Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Tuna hasara sana

Sgr hadi leo holaa

Bwawa lenyewe halikamiliki

Mwendokasi chaliii

Umeme ndo usiseme

Maji ya shida

Ufisadi na upigaji tu

Uchumi mbovu

Vitu vinapanda hovyo tu

Nchi nzima mgao kila mahali tz nzima tuna megawatts 1500 tu tunazidiwa na Msumbiji wenye megawatts 185000 (laki na 85) wakati wapo milioni 30 tu sisi tupo milioni 62

Halafu kuna wajinga wanaimba anaupiga mwingi....Kwa lipi haswa? Hii nchi adui namba moja ni ccm

Sasa hivi umeme unafifia hapa hadi taa haziwaki halaf wanaimba anaupiga mwingi hawa watu ni wazima kweli?

Samia angejiuzulu tu hakuna kitu anaweza!!Tuna hasara sana na tuna bahati mbaya sana!!

Kuna watu hata uwenyekiti wa kijiji wasingeweza lakini mfumo umewabeba hadi wanapewa mamlaka kabisa

Tuna bahati mbaya sana
Tena hasara kubwa sana
 
Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani.

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari.

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena.

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
Jana ametuanzishia safari ya kwenda flame za kiarabu.
 
Tuanpelekwa kuzimu. Unategemea nini wenye macho wanapoongozwa na wenye kutoona uzuri mwanangu?
 
Huyo ndiye Rais wa nchi hiyo cheap popularity inaingiaje?

Mkitaka msitake yeye ndiyo kiongozi mkuu wa nchi na ndiye aliyeachiwa hatamu ya uongozi, mbona aliyepita kuna miradi aliiwacha hivyo hivyo?

Tuwe na subira, kwani yeye hajatoka upinzani ni kiongozi wa CCM ileile na ilani ileile kinachotofautiana ni utendaji tu. Ukizingua unazinguliwa.
Ana point ila kutoonesha heshima kwa Rais kafanya tumdharau na kumpuuza
 
Report ya CAG tokea Aprili ipo mezani lakini hadi leo hakuna kigogo aliyeko rumande kwa wizi wa mabilioni
 
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!

Siyo kila mtu anafaa kuwa kiongozi,Uongozi ni karama ijapokuwa sikuhizi serikali imeanzisha vyuo vya uongozi ili kukabiliana na wimbi la upungufu wa karama kutoka kwa viongozi!

Kwa kifupi Samia Suluhu Hassan hana karama ya Uongozi!,Huo ndiyo ukweli sema ndivyo iliandikwa awe Rais!.

Mimi binafsi sipingi Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ambacho napinga ni yeye kuwa kiongozi wa Taifa kubwa kama Tanzania wakati akiwa hana karama ya Uongozi!

Namna anavyo iongoza nchi ni kana kwamba nchi haina kiongozi!,Majitu yanapiga pesa tu kwa kwenda mbele na hata miradi ya kimkakati hakuna hata mmoja uliokamilika!,kinachofanyika ni blah blah tu kutoka kwa wahuni na walanguzi ambao wanafaidika kwa mapungufu ya uongozi wa Samia!.

Maisha yamekuwa magumu kwa watanzania kila mahari,huko mikoani mabarabara hayapitiki tena kwasababu hakuna mfuatiliaji!.

Nauli za mabasi ziko juu,mahitaji muhimu ya kila siku ya mtanzania yako juu!,Watanzania wanakufa na kuuliwa na Askari hadharani na hakuna kiongozi yeyote anayetolea tamko!.

Ni kama watanganyika wametengwa na nguvu kuamishiwa Zanzibar!

Huu uhuni aukubaliki hata kidogo!.

Nipende kuwaambia Machawa na Samia Suluhu Hassan ya kwamba hii nchi siyo mali yako!,Hii nchi ni mali ya watanzania wote!

Ninashukuru sana Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kuitisha maandamano ya amani!,Hii kitu niilisubiri kwa muda mrefu!

Nitakuwa mstari wa mbele kuandamana na niko tayari kwa lolote!.

Polisi namna watakavyokuja ndivyo nitakavyokabiriana nao!,Sijawahi na sitawahi kumuogopa mtu anayeitwa Polisi!

UMUGHAKA WA BHAGHAKA!
 
mtoa mada unafanya kazi gani? tuanzie hapo, ukinijib ntarudi.
 
Hii nchi ngumu sana.

Tunaishi ishi tu, kila siku tunasikia mafisadi yakifisadi mali za umma na hakuna kinachofanyika, yanatamba yatakavyo mtaani kana kwamba nchi yote iko mifukoni mwao.

cc UMUGHAKA
 
Daah sema Viongozi wakosolewe kwa Lugha zenye staha na wao wanaweza kusoma na kurekebisha makosa yao hizi lugha ngumu kumeza sio kabisa Wasizwa...
 
nakubaliana na mtoa mkurya lakin kuna chawa mmoja anaitwa ChoiceVariable anakuja kutibua
 
Back
Top Bottom