Anayejua kuhusu huyu Roboti wa Tanzania anisimulie vizuri. Naona mitandaoni amekua gumzo

labda angetengenezwa na watanzania kuonyesha kazi ya vijana wetu ni sawa tuna la kujivunia
 
Mimi leo nimeshacheka hadi basi, bora angekuwa robot wa mtaani ila sio wa kwenda kupelekwa hadi bungeni.
Hii nchi sijui tunaweza kufanya nini kwa usahihi, sanamu ya Nyerere tu ilitushinda!
Aisee angekua mtu binafsi ingekua sawa lakini si serikali ya 78B GDP
 
Kifupi si kila technologia lazima iwe ina uhusiano na maji na umeme!

Naomba nikuweke sawa hapa!!
Ingawa wameboronga lakini kila kitu kuhusianisha na mwananchi wa kijijini au wa huko nachingwea au namtumbo si sawa
Hivi kwa nini mnapenda kutudhihaki sisi wa Namtumbo(kwa mama) na Nachingwea?(kwa baba)
 
Sijavutiwa na huyu robot Eunice kama nilivyokuwa navutiwa na kile kikaragosi cha miaka ile kilichokuwa kikichezeshwa huku kikiwa na bonge la msambwanda na kikijulikana kama Joyce Wowowo.
 
Sijavutiwa na huyu robot Eunice kama nilivyokuwa navutiwa na kile kikaragosi cha miaka ile kilichokuwa kikichezeshwa huku kikiwa na bonge la msambwanda na kikijulikana kama Joyce Wowowo.
sijakiona hicho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…