Anapost wanaume walionunua magari na chattings zao status wakati mimi niko kwenye hali ngumu kiuchumi

Anapost wanaume walionunua magari na chattings zao status wakati mimi niko kwenye hali ngumu kiuchumi

Kataa ndoa 3:0 walio kwenye doa. halafu uwanja umeinama possession 80% kwa 20%
Kataa ndoa 3 kivipi ilihali ndoa zinafungwa? Ukishaanza kuhamasisha watu wasifunge ndoa huwezi sema umefanikiwa baada ya ndoa kufungwa na kuvunjika, unafanikiwa kwa ndoa kutokufungwa.

Kumbuka katika ndoa zinazofungwa, zile zenye amani hazifunguliwi nyuzi au zinafunguliwa chache. Hizi zenye matatizo ndizo zinazofunguliwa nyuzi nyingi.
 
Ni dhalau mkuu, ndoa hiyo iko ICU .kumbe kumpost mwanaume ambae sio mmeo ni rahisi kivile?

Ahaaaaa imenibidi niche, mimi na uzee huu sijawahi mpost mwanaume yeyote, hope na my ex sikuwahi mpost

Ila siku nampost nitapost brand new na atakuwa mwanaume wa kwanza na wa mwisho kumpost chini ya ardhi hii.

Sasa baada ya kukuliwaza na kukupa moyo utoke kwenye hali hiyo ndo anaanza kukuumiza na michepuko yake?

Sijasema muachane ila nawaona mahakamani mwakani na divorce pole in advance karibu sana mahakamani mwakani feb kuanzia kama trh 15 kesi mpya zikiwepo yako zitakuwa zinasikilizwa.

Kwa kipindi hiki jifanye mjinga na usimuulize maana na usifanye mapenzi nae maana toto litakalo tokea wenda asiwe wako.

Mmh hii comment chonganishi 🤣
 
Samahan kijana wa miaka 29! Unaweza kutuma hizo charting za kusifia angalau tujue ukubwa wa tatizo lipo kwa namna gan??
 
Hakuna kitu nakiogopa kama ukoma kumdharau mtu sababu ya kipato chake au maumbile yake. Mtu wa hivyo hana exposure.
 
Shetani anapiga patrol hapo anataka achukue point 3 Mungu kashampa go ahead nenda kwa mtumishi wangu Ayubu mjaribu unavyoweza Ila tu usimuue, sasa kaanza kucheza na akili yako Mzee ukiileta mihemko utaharibu ndoa kwan shillings ngapi shemu haumgongi au napo pia anakubania?
Acheni kumqingizia shetani. Hizo ni tamaa tu za wanawake ambao hawajui maana ya maisha na mahusiano. Kama hujawa tayari kuolewa, usipotezee mwenzako muda. Tafuta hao wenye maisha mazuri sio unaenda sijui kanisani unaapa kwa shida na raha ili hali moyo umejaa unafiki.
 
Mens niko kwenye ndoa miaka 3,tangu mwaka jana nimekua kwenye hali isiyo nzuri financially,sasa majuzi nacheki status naona wife kapost mwanaume rika langu kanunua ndiga akapost na chattings zao za kupongezana.

Sikuona wivu kwamba jamaa rika langu kavuta chuma mimi sina ila nilifedheheka baada ya kupita kitaa mashost wa wife wanaongea kwa kebehi kwamba "mke wake anapost wanaume wenye magari ilihali mumewe hana" asee nimejikuta nina hasira za ajabu na msongo,natokaje kwenye huu mtego msaada tafadhalini..
Mkuu kwani kabla ya kumuoa mlipitia kwenye atua ya uchumba, kwani yeye kwao wana magari au kama ana kaka zake au wadogo zake wakiume wana miliki magari.
 
Naunga mkono hoja, kuna wanawake ni shenzi type kabisa.
Unakuta mke wa mtu anapost kabisa eti "leo nna hamu ya kula kuku nani aninunulie"? Siriazi ?

Mwanamke wa aina hiyo hafai ni wakupiga chini ili aende kwa hao wenye magari aone kama wana muda nae baada ya kuliwa.
Sasa kama hawezi hata kujinukulia kuku hata wa broiler mpaka atoe matangazo ,huyo iko na shida sehemu
 
Hivi hata kama mtu lets say kijana kamaliza chuo na hajapata kazi , hivi anaweza kudharaulika mpaka na wazazi wake na hata ndugu zake? Maana kuna kijana mwenzangu hapa anapitia hiyo changamoto hadi stage ya kunyimwa msosi home kwao!
Mkuu hiyo familia inafanya makosa makubwa na inajenga roho ya ajabu kwa watoto wao, mfano watoto wakike wa familia hiyo wakija kuolewa wataendelea kuwafanyia matendo mabaya waume zao kipindi wakiwa kwenye hari ngumu ya kiuchumi.
 
Kabisa wazazi hawajui ugumu wa kazi saiv wana ile mentality ukimalza ajira unapata huanze kuwasaidia.
Mkuu inategemea na aina ya wazazi, wazaz wa mjini wanajua hari halisi ya ajira kwa sasa, Wazazi wa vijijini wakulima hawajui mifumo ya ajira kwa sasa wao wanachojua upo mjini pesa unazo na hawajui aina gani ya kazi ina maslahi mazuri .
 
Back
Top Bottom