Njia rahisi ya kuua upinzani, chapa kazi, waletee maendeleo wananchi, wapende raia wako wote, usiwabague, waache wapinzani waongee kama hawaletii uvunjivu wa amani, acha kusikiliza kelele zao, wafutie kesi zao zote zilizo mahakamani za kisiasa, usiwaseme vibaya hata kama wanakusema, jitike kutatua kero za wananchi wako. Ukifanya hivi baada ya miaka miwili wapinzani wote watakuwa wamekwisha na kurudi wenyewe bila hata kusema wananunuliwa na watakaobaki huko watakuheshimu sana. Kuwa na huyu moyo unahitaji msaada kutoka wa Mungu. Biblia inasema "Upendo huvumilia, hufadhili, hauhusudu, haujivuni, haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, hauoni uchungu, hauhesabu mabaya, haufurahii udhalimu, hufurahi pamoja na kweli, huvumilia yote, hustahimili yote (1Wakoritho 13:4-8)"