Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Mademu wa Sabaya mnahangaika kweli kweli. Kama vipi kufeni tu hamna faida yoyote
 

Unadhani TISS wana kazi gani?? Hilo swala si la jana wala juzi, toka mwaka jana una uhakika halikiwahi kufuatiliwa??

Hayo mengine mbwembwe tu, kilichomgharimu ni kwenda kupiga porojo kwenye media!! Una makosa lukuki halafu unakwenda kwenye media kuharibu tena kwa kujiamini!! The guy is stupid, angebaki zake Hai ale mtori yasingemkuta hayo!!
 
Ndio maana hajafukuzwa, kasimamishwa kupisha uchunguzi. Muwe mnasoma mnaelewa, na kuhusu ushahidi unataka ushahidi upi zaidi. Yeye mwenyewe Sabaya kajitakia haya alitakiwa asome alama za nyakati, by the way. Uchunguzi ukikamilika uwenda akasafishwa kama hatakuwa na kosa na pengine kurudishwa kwenye nafasi yake. Mungu ibariki Tanzania.
Alitakiwa amtumbue kama ana ushahidi
 
Sidhani kama una akili timamu.
Wewe ungekuwa na akili timamu ungefahamu DPP kuna watu wengi amewasekwa rumande bila dhamana kwa maneno ya kusikia tu bila ushahidi wowote huku familia zao zikisambaratika bila kujua hatma za watu wao

Sponsor wako ametenguliwa tu kutoka ofisini ndio unapiga mayowe yote haya kama mjusi aliyebanwa mkia na mlango.
 
Hivi una akili kweli wewe?
Unathubutu kusema Mh. Rais amekurupuka na hana ushahidi wa kumsimamisha kazi?
Sabaya sio mtumishi wa serikali, ni mteule wa Rais. Hivyo muda na saa yeyote, ana mamlaka ya kutengua uteuzi wake bila hata ushauri wa mtu.
Lakini tukiachana na hayo, Mh. Samia hakuwa anaishi ulaya, ana mjua Sabaya kuliko unavyo dhani.
Na kwa taarifa yako, wakati wa mwenda zake, Mh. Mpango alisha tumwa kumkanya huyo dogo mnae mtetea, Mzee Mkuchika alisha tumwa, na siku chache kabla ya kifo cha Jpm kulikuwa na tume ina mchunguza huyo jambazi wenu kuhusu fujo alizo fanya Arusha.
Siyo hayo tuu aliwahi kuitwa Dodoma huyo jambazi wenu akaelezee pesa anazo nyanganya wafanya biashara.
Hivyo kama hamna vielelezo msiwe mna kurupuka kuweka urojo hapa.
 
Marehemu alikuwa anafuata sheria ? yeye hakufanya tena na kuita binadamu majipu. mkafurahi sebuse mama anatumia demokrasia uchunguzi ufanyike, mkurugenzi wa jiji Dar hakutumbuliwa akafa, OCD Njombe alitumbuliwa akazirai tena wote hadharani bila staha ,huoni mama anafuata misingi ya utumishi wa umma?
 
Ni uchunguzi unafanyika akionekana hana tatizo atapata teuzi wala usiwe na hofu....au huviamini vyombo vya uchunguzi?.
 
Kuna watu wanaamini wengi tunaosema kuhusu Ole Sabaya ni wanachadema. Hapo ndipo wanapokosea sana. Hakuna binadamu anayependa kuona mwenzake ananyanyaswa au kuonewa. Ndipo sasa hili kundi kubwa linalomwandama sabaya lilipoibuka kwa sababu ya kutetea haki ya watanzania wanaonyanyasika na kuonewa.
 
Kwa nini msiweke hiyo video na sisi tuone
 
Unamuongelea Mwendazake ?

Sababu enzi zake ilikuwa inategemea ameamkaje (maneno yake mwenyewe)....

Kiongozi ukituhumiwa ni vema upishe uchunguzi ili tubaini vinginevyo (hili mbona lipo wazi kabisa....)
 
Alisema mtanikumbuka kwa mema! JPM alikuwa hasikulizi kelele za chura! Bila ushahidi usio na chenga na sio wa kubumba wa allegations alichukulia ni majungu!
Sina uhakika kwa mama, maana kina mama saa nyingine wanakuzaga vijambo vidogo vidogo tu! Na wakipata comment mbaya juu ya mtu wanaweza kumfungia vioo bila sbb!
RIP our Hero, rest in eternal peace and power our iconic president hon Dr. JPM😭🙏!
 
Unajua kazi ya Dpp? Unajua kesi ambazo hazina dhamana?
 
Umekula Maharage ya wapi mwenzetu..Wewe unakijua kilicho mezani kwa mkubwa ?!?
 
Hata hueleweki unasema nini Ila ulieleweka unataka kusema na ulichoandika sio ulichotaka kuandika
Zaidi jiulize SSH na Jiwe Nani anachukua uamuzi kwa hisia tu.
Dogo sio angesimamishwa kupisha uchunguzi angefukuzwa na leo angeonekana mahakamani enzi za jiwe

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…