuna anayekufuata sasa hivi ndio utakuwa na mawazo ya kudoda baadae..

Kama ni mzuri na yuko confident na uzuri wake nini kinachomfanya awe desperate...?

Kuwa desperate kunaweza kukufanya uishie kuchagua mtu sio sahihi,

Kama hapo sidhani kama kampenda huyo mume wa mtu

Ni ndoa tu she is after

Sad!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…