Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Huyo brother yawezekana amekumbwa na post traumatic depression ya kumpoteza mwendazake. Ile sudden death imewavuruga baadhi ya ndugu zetu wa praise team. Ilichobaki Tuwaombee
 
Wale tuliokua tunawaita nyumbu naona sasa ndo wako na mama. Maneno yao ya kejeli na ushabiki tu. Kinachonisikitisha hakuna chama cha upinzani serious ila kama kitakuja kuwepo ntakupigia kura za hasiraaaa
Utakuwa umejifunza kitu hapa,kwamba mwendazake hakupingwa kwasababu ya chama chake alipingwa kwasababu ya ubabe wake.
 
Tutegemee mambo mengi toka kwa Rais Samia Suluhu. Mojawapo ni tabia nyingi za aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne Ndugu Jakaya Kikwete.

Safari zitakuwepo nyingi sana na majambazi yatampangia safari nyingi ili yabaki yakiiba pesa za umma. Kuna uwezekano mkubwa sana wa Nchi kusimama.

Lakini faida ni yeye katika kutaka kuwafurahisha watu kwa furaha za muda mfupi huku nchi baadaye ikiingia kwenye majanga

Wauzaji wa madawa ya kulevya na biashara haramu wanaanza kurudi wakiamini sasa watakuwana nafasi ya kuja haribu tena maisha ya watanzania. Mtandao wao unafahamika ulikuwa mkubwa mpaka ndani ya Serikali kuu.

Sijui yeye atakuwa na mtizamo gani katika hilo. Lakini tutegemee maisha yale mazuri ya kipindi cha kikwete katika awamu hii. Ya kila mbuzi kula kutokana na urefu wa kamba yake.

Tofauti na kikwete labda ni kuwa Speeches za huyu mama anaongea kwa utulivu na anakuwa amejipanga. Kikwete hakuwa na mvuto wa kuongea au kusikilizika. Tofauti ya kikwete na magufuli ni kuwa magufuli alikuwa na maneno makali but kikwete maneno yasiyo na maana.

Kama tunapenda speeches nzuri basi tutaendelea kuzipata kila mara. Hizi mama atajitahidi kuendelea kuwa nazo. Na kwa kuwa tulizimiss kila baada ya speech tutampongeza sana kwa kutufariji. Na ni kweli watanzania wanapenda maneno ya faraja. Tuendelee kupata.

Mnaweza kidogo mkachanganyikiwa kwa nlichoandika. But ndani kwenye threads mnaweza pata some points.mengine achana nayo
 
The more things change the more they stay the same
 
Wakati wa Mwendazake vs wakati wa JK ni kipindi gani nchi ilisimama?

Kama hutaki hamia North korea kule hakuna kusafiri
 
Mama piga kazi,sisi wengine tulishasema akiondoka jiwe hata aje mdudu tutamuenzi.

Mama Samia msikilize Jaakaya Kikwete sana kwa ushauri rudisha Demokrasia

Kama ni Unga wacheni tuule kuliko zile njaa za awamu iliyopita
 
Nchi iliimarika kipindi cha JPM nchi iliharibika kipindi cha miaka 10 ya JK.Natamani JPM angemalizia miaka yake 10

Iliimarika kwenye sekta ipi KWA mfano??

Ufisadi mbona ulikuwa pale pale?deni la Taifa mbona limezid Mara dufu,hali ya maisha mbona ulizid kuwa mbaya zaid??

Biashara na uchumi mbona umedorora, mwendazake bora ametanguliaaa
 
Kuna watu kwa kweli wana mashaka sana na mama...
Sijui ni mfumo dume au ni nini.

Kama unayajua majizi na mauza dawa za kulevya kuna sehemu za kuyapeleka acha kulia lia humu.

Tuliwaambia andaeni taasisi imara ambayo ingepatikana kwa katiba imara mkatuona sisi hatufai... Mkaamini katika MTU, tena mmoja.

Sasa endeleeni kulia lia humu. Karash!
 
Sijui yeye atakuwa na mtizamo gani katika hilo. Lakini tutegemee maisha yale mazuri ya kipindi cha kikwete katika awamu hii. Ya kila mbuzi kula kutokana na urefu wa kamba yake.

Kwahiyo wewe watu kuwa na maisha mazuri inakukera nini? Au wewe ulitaka yale mambo ya watu kuishi kama mashetani?
 
Inashangaza Sana,jamaa Wana balaa Sana,

Eti wanamtaman mwendazake arudi zake Tena??hawa wendazim au
Mungu anisamehe...hayati Magufuli amefanya mengi mazuri lakini sikuwahi kufurahia utawala wake kamwe.....sitakuja kuutamani naomba Mungu anisaidie katika maisha yangu yoote yalisalia nisipitie utawala kama ule
 
Ur still a learner
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…