Anapika chakula hanipi, hanifulii nguo halafu anataka ndoa

Anapika chakula hanipi, hanifulii nguo halafu anataka ndoa

Nilipozaliwa nilitamani siku moja niwe na familia yenye Amani furaha na upendo lakini vyote hakuna badala yake, Mwanamke hanifulii anapika Chakula hanipi, Anaenda mbali na tulipo haniambii.

Halafu ananimbia anataka tufunge ndoa. kweli?

Nimfanye nini huyu mwanamke?

BF416D91-ED01-4325-9E25-52782869E4B0.jpeg
 
Nilipozaliwa nilitamani siku moja niwe na familia yenye Amani furaha na upendo lakini vyote hakuna badala yake, Mwanamke hanifulii anapika Chakula hanipi, Anaenda mbali na tulipo haniambii.

Halafu ananimbia anataka tufunge ndoa. kweli?

Nimfanye nini huyu mwanamke?
Umeoa ama bado? Unataka akufulie kama mchumba ama kama mume? Fafanua pls
 
Tunaishi kienyeji hatuna ndoa ya kanisani wala bomani.
Ok, hapo nimekuelewa kamanda. Kama kaanza vituko mapema namna hiyo na hamjaingia ndani rasmi, usidhani atabadilika akishakua na ndoa rasmi. JIONGEZE.
 
Ongea nae kwa kina. Mweleze ukweli mambo ya ajabu anayoyafanya. Asipobadilka achana nae.
 
Duuuh wanaume wengi inaonyesha hamjui logic ya Mungu kuumba wanawake wengi kuliko wanaume
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] dah we jamaa nahisi utakuwa na udugu waa damu na ukoo wa Albert Einstein sio kwa smart comment kiasi hiki.
 
Chakula natoa hela mimi ila akipika ndiyo hivyo.
Hii situation nilishawahi kuiona. Kuna sampuli ya chuo ilikuwa ikija weekend kuchill from Friday to Monday. But nikanotice tabia kama hizo.

Ilikuwa kwanza ina ulafi wa kijinga sana. Imagine sampuli inapiga ile chupa ya coca-cola ya lita 2 yote bila mimi kunipa collaboration yoyote.

Yaani anakata chupa nzima ile kuanzia asubuhi hadi jioni chupa inakuwa tupu. Ukiweka vitu vidogo vidogo kama bites akiwa anaondoka anapakia kwenye pochi chupa mbili za takeaway soda, mara abebe sijui nini. Nikahisi pengine ni kukosa pocket money nikawa nampatia ila wapi.

Sasa nikaja kujifunza kuna watu wako poor na empty in home training. Hawakufunzwa ukarimu na kujali wengine. Pia hawakufunzwa au kuelewa manners ili kubehave vizuri.
 
Back
Top Bottom