Capital G
JF-Expert Member
- Jul 2, 2017
- 3,445
- 5,336
Dah, noma sana 😂😂 sema hili jambo utatuzi wake ni kuwa na funguo yako tu.Pole kwa wafiwa..
Mi nilikuwa na mazoea hayo ya kulewa na kurudi usiku naruka hizo nondo asubuhi najikuta nimekwaruzika mwili mzima kisa cha kuacha mchezo huo sitasahau.
Nilirudi siku hiyo kilevi kimezidi kuliko kawaida nikapiga simu na kugonga sikufunguliwa nikachukua maamuzi ya kuruka. Niliacha kila kitu juu ya nondo surwali shati hadi boksa. Nikaingia ndani nikalala na viatu tuu. Asubuhi kidogo mama angu afe kwa presha akajua nimeuliwa nikatupwa juu ya nondo kumbe nguo. Akaingia ndani nimelala uchi akanikagua mzima zaidi ya michubuko tuu. Sitasahau
Brother angu yeye ana funguo kabisa, tukikutana maeneo anakwambia anakuwa nayo maana kuna siku alilala kwenye gari alishindwa kuruka fensi akaona isiwe tabu..
Wake zetu / wachumba mtuzoee na mtusamehe tu, sio kama tunapenda ila kuna maeneo ikifika w/kend yaani ukiwaza kutokwenda unaumwa kabisa, mwili unakataa
RIP Mwamba, Pumzika Kwa Amani 🙏