Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Sasa naona tanzania inafunguka kiuchumi.
Mama anafanya kazi kubwa sana tena sana.
Mama sasa anatupeleka kwenye uchumi wa kati kwa kila mtanzania kuishi maisha ya kiwango cha kati kwa uhalisia sio nadharia
10000% tru
 
Ndani ya nusu muhula akashindwa pia kuwapa maelfu ya watu maji katika mji huo huo aliootesha maghorofa hafifu amabayo ndani ya miongo miwili yatakuwa kama magofu.

Unayo haki ya kuwa na maoni!
 
Tatizo ni kwamba akili yako inafikiria zaidi watu waliopo nje ya makao makuu kwenda makao makuu kuliko viongozi kutoka makao makuu kwenda wa watu aliopo nje ya makao makuu
 
Tatizo ni kwamba akili yako inafikiria zaidi watu waliopo nje ya makao makuu kwenda makao makuu kuliko viongozi kutoka makao makuu kwenda wa watu aliopo nje ya makao makuu
Kati ya watu milioni moja kutoka Dar kwenda Dodoma kumuona kiongozi au kiongozi mmoja kutoka Dodoma kuja Dar kuwaona watu milioni moja kipi ni rahisi na cha gharama nafuu zaidi zaidi?
 
Tuonesheni Tanzania ya viwanda ile kwenye ilani ya 2015..
Na pia watuoneshe hivyo viwanda venyewe maana hadi sasa kuna viwanda (chereheni 3) vingi tu vimechakaa. Viwanda kama mashine za kutotoleshea vifaranga, mashine za kufyatua matofali, misumeno ya kukatia mbao, misumeno ya kukatia nyama, mashine za kusaga, nk walivyotuaminishwa kwamba serikali ya mwenda imejenga tunaomba waje watuoneshe vivipo; wasidhani kila mtanzania ni ndondocha.
 
Kwa kweli Watanzania hawataki maneno matamu bali vitendo vitamu. Naamini umejifunza na ulishuhudia watu walivyomlilia jemedari, hayo machozi hayataenda bura.

Naungana na mtioa mada cheap popularity haitasaidia. Tafuta majembe chapa kazi kwani foundation ulikwishatengenezewa. Wapambe wasikurudishe nyuma tunachotaka tuendelee.
 
Si nasikia kuna TIMU CHATO ambayo inamikakati ya kukwamisha mama na kumkosoa kwa kila afanyacho eti kisa kaanza kueleza ukweli wa yale yaliyo kuwa yanatendeka sirini, naona mmeanza kazi sasa.
Hebu acha uongo wewe kumkwamisha nini na kila kitu sasa hivi kiko wazi. Atakwama akiendekeza mafisadi. Asikumbatie mafisadi kuna wayu wanapenda pesa bila kufanya kazi akae chonjo. Aidha haohao wapambe wake wanakitamani cheo. Mama Samia kaza buti ili ule usemi wanawake tunaweza ueleweke mwaka huu!
 
 
Kama Jpm haikummaliza, mama haitammaliza.wewe utakuwa unatumika na mabeberu
Wewe acha propaganda za kijinga JPM haikumaliza nini? Wakati tunaenjoy matunda yake wengine wanaaambulia kuifungua tu! Akaze buti mama asituangush kwa kweli
 
To the point,

Kweli Sabaya umemtendea haki.

Tusubiri kwa muda gani ili wabadhirifu waliotajwa kwenye ripoti ya CAG na BOT nao wakichukuliwa hatua?

NYONGEZA: Ule uchunguzi wa BOT ulioagiza ufanywe,wa kuanzia Januari mpaka Machi mwaka huu haujakamilika au ni SIRI?
 
Karibuni sana Mtaani Wazee wa Uamsho, Karibu sana Mtaani Habinder Seth, Karibu sana Mtaani Papa Musofe na GENTAMYCINE nafurahi angalau sasa Muziki wa Dansi utarejea na ile tabia ya Wanamuziki Kutunzwa 'Midolari' Ukumbini itarejea.

Ama hakika Muunguja sasa kaamua kutuonyesha kuwa huenda kwa 85% alikuwa hamuungi mkono Mchato ndiyo maana sasa anabadili mambo ya Mchato, ila akiwa Ukumbini au anaongea nasi anajitahidi Kutuaminisha 'Kindumilakuwili' kuwa anafanya na kuyaendeleza ya Mchato.

Hata hivyo kwa hili la ( haya ya ) Muunguja na Mchato Kwetu Sisi wengine ni Funzo ( Fundisho ) tosha kuwa unaweza ukawa na Mtu unayemuamini kumbe Yeye ndiyo akawa 'Snichi' wako Mkuu au hata na Wewe pia pamoja na Kumuamini Kwako, ila ukawa unamnyanyasa au Kumdharau kwa namna moja au nyingine.

Somo Kuu hapa Wanadamu tusiaminiane sana na pia tutambue ya kwamba uliyenae karibu au Yeye aliyekaribu nawe nyote mna nafasi sawa ya Kusalitiana na hata Kumalizana.

Na hapa ndipo GENTAMYCINE ninapoipenda sana Kauli ya ' Kimedani' ya Wayahudi na Mossad yao isemayo TRUST NO BODY EXCEPT YOURSELF na huenda ndiyo ikawa imenisaidia na inaendelea Kunisaidia japo Marafiki na Maadui zangu ( mpaka Ndugu pia ) wote hudhani 85% hadi 100% huwa nakuwa nao pamoja Kifikra, Kimtizamo na Kimaamuzi kumbe Moyoni na Rohoni huwa 'nawachora' tu Kimtindo.
 
Sisi wengine ni Funzo ( Fundisho ) tosha kuwa unaweza ukawa na Mtu unayemuamini kumbe Yeye ndiyo akawa 'Snichi' wako Mkuu
Mfano mzuri sana usiotoka akilini mwangu ni ule wa rais Chiluba na makamu wake Mwanawasa.

Chiluba aliondoa kinga kwa mtangulizi wake Kaunda ili amsulubishe vema huku akiamini kuwa makamu wake Mwanawasa ni mpenzi na muumini mkubwa wa anayoyayafanya.

Muda wake wa kikatiba wa kuongoza ulipoisha akafanya juu chini amwachie nchi Mwanawasa ili aje kuwa ktk mikono salama.

To make the story short, Chiluba alijuta kuzaliwa chini ya uongozi wa Mwanawasa.
 
Karibuni sana Mtaani Wazee wa Uamsho, Karibu sana Mtaani Habinder Seth, Karibu sana Mtaani Papa Musofe na GENTAMYCINE nafurahi angalau sasa Muziki wa Dansi utarejea na ile tabia ya Wanamuziki Kutunzwa 'Midolari' Ukumbini itarejea..
Kiongozi ukiwafunga watu wenye akili ya kuzalisha ajira, hizo ajira utazitoa wapi kwa hawa watanzania wanaozaa sana
 
Karibuni sana Mtaani Wazee wa Uamsho, Karibu sana Mtaani Habinder Seth, Karibu sana Mtaani Papa Musofe na GENTAMYCINE nafurahi angalau sasa Muziki wa Dansi utarejea na ile tabia ya Wanamuziki Kutunzwa 'Midolari' Ukumbini itarejea..
Mtakoma mwaka huu. Msiopenda haki hamieni nchini Somalia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…