Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Ukiachana na usalama Dodoma kuwa makao makuu ya nchi Ina manufaa makubwa ikiwa pamoja na sehemu nyingi ufikiwa kwa urahisi hasa swala la kutatua matatizo
Mkuu, hizo habari za kutatua matatizo inatakiwa kila wilaya na kata kuwe na vituo vya kutatua matatizo, na kila jimbo liwe na ofisi ya mbunge ambayo ina access kila kitu mtandaoni.

Tungerahisisha sana zoezi zima na kuondoa haja ya watu kusafiri kwenda Dodoma.

Hilo moja.

Pili, katika nchi ambayo watu wenye biashara, figisu, petitions etc, wengi wapo Dar, mji wenye watu zaidi ya 10% wa nchi nzima na influentials walio zaidi ya 50% ya nchi, unaweza kuondoa mji mkuu Dar kupeleka Dodoma, ili uwarahisishie watu kupata huduma za mji mkuu, halafu kinachotokea ni safari za watu wa Dar kwenda Dodoma zikawa ndiyo zinatawala. Hapo unachofanya ni kuondoa huduma Dar na kuwafanya watu wa Dar waende Dodoma kwa kiasi kikubwa, ukifikiri unawasaidia watu wa mikoani wafike Dodoma kwa urahisi.

Hesabu rahisi tu zinaonesha mji wenye watu wengi, viwanda vingi, biashara nyingi etc ndiyo unafaa kuwa mji mkuu.Watu wanamaliza kila kitu hapo.Unatoka Wizarani unaenda bandarini unaenda viwandani umemaliza shughuli, unarudi ulikotoka.

Leo mtu akitaka kufanya hivyo itabidi asimame Dododma halafu aende Dar pia.

Hata kama anatoka Rufiji mzunguko unaongezeka badala ya kupungua.

Dar is a natural hub and harbour, haiepukiki.
 

Hoja ya kitu kuwa moot achana nayo. Kila kitu ni moot at some point. Appropriateness ya decision yoyote inapimwa kwa kuangalia facts na circumstances za wakati ule decision ilipokuwa inafanywa. Ukipata muda, angalia, kwa mfano, jinsi ambavyo sababu za Marekani kuhamisha mji mkuu wake kutoka Philadelphia kwenda Washington, DC zinavyoweza kuonekana za ajabu kwa mazingira ya sasa, lakini wakati ule zilionekana za msingi sana.

Tanzania sio nchi ya kwanza (na pengine haitakuwa nchi ya mwisho) kuhamisha mji mkuu. Mifano mingine ya haraka haraka ni Marekani na Nigeria!
 
Mkuu sasa unafananisha Marekani nchi iliyofaidika na slave trade, na Nigeria nchi iliyofaidika na oil money, na Tanzania nchi hohehahe?

Wenzetu hawa waliweza ku afford hii luxury.

Nilikuwa naongea na Mzee mmoja alikuwa Mkurugenzi wa CDA. Aliniambia Wa Nigeria walivyokuwa wanaanza kuhamisha mji mkuu kutoka Lagos kwenda Abuja walikuja Tanzania kugezea makabrasha, kuona mipango inafanywaje.

Tanzania tukawapa material yote.

Wakaenda wao wakahamisha mji, wakamaliza kikwelikweli.

Sisi mpaka leo tunachechemea, na ndio tuliowafundisha.

Sasa unataka kufananisha Tanzania na US na Nigeria?
 

Nchi zilizofanya hivyo ziko nyingi (zikiwemo masikini na tajiri); Marekani na Nigeria ni fraction ndogo ya hizo nchi. As a matter of fact, nchi zingine zimefanya hivyo zaidi ya mara moja.

Vitu vingine vinakwenda kwa political will zaidi kuliko kitu kingine. Hilo halikuweza kufanyika kwa tawala nne za Tanzania, kwa sababu hakukuwa na political will ya kutosha. Akatokea mtawala aliyekuwa na political will ya kutosha kufanya hivyo, akalifanya ndani ya nusu muhula!
 
Huwezi kuhamisha mji mkuu kwa political will tu.

Panatakiwa pawepo na economic means.

Political will haijengi majengo.

Na tunapenda kujidanganya sana.

Ndiyo maana mpaka leo mji mkuu Dodoma, lakini rais wa Botswana anapokelewa Dar.
 
Hivi uliona Ile clip anayosema kwamba watu wa mwanza wasimchukie mama sababu yeye hajamuua Magu ni maneno tu ya watu????

Kama umeona basi huo ujinga ndio umeenda nae maana hakuna aliyesema mama ndio amemuua Magu na Mwanza hakuna hiyo insinuation zaidi ya MATAGA kubwatuka mitandaoni.

Sasa aliongea vile ingali mama yupo kwenye maandalizi ya ziara ya kikazi Kanda ya ziwa unajikuta unajiuliza huyu RC alikuwa anamaanisha nini kuongea hayo wakati huu wa ziara ya mama????

Kumbuka huyu ni kijana wa Magu lazima kuna vimaneno ameongea mama sio mwehu kumtimua unceremoniously, huyu ni kijana wa Magu na ni wale ambao hawaamini kwenye kuongozwa na mama.

Wacha awe jobless na hii ni message kwa wapumbavu wengine, Magu is no more na hatarudi kwani kuna shida gani wakakubali matokeo ilinwaisho maisha yaendelee? Ujinga wao unawaponza.
 
MATAGA akili zenu mnazijua nyinyi wenyewe. Unauliza Rais wetu mpendwa, Mama Samia Hassan anatupeleka wapi? Kwani dikteta Meko ametupeleka wapi hapa tulipo sasa? Au wewe labda husihi hapa nchini?

Mateso yote tunayopitia yamesababishwa na dikteta uchwara halafu leo hii unakuja kuuliza maswali yako hayo ya kiqumer kwa manufaa ya nani? Umetumwa au umerogwa na aliyekuroga kafa? Nadhani mlozi wako kafa vinginevyo angelikwishakuonea huruma na kukutoa jalalani.
 
Hahahaha. Sasa ni zamu ya SSH baada ya mwendazake[emoji38][emoji38][emoji28][emoji28]
 
Huwezi kuhamisha mji mkuu kwa political will tu.

Panatakiwa pawepo na economic means.

Political will haijengi majengo.

Na tunapenda kujidanganya sana.

Ndiyo maana mpaka leo mji mkuu Dodoma, lakini rais wa Botswana anapokelewa Dar.

Economic means bila political will ni bure pia!

Economic means za capital development ambayo imefanyika kwa muda mfupi zilitoka wapi kama wakati wa tawala zingine hazikuwepo?

Kazi kubwa imeshafanyika. Kilichobaki ni vitu ambavyo haviwezi kuzuia Serikali kufanya shughuli zake wakati ikiendelea kuvikamilisha.
 
Nakwambia hivi, kuhamishia mji mkuu Dodoma hakukuwa na utility.Na mpaka leo hakuna tija.

It was a white elephant political project.

Ndiyo maana mpaka leo watu wanaenda Dodoma, wanarudi Dar.
 
Nakwambia hivi, kuhamishia mji mkuu Dodoma hakukuwa na utility.Na mpaka leo hakuna tija.

It was a white elephant political project.

Ndiyo maana mpaka leo watu wanaenda Dodoma, wanarudi Dar.

Nakuelewa, lakini shida ni kwamba you’re evaluating an old decision kwa kutumia facts na circumstances za leo badala ya zile za wakati ule ilipofanyika!

Hata uamuzi wa kufanya slave trade, ukiupima kwa kutumia facts na circumstances za leo, haukuwa na tija!
 
Wewe mganda acha kabisa kuingilia mambo ya Tanzania jua kuwa Mama anatupeleka mahali safi na salama na watanzania wote tuna imani kubwa tuu na matumaini lukuki toka kwake! Tafakari na waulize waganda wenzio Mu7 anawapeleka wapi!
 
Hapana,

Habari za kufanya maamuzi kwa kuendekeza siasa badala ya kuangalia uchumi hazikuwa sawa miaka ile na hazipo sawa leo.

Hazikuwa sawa miaka ile kwa sababu hazikuwa sustainable.Zingekuwa sustainable Dodoma lingekuwa jiji miaka mingi sana.

Unachofanya hapo ni sawa na unasema nawalaumu waliopanda chelewa wakitegemea mnazi utaota, kwa sababu nimejua matokeo leo.

Wakati siku zote chelewa hazioteshi mnazi.

Nazi ndiyo inaotesha mnazi.

This has got nothing to do with timeline and everything to do with economic fundamentals.

The exercise is an unsustainable white elephant political project. Tunaenda nalo kibishibishi tu kwa sababu hatutaki kugeuka nyuma na hatuendi kwa kuangalia tija na statistics.
 
Mama yuko vizuri anawapatia watanzania walichokihitaji na kinacho wafaa
 
Ndani ya nusu muhula akashindwa pia kuwapa maelfu ya watu maji katika mji huo huo aliootesha maghorofa hafifu amabayo ndani ya miongo miwili yatakuwa kama magofu.
 
Sasa naona tanzania inafunguka kiuchumi.
Mama anafanya kazi kubwa sana tena sana.
Mama sasa anatupeleka kwenye uchumi wa kati kwa kila mtanzania kuishi maisha ya kiwango cha kati kwa uhalisia sio nadharia
 
Sasa naona tanzania inafunguka kiuchumi.
Mama anafanya kazi kubwa sana tena sana.
Mama sasa anatupeleka kwenye uchumi wa kati kwa kila mtanzania kuishi maisha ya kiwango cha kati kwa uhalisia sio nadharia
Kivipi fafanua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…