Anayejua dawa ya kuua hawa wadudu anisaidie

Bora uliwawahi.
Unaweza jikuta inaingia gharama za kuezeka upya.
haha waliniwahi mzee, maana walishaanza kulia ( wale dumuzi wadogo siyo wale wakubwa )
nikamwaga oil nyingi sana, nilinunua dumu za lita 20 nne nikakodi na compressor lile ya kupakia rangi magari
nikapandisha juu kule, walinitia hasara sana pumbav hao
 
Pole sana mkuu.

Ila kama ishazibwa na magypsum wanaweza kufikia kenchi kweli?
 
Tumia sabuni zenye acid zile za kuoshea chooni kwenye tile zilizo fubaa... Zipo madukani. Weka kwenye chupa au kifaa kinachoweza ku spary kama unavyo spray perfume...
Then spray kwenye hizo sehem.

Me nilifanya hivyo kwenye mlango ulikuwa unaliwa na mchwa.... Walipotea wote ghafla... Puliza kwa wingi Kila siku ulete majibu.
 
nadhani zile mbao zilikuja tayari zina mayai yao huko zilikotoka

na mayai yao huanguliwa mpaka miezi 6 huko,

ikumbukwe hao wadudu wanaruka, anatoka nyumba ya jirani anakuja kwako, anataga mayai.
Ipo haja ya kupiga midawa ya kutosha kabla ya kuezeka.Na zile za blandaring ziwe treated kuepuka hiz stress
 
Asante kwa ushaur mkuu
 
Kila nikiiona avatar yako, mie roho kwatuuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…