Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Mazoea yana tabu,watu walizoea ujanja ujanja tu,sasa haki inetawala walalia.....aendelee binafsi najua anakotopeleka
 
Habari zenu wakuu..!

Kuna swali nimejiuliza, ilikupata jibu sahihi, nimeona sio vibaya nikiwashirikisha na nyie pia.

Utawala uliopita hali ilikuwa ngumu sana kwa masikini wa nchi hii. Mfumo uliokuwepo, uliwaneemesha sana matajiri. Ila huu mfumo uliopo sasa, umewabana sana matajiri. Cha kushangaza hata masikini waliokuwa na hali mbaya awamu iliyopita nao wanalia, tena kwa wingi.

Sasa wasiwasi wangu ni juu ya hiki kilio cha "..anko Magu kabana.." wanacholia watu wa tabaka zote, ni kweli kinatuhusu sisi makabwela au tunaomboleza msiba wa mabwana wakubwa wetu?
Maana anasikia watu wakisema "habari ya tajiri muulize masikini, na habari ya masikini muulize masikini mwenyewe"
 
Mimi siyo mchumi, ni lay person, lakini kuna eti kitu kinaitwa "multiplier effect"................ simple concept to grasp anyway, consult your search engines.........................
 
wanasema n kilio cha wapga dili, sasa cjui vjana waliokosa mikopo na ajira nao walkua wapga dili?. je wakulma wanaolia uko vjijin nao walikua wapga dil? uku mitaan nako kuwekuwa kwa moto balaa hupatkanaj wa pesa umekuwa mgum balaa. ngoja 2endelee kuamnishwa kuwa jamaa anainyoosha nch
 
Tunakoelekea ni kazi tu.
Tulipoanzia ni kutumbua wafanyakazi hewa na kutengeneza afya bora kwa wafanyakazi wetu na Elimu bora .
Kwa sasa tuko na kazi ya kukusanya Kodi na kuweka taratibu sahihi wa matumizi sahihi ya Kodi .
Hivi Nov tulikusanya ngapi mkuu?
 
Habari watanzania wenzangu najua wengi tunamaliza mwaka tukiwa hoi bin taaban kutokana na mbinyo wa kodi mbali mbali ambazo haziendani na kipato halisi cha mtanzania wa kawaida.biashara zimekua ngumu saana hata zile tunazo aminishwa za Eac. mipakani kodi zimekua kubwa watu wa nashindwa kusafir kifupi serekali imeshindwa kubani njia yyt mbadala zaid ya kuwakamua watanzania wa kipato cha chini Kati na juu.nikiwa mwanachama wa ccm japo sina card ya chama lakini nilipiga kura tatu ili kuunga mkono chama changu na kwa mtu mwenye ndoto zangu Mh john magufuli.naandika waraka huu nikiwa na machungu moyoni kwani ni mmoja wa wengi walio amua isiwe taabu kama ni ofic Acha nifunge nimeamua kurudisha kwa mwenyewe kwa sababu siko tayar kulipa ml9 kwa mwaka na biashara hakuna.hali ni zaidi ya ngumu huku uraian simaanishi au napingana na uendeshaji wa nchi wa muheshimiwa rais ila nalia na kodi nyingi ambazo hazina tija ila zaid ni komoa nikukomoe. Tuachane na hili tuje suala la tanesco na hili ongezeko la 18%jaman waibe wangine tulipe wengine Muheshimiwa rais wangu kama utalikalia kimya hili na kulibariki rasmi sinta kukubali tasmi tena na nitakaa pembeni na chama chako cha ccm
 
Upo hoi peke yako. Mie nilishajizoelea kulipa kodi, ukwepaji kodi kwangu ulikuwa mwiko. Kutoa au kupokea rushwa kwangu ilikuwa mwiko. Hayo yamenifanya nisione huu ugumu mnaoulalamikia ninyi.
 
Tulishaambiwa na Mtangazaji wa Clouds tv Hassan Ngoma kuwa kama tunaona upatikanaji wa Hela / Pesa ni mgumu basi tuanze kutembeza Ice Cream katika Madeli na kuzunguka nayo mji mzima ili tupate ' mtonyo ' au Wewe hukumsikia Mkuu?
 
Mkuu tutatembeza ice cream wote
 
Upo hoi peke yako. Mie nilishajizoelea kulipa kodi, ukwepaji kodi kwangu ulikuwa mwiko. Kutoa au kupokea rushwa kwangu ilikuwa mwiko. Hayo yamenifanya nisione huu ugumu mnaoulalamikia ninyi.
Wewe utakua sio mfanya biashara huenda ni mkulima subir mvua
 
Upo hoi peke yako. Mie nilishajizoelea kulipa kodi, ukwepaji kodi kwangu ulikuwa mwiko. Kutoa au kupokea rushwa kwangu ilikuwa mwiko. Hayo yamenifanya nisione huu ugumu mnaoulalamikia ninyi.
Umezoea kulipa kodi nakupongeza ilo
Ila wewe sio mfanya biashara wa kununua na kuuza Bidhaa Kama mfanya biashara wewe ni bodaboda
 
Wewe utakua sio mfanya biashara huenda ni mkulima subir mvua
Jiaminishe hivyo. Mlipokuwa mnaibia serikali mlijiona wajanja sana, halafu sisi tuliokuwa tunalipa kodi mlituona wajinga, mbaya zaidi hata baadhi ya wafanyakazi wa TRA walituona wanoko kwa kujifanya tunajua kufuata sheria. Sasa hivi mmebanwa mbavu halafu mnalazimisha eti kiwe kilio cha kila mfanyabiashara. Lipeni kodi, mkiona biashara imewashinda fungeni mkatafute kazi zingine mnazoweza.
 
Upo hoi peke yako. Mie nilishajizoelea kulipa kodi, ukwepaji kodi kwangu ulikuwa mwiko. Kutoa au kupokea rushwa kwangu ilikuwa mwiko. Hayo yamenifanya nisione huu ugumu mnaoulalamikia ninyi.
Ni ngumu kuelewa ni ngumu sana
 
Umezoea kulipa kodi nakupongeza ilo
Ila wewe sio mfanya biashara wa kununua na kuuza Bidhaa Kama mfanya biashara wewe ni bodaboda
Usilazimishe ukwepaji kodi wako ukadhani kila mtu alikuwa anafanya hivyo. Dawa ya kuwa salama ni kufuata sheria na siyo kuwa mjanja wa kukwepa sheria. Hata ukiamua kusema mimi siyo mfanyibiashara sawa, labda ndivyo unavyoona ni rahisi kwako kujipa matumaini. Ila ukweli ni kwamba biashara za ukwepaji kodi mwisho wake ndio huu mnalialia. Kama uliamua kukwepa kodi basi pia uwe tayari kubeba kadhia zake.
 
Ukiona kodi inakushinda katika biashara yako ujue hukuwa na sifa za kufanya hiyo biashara tafuta ya daraja lako utamudu tu Sijaona kama serikali imetunga sheria mpya za kumkomoa mwekezaji au mfanyabiashara Bali imeamua kusimamia hasa sheria zilizokuwepo kabla ya serikali ya awamu ya tano kama wewe uliweza kumudu biashara kabla ya awamu ya tano ujue wazi kuwa usimamizi wa sheria hakuwa na ubora unaotakiwa hivyo basi ushauri wangu kwako Fanya biashara ya daraja lako siyo hiyo uliokuwa unaifanya kwa kukwepa kodi..
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…