Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kipindi hiki cha awamu ya tano kimepata misukosuko mingi sana hasa kwa watetezi wa rais, Mhe rais anafanya makosa ambayo hualazimu vijana hasa wengi wakiwa wa chama chake kujitoa akili ili tu waweze kumtetea, imefika maana wanaonekana kama watu wasio na akili nzuri kwa vitendo vyao vya kumtetea rais.

Rais ametukana Kagera watetezi wake wakamtetea, mara hakuna njaa wakamtetea, ni juzi tu amevunja katiba ya nchi watetezi wake wakatetea kitendo kwa kusema rais yupo sawa, leo ameteua mbunge kuwa balozi ili zile nafasi 5 za kikatiba ziwepo watetezi wake humu mitandao na huko vijiweni wametetea kitendo hicho.

Kwani Mhe rais ameamua kucheza na akili za watu hawa kwanini anawadhalilisha watu tena wengine wakiwa wasomi, Mhe rais anachofanya ni udhalilishaji.
 
Urais ni taasisi ambayo inafanya kazi zake kwa pamoja wala sio mtu mmoja, Mhe rais amekuwa akifanya makosa mbalimbali katika teuzi zake nyingi hii inadhihirisha kuwa kwa sasa ameufanya urais kama wa mtu mmoja bila kushirikisha taasisi nzima, aibu hii inayompata rais wetu isingelikuwa inampata kama angelikuwa anawashirikisha watu wengine wanaofanya kazi chini ya taasisi ya urais.

Rais anafanya maamuzi ya peke yake ambayo humletea matatizo hapo baadae, fedheha hizi zingeliweza kuepukika endapo rais angelikuwa anawashirikisha wengine katika maamuzi yake, walio karibu na rais wamshauri rais afanye kazi kitaasisi kuliko hivi sasa kumuepusha na aibu ikiwemo hii ya kuvunja katiba ya nchi aliyoapa kuilinda.
 
Wacha kumpigia mbuzi gitaa la solo
Ukitegemea apige miluzi kwa furaha wakati yake ni kula majani na kutengeneza karanga
 
Utamjuaje mchezaj timu pinzani kama mzr au la wakati humpi namba ya kucheza? Jiulze kwa nn kazuia miktano kisiasa? Kwa nn anapga vita vyombo habar na magazeti?

Magu sio mwanasiasa Bali watu walichagua chama tu na sio kuvutiwa na siasa yake, subr ifke muda wa siasa ndo utaona kama wapinzani wamepoteza mvuto au Magu ndo kapoteza!
 
Sina Uhakika na Anakoipeleka Tanzania ila Anapojipeleka Yeye mwenyewe Binafsi ni kubaya.
 
Huu ndio ukweli wa mambo kila kada wa CCM na hata mashabiki wa CCM ambao wametembelea hapa USA hivi karibuni wanatuambia jinsi wanavyojutia kuona nchi inaendeshwa kibabe na kinyume na taratibu, wengine ni watu wamuhimu ambao walikuwa wamekutana na baadhi yetu watanzania tunaosoma hapa Illinois mimi nilikuwa nawasilkiliza kwa makini huku nikisema hakika Mungu ni muweza maana walikuwa wanatuambia hakuna haja ya kubaki USA nchi imebadilika muda simrefu tutaanza kunywa maziwa na asali ila kuanzia July 2016 hawana hamu kabisa

Juzi juzi ndio kilitokea kituko mke wa waziri mmoja amekuja hapa USA tukakutana naye pale Columbus Ohio anatuambia mme wake hana hamu ya kuendelea kuwa waziri eti amechoka na uendeshwaji wa nchi

ccm wanajutia sana hata kama wanajibaraguza kubisha kinafiki hawana hamu
 
Sawa, tumejua upo usa.....ila Trump anaapishwa leo jiandae kufungasha virago.
 
Kwa nini waje kusemea Marekani?,Waache unafiki wao.
Kama wanaona mambo hayaendi sawa na Katiba ya Chama inabidi waitishe vikao na kuelezana Ukweli na kusahihishana.
Kusemea pembeni ni Majungu.
 
CCMs have nailed their mouths shut, if they dare say a word, they will be sacked up.
 
Mwigulu Nchemba, we ni kijana mwenzetu hivi hizi kamata kamata za watani wako kisiasa unazionaje. Vijana km nyinyi mnapopata nafasi za kuingia Baraza la mawaziri ni ushindi kwetu Vijana. Tegemeo letu kwa nyie vijana wenzetu ambao Mkuu amewaona lazima mlete changes..kuna haja gani wa kukamata kamata wapinzani/ watani au vyama mbadala wanapofanya mikutano. Waache nao wafanye mikutano. Mwigulu wewe bado unafuture kubwa ya kisiasa..!!
Ivi Braza unadhani kukamata wapinzani ndo inasaidia Ccm ipendwe. Ukikamata wapinzani unasababisha wanapata sympathy. Na hiyo ndo ilichangia lema kuwa mwanasiasa maarufu na strong.

Polisi imemjenga lema.

Kamata kamata inawajenga wanasiasa wa upinzani na kuwapa kiki sana. Kama kijana acha hayo mambo ..wakemee watu wako wa chini. Kama act wanafanya mikutano waache wafanye hata km wanasema kuna njaa what's problem...chadema kama wanafanya kampeni kipind hiki waachiwe tu.

Tatizo ccm mnatumika kuwajenga wapinzani kwa kutumia jeshi la polisi bila kujua. Wapinzani waachwe wafanye siasa zao. Waache washauri , wakosoe n.k. !! Unaweza dhani kuwakamata kamata ndo kuvunja upinzani unakosea mzee.
We kijana mwenzetu tunajivunia wewe. Chuki za kisiasa hazifai.
Nikupe mfano 1 mwigulu, unakumbuka sakata la Shehe Ponda. Mlipokuwa mnatumia magari na helikopta kumpeleka mahakami.mlivuta attention Nchi nzima na ponda akawa maarufu na muhimu..but leo baada ya kuanza kutumia gari 1 tu tena bila hata escort Ponda hasikiki tena.
Kaka kamata kamata wakina zito, lema, mara mbowe , lowasa..mnatengeneza uhasama tu. Na advantage wanapata hao mnaowakamata.
2025 ntaakuliza tena swali hili tena.

Mnawapa kiki wapinzani. Sympathy vote za bure.
 
mwigulu kavimbiwa at the age of 43 hatari sana akiz3ka atatuua wote,afu ndo unautaka urais!over my dead body
 
Sheria za inchi zifuate kama kuna mtu yeyote bila kujali rangi yake kabila wala chama ni lazima akamatwe,
 
Moja ya vitu vinavyonisikitisha ni ukweli kwamba Mwigulu ndiye waziri wa mambo ya ndani.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…