Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

sio uchumi wa tz tu ulioporomoka. nchi nyingi duniani, hata zile zenye uchumi mkubwa kabisa kama vile Uingereza, Ufaransa n.k zibapitia katika kipindi cha mdororo wa uchumi hii in kutokana na athari zilizosababishwa na ugonjwa wa uviko na vita ya urusi na Ukraine. Hapa hauhitaji kuwa profesa kuelewa kuwa, nguvu ya uzalishaji , utoaji huduma , na ununuzi iliathiriwa na vifo Vinci vilivyosababishwa na maradhi ya uviko. Pia Urusi kama mzalishaji Mkuu wa nishati ya gesi na mafuta katika nchi za ulaya ambazo ndizo hasa soko kuu la bidhaa kutoka nchini kwetu , vita yake dhidi ya Ukraine imepelekea nchi hizo kujihami kwa kupunguza uuzaji wa huduma na bidhaa za msingi kwetu na hivyo kupelekea bidhaa hizo kama vile mafuta, utalii, teknolojia kupanda gharama.

SSH Hajadororesha uchumi wa nchi yetu. Uchumi hupanda na kudorora kwa kufuata kanuni zake. Tuache kumbebesha mzigo rais wetu
 
Kwa mambo yanayoendelea hapa nchini kwa sasa, Ni wazi kwamba wananchi hawana tena imani chini ya uongozi wa awamu hii ya sita. Kila unapoenda ni lawama na hali ya kutoridhika na utendaji wa serikali.Mambo haya yamekuwa yakilalamikiwa sana.

1: Uchumi wa Tanzania Umeporomoka.Laiti kama uongozi ungekuwa thabiti hakika uchumi ungekuwa wa kati daraja la juu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Tanzania imeporomoka kutoka nafasi yake ya 8 kati ya nchi 10 zenye uchumi bora Africa mpaka nje ya top 10 na kuzidiwa na vinchi kama Ghana na Angola

2: Laiti kama uongozi ungekuwa imara nidhamu na uwajibikaji kazini ungekuwepo.Leo hii tunashuhudia wananchi wakihoji kuhusu hali ya umeme nchini pasipokuwa na majibu au majibu yenye uwalakini. Lakini pamoja na hayo bado viongozi wamebaki wakiwa maofisini pasipo kuwajibika kwa namna yoyote.

3: Kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa ikiifanya juhudi kubwa kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa na ya kimkakati. Licha ya kwamba tangu awamu ya sita iingie madarakani hakuna mradi wowote wa kimkakati ulioanzishwa bali pia hata ile miradi iliyokuwa ikiendelea imekuwa ikisuasua

4: Serikali ingekuwa makini hakika Umeme usingekuwa wa mgao.Tangu Rais S.S.H aingie madarakani hali ya upatikanaji wa umeme nchini imekuwa mbaya sana.Hali hii imepelekea kurejea kwa mgao wa umeme ambao watanzania wengi walishausahau tangu miaka kadhaa iliyopita.Hali inayopelekea kuwatesa wananchi hususan wale wanaotegemea umeme kujipatia vipato katika shughuli zao za kila siku.

5; Hali ya upatikanaji wa maji imekuwa ya kusuasua.Kwa miezi kadhaa hususan katika jiji la Dar es salaam pamekuwa na mgao wa maji.Hali iliyopelekea kukosekana kwa maji kwa muda mrefu katika maeneo mengi.Hali ambayo hakuwahi kushuhudiwa hapo awali.

6: Tozo zisizokuwa na tija na zilizoua uchumi wa wengi.Serikali ya awamu ya sita imedhulumu na kunyang'anya kwa nguvu fedha za wananchi kwa kigezo cha tozo katika miamala ya simu.Mama mjane anapomtumia mgonjwa wake hospitali kwa ajili ya matibabu anakatwa fedha ambayo kimsingi haikuwa ya biashara. Kwa mujibu wa report kutoka Vodacom hivi karibuni miamala ya simu imepungua kwa asilimia zaidi ya 30!.Hili si jambo la kupuuza hata kidogo kwa uchumi wa nchi.Ni sawa na kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuhamishia Kulia.

7: Kupanda kwa bei ya Mbolea.Mara tu baada ya awamu ya sita kuingia madarakani bei ya mbolea ilipanda karibu mara mbili ya bei ya awali.Hii ni imepelekea uchumi wa watanzania wengi ambao ni masikini na wanategemea kilimo kudhoofika.

8; Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia.

9; Kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol.

10; Kupanda kwa bei ya bidhaa za ujenzi kama cement,Nondo n.k.

11; Teuzi za viongozi wasiokuwa na weledi kwa kigezo cha favour/Undugu/Kujuana (Mf. Riziwani Kikwete,Nape Nauye n.k) Tanzania ina vijana wasomi na wenye upeo mpana wa kifikra. Lakini cha kushangaza teuzi zimekuwa hazina matumaini ta kuipeleka Tanzania kule tunapotarajia.

12: Ukosefu wa uzalendo na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma.Siku si nyingi tumeshuhudia kiongozi mkuu wa serikali akiwaasa watumishi wake wale kwa urefu wa kamba zao.Hii inaashiria kwamba hata kiongozi mkuu anashiriki katika ulaji huo.Hali hii ni hatari kwa rasilimali za nchi.

13; Wananchi hususan wa hali ya chini kukosa nafasi katika nchi yao.Siku si nyingi tumeshuhudia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakinyanyaswa kwa kuhamishiwa katika maeneo yasiyokuwa tija kwao.Vuta nikuvute hii imepelekea hali ya unyonge na sintofahamu miongoni mwao na kupelekea kuongezeka kwa umasikini miongoni mwa watanzania

14; Mikopo isiyokuwa na tija kwa taifa.Tangu Tanzania ipate uhuru viongozi wake wote walisisitiza kufanya mambo yetu kwa fedha zetu wenyewe bila kutegemea wahisani. Tanzania imebarikiwa rasilimali za kila aina.Mito,Maziwa,Bahari,Madini kama Tanzanite,Mbuga za wanyama,Gesi n.k Inashangaza Sana kuona kiongozi badala ya kusisitiza au kubuni namna ya kuzitumia rasilimali hizi ziweze kuwa na tija kwa watanzania,Badala yake tumekuwa tukijivunia mikopo!

15 ; Kuongezeka kwa gharama za uunganishaji umeme kutoka 27,000 iliyokuwepo mpaka zaidi ya 300,000 ya hivi sasa.Hali hii imepunguza mno kasi ya usambaaji wa umeme

16 ; Muingiliano baina ya mihimili kwa kigezo cha uchama.Inasikitisha kuona kiongozi wa mhimili mmoja anakosa uwezo wa kuikosoa na kuurekebisha mhimili mwingine kwa kuhofia kibarua chake.hili tumelishuhudia baada ya kuona spika wa bunge la JMT kujiuzulu baada ya kuhoji kuhusu mikopo na tozo.

17 ; Safari zisizokuwa na tija wala umuhimu kwa taifa. Tumeshuhudia safari nyingi mno za nje ya nchi,Safari hizi zimekuwa zikiigharimu nchi fedha nyingi.Safari za vikao visivyokuwa na tija kama mkutano wa kujadili athari za gesi ya ukaa sidhani kama ina tija hususan kwa nchi ambazo bado uchumi wake ni mdogo.Ni sawa na mzazi anayemiliki baiskeli kwenda kuhudhuria kikao cha adha wanayopitia wamiliki wa magari kwa tairi zao kukosa ubora.

18 ; Kukosekana uhuru na ukandamizaji wa demokrasia. Tunaweza kusema kwamba pia hata katika awamu zilizopita hili lilikuwepo, Lakini hili la sasa limekuja kwa namna tofauti.Wakati mwingine baba anaweza kumpa mtoto adhabu ya kulima shamba,Mtoto akalia na kulaumu sana,Lakini shamba hilohilo baadaye likaleta chakula mezani wote wakala na kufurahia. Ila tofauti iliyopo sasa,Hakuna chakula kinachokuja mezani!

19 ; Kushughulikia zaidi mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kuliko yale yenye umuhimu na tija kwa watanzania. Imekuwa jambo la kawaida kwa awamu hii kujihusisha zaidi na makongamano,Semina elekezi,Birthday Party pamoja na hafla mbali mbali badala ya kujikita katika kufufua na kubuni miradi ya kimaendeleo itakayosaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa umasikini na kuinua uchumi.Hafla ya machifu na watemi si muhimu kama hafla ya utiaji saini mradi wa uchimbaji na usambazaji wa gesi ya Mtwara!

20 ; Kukosekana ajira. Ubunifu na uibuaji wa miradi mipya si tu umekuwa na tija kiuchumi Bali umekuwa ukiajiri vijana wengi.Kukosekana kwa ubunifu na sera mbovu za serikali zimesababisha kukoseka kwa ajira miongoni mwa vijana wengi

21 ; Kuongezeka matukio ya uhalifu.
Mara tu baada ya awamu ya sita kushika hatamu sote tumeshuhudia jinsi wimbi la uhalifu lilivyoongezeka.Sio tu matukio ya wizi na ujambazi bali mpaka uchomaji wa masoko kama Kariakoo, mchikichini n.k wizi mauaji na utekaji nyara vimeongezeka kwa kasi mno. Hii inaonyesha udhaifu katika usimamizi wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama

22 ; Kuongezeka gharama za simu
Kutokana na kodi za miamala Kuongezeka kampuni za simu zimejikuta zikilazimika kupandisha gharama za muda wa maongezi na huduma zinginezo za simu kama vile huduma za vifurushi ili kuweza kubalance gharama za uendeshaji. Hali hii imesababisha mzigo mzito kwa wananchi hasa ukizingatia mawasiliano ni nyenzo muhimu sana katika shughuli zao za kila siku

23 ; Kutoa vipaumbele kwa mambo ya hovyo na yasiyo na tija kwa taifa hususan kwa wakati huu.Hapakuwa na ulazima kutumia gharama kubwa na uwekezaji katika kutumia kodi za wananchi kiongozi mkuu wa serikali kusafiri na kutumia muda mwingi kutengeneza filamu wakati fedha hiyo haina uhakika wa kurudi.Mfano fedha hiyo ingewekezwa kwenye timu maarufu zinazoshiriki ligi za ulaya ingekuwa na tija na matokeo zaidi na Rais angepata muda kutekeleza majukumu mengine ya kiserikali kuliko kupoteza muda mwingi kusafiri.

Hakika ni mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kinyume na matarajio ya watanzania wengi ambao waliwaamini viongozi wao na kuwaweka madarakani huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuondokewa na maradhi, ujinga na umasikini ambao ndio maadui wakuu wa taifa kama ilivyobainishwa na Mwl Nyerere badala yake watanzania hao ambao wengi ni masikini na wameteseka kwa umasikini kiasi cha kusahau tarehe zao za kuzaliwa huku wakishuhudia wale waliowachagua wakikata keki ikulu!
Unataka uongozi Kama wa jpm ambao vyombo vilifungwa visiripoti lolote baya hata Kama yalikuwepo? Mshukuru mungu keamba everything is open and transparent chini ya Samia. Jpm ndo aliharibu Mambo kibao kutokana na ripoti ya cag. Alitufunga kamba kwamba hakopi kumbe anakopa mikopo yenye riba kubwa Sana na akutupiga fix kuwa tumeingia uchumi wa Kati wakati ni fix tu na bahati mbaya vyombo vyote vya habari alikuwa ameviweka mfuko i
 
Mimi ni from lake zone, nampenda sana mama na wala simchukii marhemu Magufuli.

Pale anapokosea arekebishe, upande wa tozo, vyakula, mafuta, ushuru wa magari n.k. ushuru wa magari limekaliwa kimya sana sana, rekebisha mama ili watanzania wasiwe na kinyongo.


Nakupenda mama, simchukii magufuli
Mi sipendi DHARAU, kwann Hadi sasa anawakumbatia mwigu na marope??

Kati yangu me mwananchi na ye kiongozi mwakilishi wa wanananchi nani boss!!!
 
Mi sipendi DHARAU, kwann Hadi sasa anawakumbatia mwigu na marope??

Kati yangu me mwananchi na ye kiongozi mwakilishi wa wanananchi nani boss!!!

Kiongozi atabaki kuwa mtumwa kwa wananchi wake. Ameukubali uongozi maana yake amekubali kuwatumikia wananchi.


Huenda mama hana washauri wazuri, kama kuna tatizo upande wa Mui na Mar, mama anapaswa aliangalie na ikiwezekana awape wengine hizo nafasi.


Tunahitaji watu (wenye imani, huruma, waaminifu na wachapakazi)
 
Mnaweza kunambia ni kipi cha maana alichokifanya rais Samia hadi sasa ambacho kimegusa raia wa kawaida au kumsaidia??

Nambieni ni kipi kakifanya ambacho kinaweza kuwa sababu ya yeye kusema amefanya kazi ya kusaidia wananchi wake

Nataka kimoja tu ambacho kakifanya ambacho tunaweza kusema kimemgusa mtu wa chini tokea awe Rais
 
Kama kuna watu 1000 hapa Tz ambao sio wanasiasa wala watumishi wa umma wala wafanyabiashara wanaomkubali rais samia basi nipo tayari kutoa gari yangu

Wanaomkubali Samia kwasasa kati ya watu milioni 60 huku Bara basi hata 1000 hawafiki

Nimetafuta raia wa kawaida anayemuunga mkono huyu bibi hayupo hata 1000 hawafiki nchi nzima

Hakubaliki, hapendwi wala hakuna mwenye hamu ya kumsikia huo ndio ukweli, mtaani ni ngumu sana kumkuta mtu anamkumbali rais Samia ukiachana na watumishi wachache wa umma na wanasiasa, na wafanyabiashara baadhi.

Huo ndio ukweli, mwambieni Rais ukweli kuwa hakubaliki kabisa kwa upande wa Tanzania bara.
 
1. Tozo
2. Mgao wa umeme
3. Kenge road
4. Mabwana na Watwana
5. T..EAA kufika T..EAM ndani ya mwezi
6. Mchele kufika sh 4,000 kwa kilo
7. GSM kumleta Mayele
8. Uturuki
9. Chanjo
10. Uhuru wa reiniboo na elijibitii

Au mwananchi ulikuwa unamaanisha Uto? Mbona hayo yako wazi tu, yametugusa sisi uliotutaja!
 
Mnaweza kunambia ni kipi cha maana alichokifanya rais Samia hadi sasa ambacho kimegusa raia wa kawaida au kumsaidia??

Nambieni ni kipi kakifanya ambacho kinaweza kuwa sababu ya yeye kusema amefanya kazi ya kusaidia wananchi wake

Nataka kimoja tu ambacho kakifanya ambacho tunaweza kusema kimemgusa mtu wa chini tokea awe Rais
Lucas mwashambwa unaitwa huku
 
15694.jpg

Kumbe gari yenyewe hiii huyo maza mimi simkubali kama mchuzi usio na nyama.
 
Rais wa kugusa watu wa Chini kwa kupora watu wa juu kwa kulazimisha makosa ya kubambikiana hatotokea tena Tanzania katika miaka ya karibuni

ni bora watu wabaki kuwa maskini kuliko kuwapunguzia umaskini wa kuumiza wengine
 
1. Elimu bure hadi KIDATO CHA SITA

2. UJENZI WA MADARASA

3. KUPANDISHA MADARAJA YA WATUMISHI NA KUONGEZA MISHAHARA YAO.

4. KODI BILA MTUTU WA BUNDUKI NA DHULMA KWA WAFANYABIASHARA.

5. AJIRA SEKTA ZOTE (ELIMU, AFYA, ULINZI NA USALAMA, TAASISI ZOTE NK)

6. BARABARA NYINGI HASA ZINAZOSIMAMIWANA TARURA.

TUNAWEZA KUANDIKA MPAKA KESHO.

NB. CHUKI ZA DINI YAKE USILETE KWENYE MAISHA YA KAWAIDA NA KUTAKA WATU WENGINE WAMCHUKIA. ADUI WAKO SIO ADUI WETU SISI.
 
Back
Top Bottom