Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Mwalimu wangu wa biashara 1987 aliniambia (if you do not know where you are going any road will take you there) tulikuwa kwenye somo la kuandika business plan kwamba kabla ya kufanya biashara yoyote lazima uwe na mpango wa biashara uliondikwa fanya makosa kwenye karatasi siyo kwenye biashara ( sit on our pants and make mistake on papers not in business)
 
Huu utumbuaji wa maigizo tumeichoka sasa. Kama kila anayefanya kosa anatumbuliwa basi ni muda muafaka JPM ajitumbue mwenyewe kama sii kujiuzulu. Yeye ndye kaleta hii zana ya one mistake go home. Hata yeye pia kafanya blandaz nyingi kuanzia sakata la sukari. Na yeye ajitazame kwa jicho la tatu Kama ni mzalendo wa kweli.

Ni wazi kuwa serikali imemshinda. kama wizara zilizo chini yake zinafanya mambo makubwa na mazito bila kumuhusisha yeye mpaka mchakato unaisha. Inabidi na yeye ajiulize ni kwa nini? ( in condition kama haya sio maigizo)
 
Kwa katiba ambayo iko sawa na inafuatwa bunge ndiyo linatakiwa limtumbue raisi.
Kwa maoni yangu, Ukiachilia swala la one mistake go home, vile kuwa na matumizi ambayo hayajapitishwa na bunge inatosha kwa bunge kuonesha halina imani na raisi kwa kua yeye hana imani na bunge.

Lakini siioni Tanzania ya kumtoa kiongozi mkubwa kama waziri mkuu au raisi kwa sasa kupitia kura ya kukosa imani na kiongozi husika.
 
Tumpe muda

3 years is nothing compared to our anger!

anaweza badilika.

Hasa jua likiacha kutokea mashariki!
 
Kwa katiba ambayo iko sawa na inafuatwa bunge ndiyo linatakiwa limtumbue raisi.
Kwa maoni yangu, Ukiachilia swala la one mistake go home, vile kuwa na matumizi ambayo hayajapitishwa na bunge inatosha kwa bunge kuonesha halina imani na raisi kwa kua yeye hana imani na bunge.

Lakini siioni Tanzania ya kumtoa kiongozi mkubwa kama waziri mkuu au raisi kwa sasa kupitia kura ya kukosa imani na kiongozi husika.
Issue sio katiba. Kinachohitajika ni uzalendo tu. Uongozi wa nchi sio kitu cha mchezo. Ukiona sio size yako unakaa pembeni unaachia wengine sio kufanya majaribio huku anatuvurugia uchumi wa nchi yetu.
 
Malisa acha kulialia, inabidi ujifunze kuheshimu mawazo ya wenzio.

Kwa taarifa yako dhambi ya kubadili gia angani na kuuza chama kwa mafisadi itawatafuna milele na huu ni mwanzo tu.

Chadema ya Leo ni watetezi wa kila aina ya maovu ya nchi hii .

Kubenea anajaribu kuweka hadharani usanii wa viongozi wa chadema lakini wewe Malisa na bavicha mnajaribu kuficha!!!

Kumbuka hata ulipoenea uvumi kwamba lowasa ameuziwa chadema na atagombea urais, ulijitokeza kupinga sana habari hizo, lakini leo ndio muogeshaji na mbeba viatu mkuu wa lowasa!!!

Bado unatakiwa kuaminiwa tena na jamii???
 
Kwakua ameahidi kuwalinda watu, wale walioahidiwa kulindwa sidhani kama wataridhika wakisikia raisi anataka kuachia ngazi. Wala hawataridhika wakisikia wabunge wao wanataka kumwachisha ngazi raisi.

Concept ya uzalendo ni pana sana, kwa Tanzania haitekelezwi hata robo yake siyo kwa viongozi wanaouza wakina Faru John na Twiga siyo kwa wananchi tunaoacha hayo yakitokea na kupita kimya kimya.
 
"...kuna watu TANESCO wanafanya hujuma za kukata umeme ili muichukie serikali msiichague CCM. Nawaambia wajiandae kuondoka nikiapishwa" JPM 2015

"...Kuna watu hawana huruma. Wanafungulia maji ili wauze mafuta. Tutawashughulikia" 2015

"...Nilipewa urais kushughulikia mashetani. Nataka nianze kushughulikia na huyu TANESCO" JPM 2016

..Uhusiano uliopo kati ya maneno haya na yaliyotokea ni wazi kabisa kuwa ni muda tu ulikuwa unasubiriwa!!
Sasa tumeona na tutazidi kuyaona mashetani yakitembea duniani..!!
 
Malisa acha kulialia, inabidi ujifunze kuheshimu mawazo ya wenzio.

Kwa taarifa yako dhambi ya kubadili gia angani na kuuza chama kwa mafisadi itawatafuna milele na huu ni mwanzo tu.

Chadema ya Leo ni watetezi wa kila aina ya maovu ya nchi hii .

Kubenea anajaribu kuweka hadharani usanii wa viongozi wa chadema lakini wewe Malisa na bavicha mnajaribu kuficha!!!

Kumbuka hata ulipoenea uvumi kwamba lowasa ameuziwa chadema na atagombea urais, ulijitokeza kupinga sana habari hizo, lakini leo ndio muogeshaji na mbeba viatu mkuu wa lowasa!!!

Bado unatakiwa kuaminiwa tena na jamii???

Chadema wapi imetajwa kwenye mada?

Habari za Lowassa ni za mwaka gani?

Au umezoea kuzungumzia tu mabaki ya chakula cha jana tumboni hadi unasahau leo nini utakula?

ACHENI MAIGIZO!
 
Kwa katiba ambayo iko sawa na inafuatwa bunge ndiyo linatakiwa limtumbue raisi.
Kwa maoni yangu, Ukiachilia swala la one mistake go home, vile kuwa na matumizi ambayo hayajapitishwa na bunge inatosha kwa bunge kuonesha halina imani na raisi kwa kua yeye hana imani na bunge.

Lakini siioni Tanzania ya kumtoa kiongozi mkubwa kama waziri mkuu au raisi kwa sasa kupitia kura ya kukosa imani na kiongozi husika.
Watafanya hicho unachofikiria ww endapo atatumia fedha kwa manufaa yake binafsi, usidhani anachukua pesa kienyeji bro, unajua sisi tunaopata viuzushi kwenye mitandao tunaona kama anafanya kosa, lakini sheria inamruhusu kufanya anavofanya bro. Na yote anayoyafanya ni kwa faida yetu sote ntakushangaa sana kulalamika kanakwamba hayo maendeleo yanafanyika Kenya au Uganda.
 
Siwezi kujilaumu kwasababu sikumchagua coz bilijua tu pombe sio mtu makini kwenye uongozi na cku zote nitaendelea kuwalau waliomuingiza pombe madarakani
 
Malisa acha kulialia, inabidi ujifunze kuheshimu mawazo ya wenzio.

Kwa taarifa yako dhambi ya kubadili gia angani na kuuza chama kwa mafisadi itawatafuna milele na huu ni mwanzo tu.

Chadema ya Leo ni watetezi wa kila aina ya maovu ya nchi hii .

Kubenea anajaribu kuweka hadharani usanii wa viongozi wa chadema lakini wewe Malisa na bavicha mnajaribu kuficha!!!

Kumbuka hata ulipoenea uvumi kwamba lowasa ameuziwa chadema na atagombea urais, ulijitokeza kupinga sana habari hizo, lakini leo ndio muogeshaji na mbeba viatu mkuu wa lowasa!!!

Bado unatakiwa kuaminiwa tena na jamii???
km si uwendawazimu basi uchizi unakumendea
 
Hivi malisa kaingiaje humu?
 
Watafanya hicho unachofikiria ww endapo atatumia fedha kwa manufaa yake binafsi, usidhani anachukua pesa kienyeji bro, unajua sisi tunaopata viuzushi kwenye mitandao tunaona kama anafanya kosa, lakini sheria inamruhusu kufanya anavofanya bro.
Kwanini unadhania kua kutumia pesa ndiyo kunatosha kupiga kura ya kukosa imani?

Hata maamuzi ambayo yanakiuka katiba yanatosha, hata kuiminya demokrasia inatosha kua sababu. Mimi nimetoa huo mfano mmoja tu wa fedha lakini ipo mingi.
Na yote anayoyafanya ni kwa faida yetu sote ntakushangaa sana kulalamika kanakwamba hayo maendeleo yanafanyika Kenya au Uganda.
Ikijengwa barabara Tanga hata mimi huku nitafaidika nayo kwa kua yatakuja matunda kutoka Tanga nitapata kazi ya ukuli Kariakoo.

Ukijenga uwanja wa ndege Chato, huku chanjo hakuna hospitali inakuaje?
Ukijenga fly over daraja la Selander huku antidote kwa atakayegongwa na nyoka ni laki saba na nusu inakuaje?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom