Anayejua anachokisimamia Dkt. Slaa kwa sasa atuambie

Kwa akili zako finyu huwezi kumwelewa
 
Kwa hiyo mtu akishakufa tuhuma hakuna?!
 
uyu mze namkubali tena sana na chadema ni chama changu ila kosa walilofanya kama chama ni kumkaribisha mamvi na kumteua agombe uraisi hapo ndo tatzo lilipoanzia,wangemwacha slaa agombe mana alikuwa anaitikadi kama magufuli kwenye mambo ya ufisadi akibua hoja nchi ilikuwa haikaliki,kwa kifup upnzani wakweli na imara ulikuwa enzi za huyu mwamba dk slaa ungekuta upnzani unaongonza nchi kupitia huyu mwamba wa kaskazini na tuache unafki mamvi alikuwa fisadi tena mkubwa sana miaka yote tulikuwa tunamnanga kwa ufisadi wake alafu tunamkaribisha aje agombee uraisi, hapo ndo tatzo lilipoanzia namkubali sana slaa ila chadema ni chama changu ila naona kwa sasa ameshapoteza mvuto sababu mainzi ya kijani yameshampaka mavi
 
Ndugu umehemka sana relax.
 
Magufuli alipinga Ufisadi ?
 
Chadema hipi ambayo haijafa?hii yenye mbunge mmoja na COVID-19 🤣🤣🤣ndani ya Chadema ndani kuna mpasuko mkubwa, Kuna wanaounga mkono akina COVID-19 na wanaopinga, Chadema haiko Salama kama unavyozania.
 
Kwani mbona Ni muda mrefu tunaambiwa upinzani unakufa haufi wanakufa wao, Hata mzee slaa atakufa upinzani atauacha.
 
Inawezekana kuna jambo unajaribu kulielezea, lakini hujapata njia nzuri ya kulieleza likaeleweka kirahisi.
Ngoja mimi nijaribu kwa kifupi, kama hivi ndivyo unavyowaza juu ya CHADEMA.
Mbowe, ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA, na ambaye bila shaka anapozungumza anawakilisha mawazo ya chama hicho, kisha eleza yaliyozungumzwa kati yake na Samia walipokutana baada ya kutoka jela. Hili linaeleweka, na sina sababu ya kuyarudia hapa waliyoazimia kuyafanya.

Sasa niambie, katika muda huu mfupi, na ukizingatia hayo waliyokubaliana, utategemea vipi CHADEMA waonyeshe yale yale waliyokuwa wanaonyesha wakati wa Magufuli, wakati ambapo walikuwa wakiwindwa kupigwa virungu, kuwekwa mahabusu, na hata kutishiwa kuuwawa?
Hilio moja.

La pili, hata kama halina uzito mkubwa kwa sasa; anayoyasimamia Samia ndani ya chama chake, na matamanio ya mafanikio anayotarajia kwenye utawala wake, hayana tofauti kubwa sana na yale yanayotamaniwa na CHADEMA, kisera. Tofauti pekee iliyopo kwa sasa kati ya CCM ya Samia na CHADEMA ya Mbowe, ni kushikilia, au kutafuta madaraka ya kuongoza nchi. Samia hataki katiba mpya, siyo kwamba haoni ubovu wake, ila katiba hiyo inampa wigo zaidi wa kumbakisha madarakani.
CHADEMA wao wanaona Katiba hii ni kizingiti kikuu kinachowanyima fursa ya kushika madaraka, kwa hiyo watafanya kila juhudi, ipatikane Katiba Mpya.
Sasa basi, kama bado unaona CHADEMA wamenyang'anywa agenda ya mambo ya kusimamia, ikiwa ni pamoja na hili la Katiba Mpya, hapo nadhani labda una maana nyingine ambayo bado hujaielezea hapa ili tukuelewe vizuri.

Uwanja ni wako.
 
Anasimamia kweli.

Mbowe asipokomaa upinzani utakufa rasmi!
Bwashee, upinzani ni uwepo wa mawazo kinzani na mbadala. Kitu hicho hakiwezi kufa bali kujibadili au kujinyumbua.
Kinyume chake ni ukondoo au mtindo wa kibatabata.
Vyama vyawerza kufa lakini upizani hapana. Wazo kinzani huzaliwa ndani watu na kwa pamoja hujongea.
 
In short Dkt Slaa ana msimamo, kamwe siyo bendera fuata upepo.
 
Mzee wetu nae mayala(njaa)inamsumbua Kama anataka kurudi chadema aombe
 
Navyojua kadri mwanadamu anavyozidi kuzeeka ndio akili yake inarudi kuwa kama ya mtoto, hivyo simshangai huyo babu.
Umeniwahi nilichokuwa nafikiria kukiandika, bravo[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Kwa bahati mbaya sana, uliyempa somo hili (uliyemjibu) aidha hana uwezo wa kuelewa au ni mtu ambaye hana umakini wowote na majibu kama haya. Nasema hili, kutokana na uzoefu na mtu huyo hapa hapa jamvini. Leo utamueleza jambo rahisi alielewe, kesho unakuta anabwatuka tena na yale yale uliyojaribu kumfundisha.

Umejitahidi sana kumpa somo zuri hapa, lakini najua halimwingii akilini.
 
Akafe mbele tu, kwa umri huo ni anaongeza mabadiliko ya tabia nchi ameshakuwa mzoga unaopumua.....
 
La kwanza unasema kuwa sasa hivi CHADEMA hawana sera kwa vile Mbowe ambaye ndiye chama chenyewe alikuwa na msukosuko kwa hiyo anahitaji kufanya maandalizi. Ninakubalina nawe kuwa Mbowe anahitaji maandalizi baada ya msukosuko huo. Binadamu yeyoyte akipitia muda mgumu aliopitia, ni lazima apewe muda wa kujipanga upya. Hata hivyo unakubaliana nami kuwa CHADEMA kama chama hakina sera, kinategema matamko ya Mbowe tu.

la pili, unarudia yale ya zamani kwa lugha tofauti kuwa Samia anasimamia mambo ambayo CHADEMA nayo ndiyo wanayotaka. Ni kama tulivyowahi kuambiwa zamani kuwa Chadema inataka kufufua ATCL, TRC na kuimarisha elimu. Magufuli alipofanya mambo hayo hayo hayo wakampinga kwa nguvu sana hadi kuyaita maendeleo ya vitu. Kwa hiyo la pili inawezekana unalisema wewe kwa logic yako tu lakini siyo msimamo wa CHADEMA ambao walishajitanabahi kuwa wao ni chama mbadala kwa maana ya kutokukubaliana na CCM kwa kila kitu, ila wananatoa mbadala, ambao sasa hivi hawana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…