Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Aseee umeongea kwa Uchungu sana
 
Yani umekosa pesa ya kula wewe na familia yako inakuja na poroji serikali imeferi acha ujinga fanya kazi
 
Mimi ni from lake zone, nampenda sana mama na wala simchukii marhemu Magufuli.

Pale anapokosea arekebishe, upande wa tozo, vyakula, mafuta, ushuru wa magari n.k. ushuru wa magari limekaliwa kimya sana sana, rekebisha mama ili watanzania wasiwe na kinyongo.


Nakupenda mama, simchukii magufuli
 
Huyu mama ni kama ameokota dodo chini ya mbuyu. Yaani mfano hapo ukiamsha ukimuuliza umepanga kuifanyia nini tanzania, hana jibu.

.
Je umemuuliza Samia na ukakauta hana jibu kama unavyodai? Au unaandika tu kufurahisha wasomaji?

Na haya makubwa mengi anayoyafanya huyaoni? Au umevaa mawani ya mbao?
 
Acha ujinga wako hapa na msingi wako wa mawazo hapa, umeandika utazani umekunywa au kuvuta vitu vibaya, unasema mbolea zimepandishwa Bei, hivi kwa akili yako unafikiri Rais ndio amepandisha Bei ya mbolea? Kwani hujaona juhudi za Rais kukabiliana na suala la mbolea? Hujaona Rais akitoa billion Mia moja hamsini Kama Ruzuku kwenye mbolea na kupelekea kushuka Bei sokoni? Hujaona mbolea ya DAP inapatikana kwa elfu 70 kutoka huko kwa laki 40?

Unasema na kumtupia lawama Rais wetu mpendwa juu ya petrol, kwani Rais ndio alipandisha Bei ya petrol? Kwani Tanzania pekee ndio Bei ilipanda? Kwani sisi ndio tunaozalisha hayo mafuta Hadi umtupie lawama Rais wetu mpendwa? Je hukuona juhudi za Rais wetu kukabiliana na suala Hilo? Hukuona Rais wetu akitoa billion Mia moja Kama Ruzuku katika mafuta ili mafuta yapatikane kwa Bei itakavyokuwa na unafuu? Au umeandika ukiwa bar?

Unasema habari za ajira kwamba Rais hatoi, wewe ni mpotoshaji, kwa hiyo ulitaka mh Rais wetu ndani ya mwaka mmoja atuajiri vijana wote ndani ya mwaka mmoja pekee wakati ilishindikana katika miaka mitano iliyopita? Kwani hujaona ajira kipindi hiki zikitolewa sana? Hujaona ajira za ualimu, Afya,kilimo,Sheria, zikitolewa na serikali hii ya mama Samia? Hujaona secta binafsi ikipewa nafasi ya ukuaji ambayo inasaidia katika utoaji wa ajira? Hujaona uwekezaji ukiongezeka na hivyo kutoa ajira kwa vijana? Au unafikiri serikali peke yake inaweza kutuajiri vijana wote tuliopo mitaani? Hujaona serikali hii ikiweka mazingira mazuri ya kibiashara?

Suala la Tozo, kwani wewe unazani nchi za ulaya zimefika hapo zilipo hapo kimaendeleo kwa kuyapokea toka angani? Unazani hawakujibana na kujinyima kujenga nchi zao, unazani wao hawakupitia tunayopitia sisi? Unazani nchi zao walijengewa na wageni? Unataka Nani akujengee nchi yako? Unataka Nani abebe wajibu wetu? Unataka Nani alipe Kodi na Tozo ili wewe ukae na kutumia kwa Raha zako? Unataka huduma Bora kutoka fedha za Nani? Alizolipa Nani? Unataka maisha mazuri na huduma Bora kwa jasho la Nani?

Unasema habari za demokrasia, hivi demokrasia gani unayoitaka wewe? Au yakutukana ndio kwako demokrasia? Kwani nani umeona amezuiwa kutoa mawazo yake au maoni yake? Mbona umeandika hapa bila kuzuiwa au kukamatwa? Je hiyo siyo demokrasia na Uhuru?

Sitaki Kuendelea kuchosha akili yangu hapa maana umeandika upotoshaji mtupu hapa na uongo uongo tu wakibabaishaji tu hapa
 
Huu uzi umeletwa kwa sababu Rais

1) Ni Mzanzibari
2) Ni Muislam
3) Ni Jinsia Yake
 
Ulichosahau ni kwamba hata wewe kuna mahali umefeli ndio maana upo hapa JF unatafuta wakumlaumu. Kaza kijana hakuna maisha rahisi
 
Ukiweza andika hata kitabu kabisa. Lakini huyu tunaweza kuwa naye hadi mwaka 2030. Upo hapo ndugu? Haya maandamano ya huku mitandaoni hata haiwanyimi usingizi wale waliopata fursa ya vidole vyao kufanikiwa kupenyeza kwenye Buyu la Asali.
 
Ukiweza andika hata kitabu kabisa. Lakini huyu tunaweza kuwa naye hadi mwaka 2030. Upo hapo ndugu? Haya maandamano ya huku mitandaoni hata haiwanyimi usingizi wale waliopata fursa ya vidole vyao kufanikiwa kupenyeza kwenye Buyu la Asali.
Mama Samia bado yupo Sana hapa, Ni samia Hadi 2030 ndio kituo Cha kupumzikia, halafu ndio tutaangalia katiba yetu unasema Nini, kikubwa Ni Kuendelea kumuombea mh Rais wetu mpendwa mama Samia ili mwenyezi Mungu amjalie Afya njema na nguvu za kututumikia watanzania tunaoendelea kumwamini na kuhitaji utumishi wake uliotukuka
 
Mkuu c uhame Nchi tu, kwa nini unajiumiza kwa msongo Wa mawazo

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
Acha ujinga wewe kwani huoni juhudi za mh Rais wetu mpendwa kuijenga Tanzania yetu na kuinua maisha ya watanzania wanyonge? Huoni wakulima kwa Sasa namna wanavyoneemeeka na kufurahia uamuzi wa mh Rais wetu mpendwa kutoa Ruzuku ya mabillioni katika kilimo na kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni? Huoni mama kwa ujasiri na huruma zake kwa watoto wa maskini kuamua kufuta Ada Hadi kidato Cha sita ili wote wapate Elimu bila shida? Huoni namna huduma za Afya zilivyoboreshwa na kusogezwa karibu ya mwananchi? Huoni huduma za umeme zinavyoendelea kupelekwa Hadi vijijini na hivyo kutoa fursa za ajira kwa vijana?

Huoni mama alivyoimarisha diplomasia yetu na hivyo kupelekea kupata wawekezaji na watalii wengi Sana wanaopigana vikumbo katika kuwahi kukata tiketi za kuja kutalii na kuwekeza hapa nchini?
 
Gesi inafanya kazi gani?? Kuna bomba la gesi lilijengwa kwa trillion za pesa kupeleka gesi Dar es salaam. Hiyo gesi itemise kuzalisha umeme. Tumechoka ngonjera za mvua.
Kuna watu wako jangwani na umeme haukatiki.
Hali ya mvua ikoje Tanzania kwa sasa? Je Rais ndo anafanya mvua isinyeshe?
 
Inasikitisha sana, Baadhi ya maeneo karibu wiki nzima hawapati umeme. Maji ndiyo balaa! Wakati huo kiongozi anabadili route kutoka Oman mpaka USA
Acha uongo wako hapa, maji na umeme vipi kila mahali ukiona maji yanasumbua nenda Katoe taarifa kwa viongozi wako wa serikali za mitaa ili wafuatilue na kujuwa tatizo Ni Nini, mama anaendelea kuwasogezea watanzania huduma karibu yao, Ni wajibu wako kutoa Taarifa penye tatizo na siyo kuja kufanya upotoshaji wako huku
 
Sio tu yeye kutokuwa chaguo la wananchi, lakini pia sio chaguo la hiyo nafasi.
Rais Samia Ni kipenzi Cha watanzania na ni chaguo la watanza na hitaji la watanzania Hadi 2030, Tunamhitaji mama Kuendelea kututumikia
 
Magufuli alikuwa mjinga na mshamba, samia ni kwamba hana uwezo wa hiyo nafasi.
 
Kaajiri machawa kibao wanamsifia eti anaupiga mwingi wakati wenye akili zetu tunaona anavyovurunda
 
Kafanye kazi hutafanikiwa ktk uzushi na propaganda zako za uwongo. Wananchi wamekata tamaa? Lini ulifanya mkutano wa hadhara na hao wananchi? Mtu mzima bila aibu unakaa una-fabricate vihoja bila aibu. Ushindwe na ulegee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…