KWA wale waliowahi kusafiri na midege mikubwa hasa Boing wataelewa hiki ninachosema.
Ndege ikifika masafa ya juu na safari ni masafa ya mbali mathalan kutoka JNIA kwenda China, inafika mahali rubani anaseti mitambo na kuacha ndege kujiendea tu. Rubani anaweza kuja nyuma kwa abiria kupiga nao story na hata kulewa Pombe. Ila ni hatari pale ambapo rubani atajisahau ama kulewa asijue ni muda gani anatakiwa kurudi kwenye usukani kushusha ndege chini. Ndege itajiendea tu hadi mafuta yatakapoisha na kudondoka na kuwaka moto na kuua abiria wote. Hiki ndicho kilichotokea Kwa Air Malasia iliyopotea na watu 320 hadi leo!
Tanzania kwa sasa iko kwenye aoto-pilot. Nchi inajiendea tu. Rubani ama kachoka, kachoshwa, kajichosha au makusudi. Ni kama nchi haina kiongozi tena. Hakika tutaanguka na tutakufa wote. Ni suala la muda tu.