Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Subiri hukumu au uiamini Mahakama? Rais ni binaadamu kama wengine tu anaweza kusema neno na ulimi ukateleza(kukosea) alisema kuna magaidi wamefungwa Tanzania je tunamfungwa walau mmoja wa ugaidi katika Nchi hii?
😍
 
Usipindishe maneno. Wala usitake kumsemea, ulimi umetelezaje? Kakuambia? Amewahi kukanusha wapi? Clip zipo, wewe unatetea ujinga
 
Kaka, hata nyumbani kwako huwezi badiri Kila kitu kwa wakati mmoja.
Na hili ndilo kosa alilofanya Magufuli alipoingia madarakani.
Ndani ya miaka mitano alitaka haya,
1. Serikali kuhamia dodoma,
2. Kujenga bwawa na umeme
2. Kununua ndege
3. She
4. Ukuta mererani
5. Daraja kigongo
6 Airport chato
7. Ujenzi wa kivuko na Meri nk nk
HII NI AKILI?
Akasababisha maisha ya watu kuwa magumu afadhari ya wafungwa huko jela.
Maana mfungwa anachojua no kazi na muda wa kulala, hajui mwanamke, kusomesha, na kutunza familia, hajui Kodi ya nyumba Wala ardhi.

Mimi siyo muumini wa ccm islani, lakini no muumini wa viongozi toka Zanzibar, wanaharikia kwenye ccm tu.
MWACHENI MAMA AFANYEKAZI TARATIBU MSIMUINGILIE KWENYE MJUKUMU YAKE

Uliza China ili kufika pale walipo sasa walikufa wangapi kwa ugumu wa maisha…hakuna maendeleo bila kufunga mikanda…maendeleo kwa spidi hii mnayotaka Tanzania itasubiri sana…tulimuhitaji mwamba kwa miaka mingine 20 ili Tanzania itoboe…sio wewe ila watoto na wajukuu zako wangekuwa pazuri…maana tungekuwa na discipline ya uwajibikaji na akili ya kujitegemea…sio taifa la kuomba omba na upigaji…

Mfano rahisi…Kuna watu wameweka kwao vizuri na kusomesha wadogo zao kwa boom la chuo…wali sacrifice anasa wengine wanakula mlo mmoja..anamaliza chuo familia ipo pazuri na nguvu ya uchumi kwa familia imekua…angekufa je kwa stress za kujinyima?!.. kwake ingekuwa uzalendo kwa ajili ya wadogo zake na jamii iliomzunguka..lazima kuwe na starting point na maumivu hayakwepeki…

Sasa taifa zina v8 za kutosha halafu shuleni hakuna vyoo na madawati..wanasema tunasubiria wazungu watupe msaada, sijui hatupo kisiwani kwenye dunia yetu tunawahitaji…sijui tunafundisha watoto wetu nini…
 
Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani.

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari.

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena.

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.

tunapotea mara mbili?​

We jamaa hii ilitakiwa iwe topic/uzi. Aisee nakussuport 100%
KAti ya comment nilizokua nazisubiria ni hizi
Kaka! Glasgow.

Wako huko kutafuta suluhu ya Tabia ya nchi kutugeuka walimwengu.

Hili ni suala la muumba na muumbwaji. Nini tumemkosea, ili aachia majanga kutifikia?
 
PM Majaliwa huu Utawala wa Samia unaenda kukuharibia sifa ya kiuongozi/kisiasa huko mbele ya safari.

Ukweli ni kwamba huna tena uwezo wa kuhoji hata yale yaliyo kinyume na maadili ya kiuongozi yanayofanywa ama yatayofanywa na mawaziri wateule wa Samia hasa wale waliotumbuliwa na JPM na kurejeshwa na Samia.

Brother M gutuka na ikiwezekana resign kwa maana tofauti na hapo unaenda kuchafuka.
 
Aki resign atakula wapi? We unawaona vile tu
 
PM Majaliwa huu Utawala wa Samia unaenda kukuharibia sifa ya kiuongozi/kisiasa huko mbele ya safari.

Ukweli ni kwamba huna tena uwezo wa kuhoji hata yale yaliyo kinyume na maadili ya kiuongozi yanayofanywa ama yatayofanywa na mawaziri wateule wa Samia hasa wale waliotumbuliwa na JPM na kurejeshwa na Samia.

Brother M gutuka na ikiwezekana resign kwa maana tofauti na hapo unaenda kuchafuka.

Umekula bwana mdogo?
 
Back
Top Bottom