TANZIA Anayesadikiwa kuwa MwanaJF afariki dunia

Dah, noma sana 😂😂 sema hili jambo utatuzi wake ni kuwa na funguo yako tu.

Brother angu yeye ana funguo kabisa, tukikutana maeneo anakwambia anakuwa nayo maana kuna siku alilala kwenye gari alishindwa kuruka fensi akaona isiwe tabu..

Wake zetu / wachumba mtuzoee na mtusamehe tu, sio kama tunapenda ila kuna maeneo ikifika w/kend yaani ukiwaza kutokwenda unaumwa kabisa, mwili unakataa

RIP Mwamba, Pumzika Kwa Amani 🙏
 
Wakati mwingine Kuna mambo yanatokea kwaajili ya kuwa Somo ili wengine waweze kujifunza.

Kule kwetu hakuna Mwanamke anakuwa na Sauti kwa Mume wake. Never on Earth, na wao wanajua Hilo.

Yaani kule kabisa Mwanamke amfungie mlango Mume wake, mbona huyo Mwanamke anakuwa anahamu ya kujiuguza kwa kipigo, manake kipigo atakachopigwa sio Cha Nchi hii.

Anyways, huenda ndiyo Kifo alichoandaliwa Member mwenzetu.

Mbele yake, Nyuma yetu.
 
Haitosaidia kitu, na mpaka mnafanyiana hayo makusudi ni mmechokana au??

Huyo mjane labda hakusikia simu?
 
To yeye ni single mom bado hajapata ndoa🏃🏃
Kumbe bado yupo Single, kwa mchango aliotoa hapa inaonesha Mume atakayempata atainjoi maisha.

Kuna baadhi ya Wanawake wakishajua ameolewa na Mume Mlevi basi atahakikisha anahela za kunywa Kila siku, anamwachia mlango wazi au hata kumfata Bar kwenda kumchukua akiwa amelewa n.k
 
vp akifunga na komeo utaweza kufungua
 
Nitafanya kila namna akae sawa,kuna sababu ....hawaanzi iviivi mkuu
 
Yeah,tusiwe na mengi ya kuongezea
 
Wakati unakunywa mipombe huku ulimwita mjumuike pamoja wanaume tuache ubabe tembea na funguo zako utadhibiti hayo yote
Kwanza tukubaliane , kifo kipo ila kinatafuta sababu TU

Mwenza mmoja akiamua kumkoa mwenzake, wakati mwingine hajui matokeo yake Nini

Nimeshuhudia vifo vyenye mahusiano na wenza kufungiwa geiti ,× 2. Arusha sehemu inaitwa kwa "Tondi" alifariki mwanafunzi wa chuo Cha uhasibu kwa kuchomwa na mkuki wa geitini.

Hapohapo Arusha Njiro jirani na "kisaka villa"kijana mmoja alikua amehamia kwenye nyumba yake nahuyo mkewe , Tena Mungu kawajalia kipato wamejenga ghorofa . Siku ya tukio, kwamasimlizi ya walio msikiliza mlinzi, na mjane mwenyewe.

Mme alirejea nyumbani mida ya saa 4 , usiku.
Jamaa anafika kapiga honi, mlinzi ,kamueleza kua geiti limefungwa na funguo ziko ndani.
Jamaa kapiga simu na kubembeleza angarau afunguliwe geiti aingize Gali , atalala kwenye gari.
Mke aligoma kupitisha funguo dirishani Ili mlinzi afungue geiti.

Kilicho fuata ,jamaa aliomba ushauli kwa washikaji ,wakamshauli kwenda Masai camp Ili azuge walau kupambazuke bila kuona usiku ummekua mlefu.

Ile anarudi alfajiri kakutana na Hiace kwenye Kona za mlima uitwao Radio, na
Maisha ya kaishia hapo.
Jamaa zake walio simlia walidai kua.walimsihii apumzike kwenye kota za NHC kijenge, akagoma kwamadai anawahi amuone mkewe asije kushindwa kumsamehe.

Visa viko vingi, nimejalibu kusimlia vicache Ili nisiwachoshe.

Wito wangu kwa mashemeji nawake zetu watarajiwa , jitahidi kutokua vya vifo wenzawenu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kudaadeki innalilah wainnailaih rajiun. Mimi nadhani huyo mke wa jamaa vyombo vya usalama vile nae sahani moja akisota jela walau miaka 9 kwa kesi ya mauwaji isiyokuwa na ushahidi itakuwa ni funzo kwa wanawake wapumbavu wapumbavu kama huyo ......
 
Hapo ungeshauri wanawake wenzio kuwa waache viburi visivyokuwa na maàna. Sasa aligoma kufungua alitaka akalale wapi wakati hapo ndipo nyumbani kwake!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…