Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Mnaposema anaupiga mwingi sijui ni kwenye sekta gani maana kila kona hali tete.

Gharama za maisha zipo juu, umeme wa majanga nchi nzima ina mgawo, gharama za vyakula kila kitu juu.
 
Hili nalo wakalitazame.

NCHI HALI TETE KILA MAHALI.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani.

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari.

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena.

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
Tunapotea mara ngapi?
 
Great thinkers

Kwa msaada wa Video hii.(Modes DON'T edit)

1. Gari ni Tanzania
2. Dereva ni samia
3. Abiria ni wapiga kura.
4. Anayechukua video ni Sukuma gang.
5. Waliopo Ng'ambo wakimwongoza Dereva ni Msoga gang(Wahuni) na Baraza la mawaziri.
6. Maji ni lundo la Matatizo Nchini..
 
Nchi ipo ktk mtanziko mkubwa sana.
Kitakachoweza kutunusuru kwa sasa ni kuitisha uchaguzi mkuu tu ili tuchague viongozi wa kutuvusha hapa!
 
Great thinkers

Kwa msaada wa Video hii.(Modes DON'T edit)

1. Gari ni Tanzania
2. Dereva ni samia
3. Abiria ni wapiga kura.
4. Anayechukua video ni Sukuma gang.
5. Waliopo Ng'ambo wakimwongoza Dereva ni Msoga gang(Wahuni) na Baraza la mawaziri.
6. Maji ni lundo la Matatizo Nchini..
View attachment 2910764
Hiyoo imeenda imeendaaa
 
Great thinkers

Kwa msaada wa Video hii.(Modes DON'T edit)

1. Gari ni Tanzania
2. Dereva ni samia
3. Abiria ni wapiga kura.
4. Anayechukua video ni Sukuma gang.
5. Waliopo Ng'ambo wakimwongoza Dereva ni Msoga gang(Wahuni) na Baraza la mawaziri.
6. Maji ni lundo la Matatizo Nchini..
View attachment 2910764
Kwa wanaonifuatilia hapa JF mimi nilikuwa mpiga debe ya saa100 baada ya jiwe kudondoka! Sasa nimejirudi, nimetafakari, na nimeamua kuwa huyu si rais ni bonge la mchongo wa mafisadi wa nje na ndani ya nchi tutakwisha tukimpa mitano tena.
1. Ufisadi kumbe uko kwenye damu. Huyu ni Binti wa Mzee Ruksa ambaye alianzisha ufisadi kupitia mkewe |Siti miaka ile. Na huyu yuko na genge la msoga alilolikataa jiwe ili watufilisi.
Ruksa ndiye aliyetutumbukiza kwenye kiza kinene cha kuuza raslimali za mbuga zetu alipoanzia na Loliondo, Bintiye anamalizia tu.
2. Nyie wazanzibar endeleeni kugugumia chini chini tu maanake huyo mtalii mwanaye ruksa wa kiume amepania kumaliza zanzibar yote. Yule Simai aliyejiuzulu kumbe ni dili la pombe ambalo Hussein alicheza na wabara wenzie na kusababisha biashara ya utalii idorore.
3. Familia ya Mwinyi (ruksa) ni majambazi madalali ya raslimali zetu JMT iondoshwe come 2025 la sivyo----
 
Huyo ndiye Rais wa nchi hiyo cheap popularity inaingiaje?

Mkitaka msitake yeye ndiyo kiongozi mkuu wa nchi na ndiye aliyeachiwa hatamu ya uongozi, mbona aliyepita kuna miradi aliiwacha hivyo hivyo?

Tuwe na subira, kwani yeye hajatoka upinzani ni kiongozi wa CCM ileile na ilani ileile kinachotofautiana ni utendaji tu. Ukizingua unazinguliwa.
Jibu hoja zilizowekwa acha mbwembwe za kutetea chama. Kazi hiyo muachie Makonda
 
Kwa siku nyingine tena tupo gizani baada ya umeme kukatwa. Hakuna ratiba yoyote ya siku ya wiki wala saa. Umeme unakatwa na kurudishwa na Wahusika wakiamua au tuseme kama wapendavyo na bila taarifa. Hakuna tamko lolote kuhusu hali hii kutoka kwa kiongozu wa nchi, na imeishia wateuøe wake kila kuchao wanakuja na matamko mbalimbali kinzani ya lini adha hii itafikia tamati. Kee hii nchi Rais kweli yupo na anafahamu uhalisia wa maisha haya ya mateso matupu kwa Raia wake? Huyu Rais kama kweli yupo kwanini anajificha na haonyeshi kuguswa wala kujali?
 
Back
Top Bottom