Hamna mtu mwenye alama wala sijui nini, ila kila mtu anatabia yake. Hilo uliloliongelea sijui kusameheana na kuvumiliana mwenzako alishalishindwa na akavunja hadi ndoa na familia pamoja na kukuachia umasikini, sasa wewe unataka utudanganye nini tena hapa. Uvumilivu umemshinda akakimbia ndoa, na akaivunja, je hiyo ndio dhana ya uvumilivu au kutuletea maigizo kwenye ndoa. Unatuambia hiyo ndio ndoa ilivyo, 😂😂😂 kwamba ndoa ndio mnavumiliana kwakuivunja na hata kusambaratisha familia kisha urudi mara ya pili. Hapo ndio kukosa uvumilivu sasa. Kwamba na mwanaume naye avumilie kwakuikimbia familia halafu kesho arudi😂😂😂, hivi nyie kwanini hamkomboleki na mnajichimbia kaburi wenyewe. Point ni vumilia ila kamwe usijaribu kuivunja familia, otherwise huo ni utoto, ubinafsi na upumbavu, achana na ndoa kabisa haikufai.