Anayepinga maandamano ya 23/09 anaunga utekaji na mauaji ya raia

Anayepinga maandamano ya 23/09 anaunga utekaji na mauaji ya raia

Wewe ni mjinga, uliyekosa ufahamu. Hivi Urais wa Samia una thamani kuliko uhai wa watu wanaorekwa na kuuawa? Rais anaweza kupatikana mwingine. Alikuwa Mwalimu Nyerere, Akaja Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Samia, watakuja na wengine wengi, LAKINI uhai unaokatizwa na mashetani yaliyopo ndani ya Serikalini yake, Samia ana uwezo wa kurudisha japo wa mtu mmoja?

Tuna watanzania wengi ambao wana uwezo wa kuwa marais LAKINI hatuna hata mmoja mwenye uwezo wa kurudisha hata uhai wa sisimizi mmoja, ukishapotezwa.
Nadhani we ndo mpuuzi, hivi kila mtu akitekwa rais aachie office si kila mwaka tutakuwa tunabadili rais? Hivi unajua gharama za kumpata kiongozi we bawacha?
 
Kabla ya maandamano ningeshauri ifanyike dua ya taifa kuwalaani hawa watekaji na washirika wao.

Hayo maandamano hayana athari zozote kwa wasiojulikana.,
Tumeshihudia maandamano kadhaa lakini still NO CHANGE.
Kama kwl mnataka yawakute mazito basi ifanywe dua nzito ALALBADIL.

Nina sasiwasi hayo maandamano ni kukwepa dua ya kulaani wasiojulikana...
Dua haisaidii chochote, ni kupoteza muda tu.
 
Katika nchi hii kuna mambo mengi hayaendi sawa na si hilo la utekaji pekee
Hivyo basi wanaopinga kuunga mkono maelekezo ya kuandamana wanatakiwa waheshimiwe maoni yao hiyo ndiyo Demokrasia siyo kila unaloona linafaa kwako basi kila mtu aunge mkono na ukipingwa unaleta fujo unasahau kwa kitendo hicho unarudia makosa ya watawala ambao wakikosolewa wana kuja juu.
Sheria mama inazungumzia presumption of innocent tumekuwa tukilaumu uvunjifu wa sheria kwamba mtuhumiwa hawezi kuchukuliwa ni mkosaji mpaka Mahakama itakavyo tamka lakini ajabu kundi la watu kwa kujifanya wao ni wana harakati wameanza kutoa hukumu jukumu ambalo siyo Lao.
Labda nigusie kwanini siyo haki kutoa hukumu bila kufanya uchunguzi ni kwamba binadamu tumekuwa tukikosea na kutuhumu watu wasio na hatia kutokana na mihemko kuna watu wasio na hatia wameuwawa kwa kupigiwa yowe kwamba ni wahalifu kumbe kuna mtu mmoja kwa maslahi yake anataka kuchukua udhaifu wa wananchi wanaojiita wenye hasira kali ili kufanikisha malengo yake binafsi.
Nimeangalia orodha ya waliotekwa inaenezwa na kutuaminisha kwamba wametekwa wakati wengi ninawafahamu baadhi wamejiteka kukimbia madeni ya benki na mmoja ametoroka na kuacha maagizo hivyo hali inayozungumzwa siyo kwa kiwango hicho kinachoenezwa.
Hivi karibuni pale Geita wananchi wameeneza kwamba kuna mtu ameiba watoto wakataka kumuua na kabla ya tukio wakachoma moto gari na kuharibu kituo lakini baada ya uchunguzi ikabainika kwamba hakuwa mwizi wa watoto bali ni watoto wake.
Sisi wananchi teacher uchunguzi ufanyike kwasababu hakuna namna tunaweza kukwepa hilo kufanyika ndiyo utaratibu wa sheria uliopo kwa sasa na kama hatutaamini matokeo ya u hunguzi tunaweza kutoa maoni yetu na si kulazimisha. Polisi kutuhumiwa siyo kigezo cha kuacha kufanyika kwa uchunguzi kwasababu kuna tuhuma nyingi dhidi ya Polisi zimewahi kutolewa na uchunguzi ulifanyika na hatua zilichukuliwa kutokana na ukweli kwamba Matukio ya kutekeleza Uhalifu ni kinyume cha majukumu waliyopewa kisheria.
Wananchi wengi hawaungi mkono maandamano siyo kwasababu ni waoga au hawana akili bali wanaangalia mustakabali wa maandamano hayo mwisho wake ni kuumizana wapenda amani wanaamini njia nzuri ni kutafuta njia sahihi ya kupambana na waovu ambao wapo pande zote iwe kwa chama tawala au upinzani.
Tupate watu mahili watakaokuja na mbinu iliyo bora ya kuondoa kundi la wadhalimu kupitia njia isiyo haribu maisha ya watu wasio na hatia kwakuwa haina maana kulaani watu kuuwawa hovyo alafu unahamasisha watu wakauwawe hadharani zaidi ili tu update huruma za kisiasa kwani huruma za watu wa Libya zimetusaidia nini au Palestina nk.
Mwisho wa siku tunauwezo wa kuwaondoa watu wa ovu kwa kutumia utaratibu mzuri tuweke bayana sisi tunaowapinga hawa mafisadi,wadhalimu tutafanya nini ili wananchi watuelewe na watuunge mkono na tusitumie kakikundi ka familia na ndugu zetu au mahasimu wa mpinzani wetu na kuwapa jina la wananchi hiyo ni kujidanganya.
 
Kabla ya maandamano ningeshauri ifanyike dua ya taifa kuwalaani hawa watekaji na washirika wao.

Hayo maandamano hayana athari zozote kwa wasiojulikana.,
Tumeshihudia maandamano kadhaa lakini still NO CHANGE.
Kama kwl mnataka yawakute mazito basi ifanywe dua nzito ALALBADIL.

Nina sasiwasi hayo maandamano ni kukwepa dua ya kulaani wasiojulikana...
Unataka kuniambia hamas, hizbollah na Iran na HOUTH wanapiga ALALBADIL kwa IDF...... We jamaaa emu kuwa serious kidogo eti
 
Unataka kuniambia hamas, hizbollah na Iran na HOUTH wanapiga ALALBADIL kwa IDF...... We jamaaa emu kuwa serious kidogo eti
Kumefanyika maandamano mangapi?
Ikawaje?

Hicho kisomo hakiwezi kukubaliwa na wahusika.
Ndy hapo itakapojulikana kwann hawataki dua ya kulaani wasiojulikana..

Kumlila MUNGU ni zaidi ya maandamano.
 
Dua haisaidii chochote, ni kupoteza muda tu.
Ndy ifanywe sasa halafu tuone kama MUNGU anadhihakiwa.

Maandamano ni sarakasi kuzima dua maalum kuwalaani wale wote wanaohusika na mauaji..
 
  1. Haya ni maandamano kwa minajili ya kutetea haki ya kuishi.
  2. Polisi na vyombo vya dola wametuhumiwa kushiriki utekaji na mauaji ya raia
  3. Serikali imeonesha uzembe mkubwa kulinda maisha ya watanzania
  4. Bunge limegoma kujadili na kuihoji serikali kilio cha wananchi cha utekaji na mauaji ya raia
  5. CHADEMA wameibeba agenda hii kwa niaba ya Watanzaia, wameileta kwetu Watanzania bila kujali itikadi, imani na ukabila.
Je, Wananchi sisi tunakubali haya yaendelee?

Pia soma: Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea

Yeyote anayepinga ama kukwepa haya maandamano, tunamuelewa kwamba anaunga mkono utekaji na mauaji dhidi ya raia.

Samia Must Go
Ninakubaliana na maudhui ya mada moja kwa moja.

Huenda hao "...wanaopinga au kukwepa haya maandamano" ni kwa sababu kuu moja tu, nayo ikiwa ni hiyo 'signature' ya
Samia Must Go
 
Kabla ya maandamano ningeshauri ifanyike dua ya taifa kuwalaani hawa watekaji na washirika wao.

Hayo maandamano hayana athari zozote kwa wasiojulikana.,
Tumeshihudia maandamano kadhaa lakini still NO CHANGE.
Kama kwl mnataka yawakute mazito basi ifanywe dua nzito ALALBADIL.

Nina wasiwasi hayo maandamano ni kukwepa dua ya kulaani wasiojulikana...
Wewe unazo sababu zako nyingine za kuwapa ahueni hao hao watekaji na wauaji. Kila mtu anaibuka na visababu vyake vya uongo na kweli, ali mradi mambo yaendelee kama yalivyo.
 
Maandamano ya kumlazimisha Samia aachie office ni uhaini, polisi Kwa namna yoyote wasiruhusu hawa wahuni kuingia road, Samia yupo Kwa mujibu wa katiba na ataachia office Kwa mujibu wa katiba na si Kwa maandamano.

..Samia ashughulikie watekaji, au aondoke madarakani kikatiba.

..Amiri Jeshi Mkuu asiteweza kuongoza na kudhibiti vyombo vyake hafai kuwepo madarakani.
 
Siungi mkono utekaji/mauaji, na wala siungi mkono maandamano!
Mtazamo wako wa kutuweka kwenye makundi mawili peke yake ni finyu. Usitufanye sote kuwa tunafikiria kama wewe, wengine tunaweza kufikiria nje ya box 📦
Haya tusaidie kufikiri nje ya box...
 
Hayo maandamano ni haramu. Msingeanza na hiyo kauli ya kihaini ya SAMIA MUST GO mngeweza kueleweka. Hata kwenye huu uzi umeandika hiyo kauli kudhihirisha nia yenu ovu. Hawa polisi mnaowatukana kwa kuwaita Policcm mtakutana hiyo tarehe 23.
 
Ninakubaliana na maudhui ya mada moja kwa moja.

Huenda hao "...wanaopinga au kukwepa haya maandamano" ni kwa sababu kuu moja tu, nayo ikiwa ni hiyo 'signature' ya
Hiyo slogan inassidia kuamsha concern.

Samia anafahamu kila kitu. Hajaonesha kuguswa na hizi issue za utekaji na mauaji ya raia.

Dhamana ya uongozi imemshibda. Anatumia vyombo vya usalama kuwajengea raia hofu, woga na misukosuko.

Arudi uraiani ili tumpe Mtanzania mwingine nafasi ya uongozi ws Taifa hili
 
Hayatafanyika
Hayataleta manufaa
Watanzania wengi wajinga

Maandamano yalipaswa yasiwe yanahusiana na chama cha siasa
 
  1. Haya ni maandamano kwa minajili ya kutetea haki ya kuishi.
  2. Polisi na vyombo vya dola wametuhumiwa kushiriki utekaji na mauaji ya raia
  3. Serikali imeonesha uzembe mkubwa kulinda maisha ya watanzania
  4. Bunge limegoma kujadili na kuihoji serikali kilio cha wananchi cha utekaji na mauaji ya raia
  5. CHADEMA wameibeba agenda hii kwa niaba ya Watanzaia, wameileta kwetu Watanzania bila kujali itikadi, imani na ukabila.
Je, Wananchi sisi tunakubali haya yaendelee?

Pia soma: Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea

Yeyote anayepinga ama kukwepa haya maandamano, tunamuelewa kwamba anaunga mkono utekaji na mauaji dhidi ya raia.

Samia Must Go
Kule M 23 huku S 23.....akili moja hiyo....

TREASON inanukia......
 
Back
Top Bottom