Anataka kuacha ajira ya kudumu ajikite kwenye kilimo

mwenyewe bado sielewi anaomba ushauri upi
 
mi nliacha kazi na mil 6 benk... na siji kuajiriwa tena
 
Ualimu si taaluma hiyo hata kama akiacha bado anaweza kuja kupata hata private mwambie asiogope kuacha kazi maisha yatasonga tu hata kwa aje. Yaan
 
Nimesoma comments za watu humu JF kama huna msimamo huwezi toboa. Kuna watu wanalaumu kilimo ni umaskini wakati hicho kisa jamaa katusua 180m. Wengine wanalaumu ajira ni umaskini. Sasa mnamshauri nini hapo zaidi ya kumtengenezea jamaa confusion jamaa wa watu. Mimi ningekuwa huyo jamaa ningekaba kote kote kwa muda mfupi. Kwa mfano kama alipiga 180m kwa mwaka. angeweka 100m kwenye kununua hisa kwenye mabenk au fixed accounts. Mwaka mwingine apambane tena aweke 100m. akifanya hivyo kwa miaka mitano atakuwa na zaidi ya 500m. Baada ya hapo ni mwendo wa kuachana na ualimu na kujikita kwenye biashara maana faida ya kila mwaka kwenye hisa tu inatosha kucover basic life necessities.
 
Mil. 180, na kukaa darasani , hivi vitu viwili huwa havikai pamoja. Nashauri aendelee na mil. 180!
 
Hiz za kukoboa mpunga size ndogo inaeza kuwa Bei gan
Zipo ndogo Hadi 6M ila nzuri ni zile kubwa za kuanzia 24M plus , asiogope hizo mashine anaweza kukopa hata ya 50M na Bado akabaki na mtaji wake, namshauri aende Benki ya Kilimo watamsadia sana kumshauri na kumpa mkopo, kigezo Chao Cha kupata mtambo wa kusindika Mpunga uwe na Shamba ekari kuanzia 70 wanakumpa Mkopo wa Trecta , wanakujengea warehouse store/ Godauni, Riba ya ni 10% Kwa mwaka, au waone NMB agribusiness department au Nenda EFTA wanatoa mikopo ya matrecta na mitambo bila Dhamana una Deposit25% ya gharama kamili ya chombo husika ribs 16%
 
Kaa mbali na kilimo.

Kaka Hawa efta unawapelekea list ya mitambo kama lengo ni mashine za kukoboa mpunga, kukoboa mahind na kusaga mahind Kisha wanafanya hesabu wanakulipia kwa ww kulpa 25% km malipo y kwanza au za kusaga hazihusiki ni y kukoboa mpunga tu?
 
Nakumbusha jaman mafao ya huyu mtu ni 33% tu ndio atakayopewa anapostaafu ko penshen haitafka hata 70m.
 
Sawa tuu awamu ya 6 kilimo.kinalipa na kilimo ni biashara inaweza kukupa pesa nyingi za haraka na Kwa pamoja ukapata mtaji tofauti na hizo kazi za kupimiwa level zako za maisha.
 
Aingie shamba asiogope.. ajira haijamaliza Kila kitu kwenye maisha. Mm mzee wangu pale Masaki Dr. Xxxxxxx ameacha kazi Ocean road pale udaktari na amejikita kwenye kampuni yake na biashara zake. Hata wabunge wenyewe wanasubiri mana amefungua ofisin mpaka Uganda
 
Kama ana uwezo wa kupata hizo pesa kwa mwaka mmoja kupitia kilimo na anajishauri kwa kuogopa basi hajui analolifanya.

Hiyo pesa inaweza mfanya afungue biashara nyingine za kumuingizia pesa na asijute. Mfano hardware inaweza kumfaa kwa kuanzia 20M tu. Na 60M akawekeza UTT ikawa mbadala wa take home salary ya ualimu kila mwezi. Halafu 100M anairudisha shambani. Baada ya hapo kazi yake itakuwa akitoka shambani anaenda kushinda kijiweni kwake kwenye hardware pale ambapo shughuli hazijambana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…