Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Bado muda wa kuhoji mwelekeo mzima wa taifa mbona huku wabunge tumewapa muda cha kwanza nidhamu ndani ya kazi.
 

Tatizo na wewe hutaki kuona wala kuelewa. Kwani kushughulika na watumishi hewa ni nini? Ama kupunguza matumizi yasiyo na tija (mfano; safari, posho, matamasha, n.k..) wewe unaona ni kitu gani kwani?
Msilete hoja/mada za kishabiki humu halafu mkijibiwa kishabiki muone wanaowajibu kuwa ni punguani.
Maendeleo gani unayotaka kuyafikia bila kuchukua hatua za udhibiti, kurekebisha maadili na uwajibikaji?
Wewe mwenyewe ukiulizwa dira yako ni ipi, hata majibu huna halafu unataka serikali ije na dira?!!! Toa boriti jichoni mwako ndipo uone kibanzi kwa mwenzako.
Nakushauri ongeza juhudi kufanya kazi, lipa kodi shauri na familia yako yote ifanye hayo, jirani zako, ukoo wako nao pia kisha rudi hapa kuuliza tena hayo maswali yako.
 
Siasa za vyama tumeacha 2015 Wewe mpu..mbavu. hapa tunajadili mwelekeo wa taifa letu. Hayo mawazo yako ya mgando peleka chumbani kwako
We mbona hujadili mwelekeo wa chadema? Mna Sera ipi kwa sasa, je ya sukari, au kupambana na ufisadi au ipi hasa??
 
CCM wanapenda sana watu wanaofikiri kama wewe Hongera
 
We ndio hujui unakokwenda sisi tunaona anatupeleka pazuri sana asante mzee magufuri mafisadi wanaanza kulia hawaelewi pa kushika
 
Mbona Enzi za jakaya mlikuwa hamuongei mlikuwa mnajua mnakoenda kwan... Achen unafiki muachen rais afanye yake
 
Hivi Dr. Bana huwa sio member hapa?
Maana wakati wa mzee Mkapa alijitahidi kwenda naye sawa na alivyokuja JK na 'sera' zikabadilika naye wakabadilika naye. Sijamsikia akitoa mwelekeo wa redet siku za karibuni wala kutoa comments za awamu ya tano!
 
Anatupeleka kwenye nchi ya asali na maziwa "bila sukari"
[emoji87][emoji87][emoji87][emoji87][emoji87]
 
Swali ni lamsingi kwelikweli mdau anataka kufahamu cha ajabu Sasa wachangiaji mnaleta ushabiki na kutupiana vijembe. Hakuna anayepinga kwamba raisi hana nia njema ishu ni kwamba strategies (mbinu) za kutimiza hizo nia njema
 

Sasa madawati yanapoongezwa ili watu wapate elimu we huoni kwamba hiyo ndiyo njia mojawapo ya kutoamka asbh na kwenda kwenye viwanda? Lakini unafikiri uwekezaji wote huo unafanyika kwa gharama zipi? Kama una Taifa la watu mafisadi, wavivu, wakwepa kodi, wazembe, utawezaje kamilisha mambo yote hayo??
Tusing'ang'anie kwenda mbele wakati hatusafishi na kurekebisha mambo ya msingi kwa ajili ya maendeleo endelevu.
Hicho ni kichekesho!
 
Chief Bahati mbaya sana chadema siyo reference point yangu.Chadema ni reference point ya ccm,wanaccm na watu wenye brain nyingi kama wewe.ila kwangu Mimi mtu mzima kujilinganisha na mtoto naona kama ni aibu kubwa vile
 
Hatujui kwamba ataanza kuboresha kwanza umeme ndo afwate viwanda..

Au aanze viwanda kwanza ndo afwate umeme...
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] hii ndo Bongoland
juzi waziri mkuu wake kasema kuna makampuni 52 yanakuja kuwekeza kwrnye Umeme, jpm anasema serikali haitaki tena makampuni yatuuzie Umeme, hawajipanda hawa
 
Ni aibu sana mtu kutoa swali kama hili la msingi na likajibiwa na baadhi ya watu kimzaha au kutoa vijibu vya kipuuz au visivyo na mashiko,hoja hujibiwa kwa hoja,kama huna hoja kaa pemben,swali lako ni la muhimu kwa mtu anayeitakia nchi hii mema,na siyo kupelekwa pelekwa kama Kondoo.Hoja yako haina tofauti na hoja niliyomuambia rafiki yangu mmoja kuwa "NCHI YETU INA TAKRIBANI MIAKA 55 HAINA DIRA YA MAENDELEO ILIYOTEKELEZEKA",akabisha akasema Dira ipo,nikamuambia Dira ipo kwenye MAKABRASHA TU.
 
juzi waziri mkuu wake kasema kuna makampuni 52 yanakuja kuwekeza kwrnye Umeme, jpm anasema serikali haitaki tena makampuni yatuuzie Umeme, hawajipanda hawa
Wanasafiri vyombo tofauti
 
Hivi ni sehemu gani, jf, au mitandao mingine naweza pata hoja na mada zinazojibiwa Wa hoja. Maana inaonekana kama huwa kuna watu wanatumwa kujaribu kila mjadala sijuini kwa faida ya nani.

Nitarudi bdae
Mkuu mi naamin hoja hujibiwa kwa hoja,inashangaza mtu anapojibu kama yupo FB,hii ni hatari sana
 
Mkuu umenena
 
Pole!endelea kulala ukiamka utakuta uchaguzi wa 2020 umekwisha.
 
Mkuu mi naamin hoja hujibiwa kwa hoja,inashangaza mtu anapojibu kama yupo FB,hii ni hatari sana
Mkuu kauliza nani anayejua Magufuli anatupeleka wapi,kwa hiyo tegemea majibu kama hayo kwa sababu kuna watu wanajua anakotupeleka na wengine hawajui.
 
Hivi wewe mtu anaomba kura kwa wananchi kwa mtindo wa kubinuka binuka ulitegemea angeweza kuwa na dira ya kuongoza nchi basi unandoto za alinacha
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…