Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Tena hasara kubwa sana
 
Jana ametuanzishia safari ya kwenda flame za kiarabu.
 
Tuanpelekwa kuzimu. Unategemea nini wenye macho wanapoongozwa na wenye kutoona uzuri mwanangu?
 
Ana point ila kutoonesha heshima kwa Rais kafanya tumdharau na kumpuuza
 
Report ya CAG tokea Aprili ipo mezani lakini hadi leo hakuna kigogo aliyeko rumande kwa wizi wa mabilioni
 
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!


Siyo kila mtu anafaa kuwa kiongozi,Uongozi ni karama ijapokuwa sikuhizi serikali imeanzisha vyuo vya uongozi ili kukabiliana na wimbi la upungufu wa karama kutoka kwa viongozi!

Kwa kifupi Samia Suluhu Hassan hana karama ya Uongozi!,Huo ndiyo ukweli sema ndivyo iliandikwa awe Rais!.

Mimi binafsi sipingi Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ambacho napinga ni yeye kuwa kiongozi wa Taifa kubwa kama Tanzania wakati akiwa hana karama ya Uongozi!

Namna anavyo iongoza nchi ni kana kwamba nchi haina kiongozi!,Majitu yanapiga pesa tu kwa kwenda mbele na hata miradi ya kimkakati hakuna hata mmoja uliokamilika!,kinachofanyika ni blah blah tu kutoka kwa wahuni na walanguzi ambao wanafaidika kwa mapungufu ya uongozi wa Samia!.

Maisha yamekuwa magumu kwa watanzania kila mahari,huko mikoani mabarabara hayapitiki tena kwasababu hakuna mfuatiliaji!.

Nauli za mabasi ziko juu,mahitaji muhimu ya kila siku ya mtanzania yako juu!,Watanzania wanakufa na kuuliwa na Askari hadharani na hakuna kiongozi yeyote anayetolea tamko!.

Ni kama watanganyika wametengwa na nguvu kuamishiwa Zanzibar!

Huu uhuni aukubaliki hata kidogo!.

Nipende kuwaambia Machawa na Samia Suluhu Hassan ya kwamba hii nchi siyo mali yako!,Hii nchi ni mali ya watanzania wote!


Ninashukuru sana Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kuitisha maandamano ya amani!,Hii kitu niilisubiri kwa muda mrefu!

Nitakuwa mstari wa mbele kuandamana na niko tayari kwa lolote!.

Polisi namna watakavyokuja ndivyo nitakavyokabiriana nao!,Sijawahi na sitawahi kumuogopa mtu anayeitwa Polisi!

UMUGHAKA WA BHAGHAKA!
 
mtoa mada unafanya kazi gani? tuanzie hapo, ukinijib ntarudi.
 
Hii nchi ngumu sana.

Tunaishi ishi tu, kila siku tunasikia mafisadi yakifisadi mali za umma na hakuna kinachofanyika, yanatamba yatakavyo mtaani kana kwamba nchi yote iko mifukoni mwao.

cc UMUGHAKA
 
Daah sema Viongozi wakosolewe kwa Lugha zenye staha na wao wanaweza kusoma na kurekebisha makosa yao hizi lugha ngumu kumeza sio kabisa Wasizwa...
 
nakubaliana na mtoa mkurya lakin kuna chawa mmoja anaitwa ChoiceVariable anakuja kutibua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…