Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Mkuu, hizo habari za kutatua matatizo inatakiwa kila wilaya na kata kuwe na vituo vya kutatua matatizo, na kila jimbo liwe na ofisi ya mbunge ambayo ina access kila kitu mtandaoni.Ukiachana na usalama Dodoma kuwa makao makuu ya nchi Ina manufaa makubwa ikiwa pamoja na sehemu nyingi ufikiwa kwa urahisi hasa swala la kutatua matatizo
Tungerahisisha sana zoezi zima na kuondoa haja ya watu kusafiri kwenda Dodoma.
Hilo moja.
Pili, katika nchi ambayo watu wenye biashara, figisu, petitions etc, wengi wapo Dar, mji wenye watu zaidi ya 10% wa nchi nzima na influentials walio zaidi ya 50% ya nchi, unaweza kuondoa mji mkuu Dar kupeleka Dodoma, ili uwarahisishie watu kupata huduma za mji mkuu, halafu kinachotokea ni safari za watu wa Dar kwenda Dodoma zikawa ndiyo zinatawala. Hapo unachofanya ni kuondoa huduma Dar na kuwafanya watu wa Dar waende Dodoma kwa kiasi kikubwa, ukifikiri unawasaidia watu wa mikoani wafike Dodoma kwa urahisi.
Hesabu rahisi tu zinaonesha mji wenye watu wengi, viwanda vingi, biashara nyingi etc ndiyo unafaa kuwa mji mkuu.Watu wanamaliza kila kitu hapo.Unatoka Wizarani unaenda bandarini unaenda viwandani umemaliza shughuli, unarudi ulikotoka.
Leo mtu akitaka kufanya hivyo itabidi asimame Dododma halafu aende Dar pia.
Hata kama anatoka Rufiji mzunguko unaongezeka badala ya kupungua.
Dar is a natural hub and harbour, haiepukiki.