Anapost wanaume walionunua magari na chattings zao status wakati mimi niko kwenye hali ngumu kiuchumi

Anapost wanaume walionunua magari na chattings zao status wakati mimi niko kwenye hali ngumu kiuchumi

Mens niko kwenye ndoa miaka 3,tangu mwaka jana nimekua kwenye hali isiyo nzuri financially,sasa majuzi nacheki status naona wife kapost mwanaume rika langu kanunua ndiga akapost na chattings zao za kupongezana.

Sikuona wivu kwamba jamaa rika langu kavuta chuma mimi sina ila nilifedheheka baada ya kupita kitaa mashost wa wife wanaongea kwa kebehi kwamba "mke wake anapost wanaume wenye magari ilihali mumewe hana" asee nimejikuta nina hasira za ajabu na msongo,natokaje kwenye huu mtego msaada tafadhalini..
Huyo ni mkeo au ni demu tu
 
Ila wanaume wa sikuhizi tunapoteza pambano kirahisi Sana mbele ya wanawake
 
Kaa kimya usiongee Chochote wala usifanye chochote. Chochote utakachofanya sasa kitakuwa ni zao la hasira na huzuni hakitakuwa na matokeo mazuri baadae.

Kaa kimya tazama mustakabali wako kama mwanaume asiye na gari halafu anaishi na mwanamke mwenye tamaa.

Ushauri kwa wanawake. Mnaona namna huyu jamaa analalamika hapa maumivu anayojiskia mwanamke wake kupost mwanaume mwingine mwenye gari ila akiishi na mwanaume asiye na gari (wenyewe mnaita kuvumilia). Huyu bwana MUNGU akimkunia nazi akanunua gari na kuwa na mafanikio zaidi ya huyo anaempost then utakuja sikia analalamika mwanaume amebadilika baada ya kupata mafanikio kumbe anasahau dharau na treatment za kudhalilisha alifanya siku za nyuma.
 
Hivi ni mm na ushamba wangu au mwanamke akiolewa anatakiwa achunge anachopost hasa kinachohusu wanaume wengine ambao si ndugu zake!
Yaani hata namna anawasiliana na baba yake na kaka zake huwa inakuwa sio kama alivyokuwa single sembuse kupost mwanaume mwingine ambaye hana udugu nae.
 
Mpaka anafikia kupost, shida ni kubwa sana mkuu. Na haijaanza hapo hayo ni matokeo tu. Kuna asilimia kubwa sana anakudharau au analiwa kabisa.

Kikubwa ulitakiwa kuwasha moto kuhusu hiyo ishu, sometime wanaume tunakwama kwa kupuuzia redflag kama hizo.

Wewe ni mwanaume na kiongozi wa hiyo nyumba, nafasi yako kwa mkeo haipimwi kwa hali yako ya uchumi, Mungu alikuumba uchi kabisa but still ulikua na mamlaka kama mwanaume.
 
Mens niko kwenye ndoa miaka 3,tangu mwaka jana nimekua kwenye hali isiyo nzuri financially,sasa majuzi nacheki status naona wife kapost mwanaume rika langu kanunua ndiga akapost na chattings zao za kupongezana.

Sikuona wivu kwamba jamaa rika langu kavuta chuma mimi sina ila nilifedheheka baada ya kupita kitaa mashost wa wife wanaongea kwa kebehi kwamba "mke wake anapost wanaume wenye magari ilihali mumewe hana" asee nimejikuta nina hasira za ajabu na msongo,natokaje kwenye huu mtego msaada tafadhalini..
Ongea naye kabisa ajue mapema isee faster mwambie asimame kwenye himaya yake na akumbuke wewe ni nani hayo yote yanapatikana mkiwa na umoja navision kubwa.
 
hizi ndoa siku hizi zimepoteza maana kabisa yaani. Pole sana kiongozi.
 
Hata mi nashangaa pia sio wanawake tu hata wanaume wanaonunua magari na kudharau wengine na kuona gari ni kitu cha maana sana au wanaume wanaoona kuwa mwanaume mwenzake akimiliki gari kama ana maisha mazuri. Mimi nina magari 2 (langu na la wife) ila sijawahi ona uthamani wake hadi ninyanyase au nidharau wengine kwa namna yoyote. Napakiza yoyote mtoto au mkubwa. Mgonjwa au mzima. Kukiwa na ugonjwa au msiba huku Kijijini ninapoishi huwa Natoa gari 1 hususani ninalolitumia mimi kwa ajili ya shughuli za kijamii.

Pole na Mungu akusaidie bro. Usijihukumu wala kujisikia vibaya. Gari sio kitu mkuu. Pambana kaka.
Acha uongo mzee huna hata guta
 
Hivi unaanzaje kupost status picha ya mwanaume na charting juu..huu ni uongoo..kama ni ukweli huna mke una kichenchede...
Haipo na haitakaa iwepo....
 
Hivi unaanzaje kupost status picha ya mwanaume na charting juu..huu ni uongoo..kama ni ukweli huna mke una kichenchede...
Haipo na haitakaa iwepo....
Ndugu huo ni ukweli mimi iliwahi nitokea kwa mpenzi wangu mimi sijawahi postiwa nina mwaka mzima ila katika huo mwaka kuna rafiki yake mwenye gari kapostiwa mara 3 ilikuwa inauma sana
 
Back
Top Bottom