uhaba wa ardhi ulipelekea wachaga wengi kuhama toka kilimanjaro. wakati wa utawala wa mwalimu nyerere kuna wachaga walihamishiwa maeneo ya morogoro na kutokana na uhaba wa ardhi kilimanjaro.
miaka ya 70 na 80 kulitokea changamoto ktk kilimo cha zao la kahawa na hiyo ikasababisha wachaga wengi kukimbilia mijini. jamii ya kwanza kufanya umachinga dar es salaam, kwa mfano, kushona na kupiga rangi viatu, kukaanga chips, na gereji bubu, ni wachaga na hiyo ilikuwa miaka ya 80. ilipofika miaka ya 90 ndipo wakaja wamachinga toka mikoa ya kusini ambao walijishughulisha zaidi na uuzaji wa nguo.
hivi majuzi mbunge wa vunjo dr.kimei aliiomba serikali ifikirie kuwapatia wapigakura wake maeneo ya kulima sehemu mbalimbali za tanzania. sasa inabidi watu wajiulize ni mbunge gani mwingine amewahi kutoa ombi la namna hiyo kwa serikali? mchango huo wa mbunge ni kielelezo cha tatizo kubwa la ardhi na ukosefu wa fursa unaowakabili wananchi wa kilimanjaro.
moshi ingekuwa na fursa mpya kama arusha tusingewaona wachaga wengi maeneo mengine ya tanzania. pia wasingekuwa na tatizo la ardhi wasingetapakaa tanzania nzima. na wasingebahatika kupata elimu wasingehamia maeneo mengine kikazi na kuweza kuziona fursa zilizoko nje ya uchagani.
mwisho, wachaga wanapaswa kuwekeza ktk mji wao wa moshi ambao kwa sasa hivi umedumaa. wako wengi wenye mitaji mikubwa ambao wangeweza kuichangamsha moshi kwa kuwekeza kwenye viwanda. hii habari ya kujisifia kujenga majumba ya kifahari migombani naamini imepitwa na wakati. wachaga wa karne ya 21 wanatakiwa wajisifu kwa kuwekeza ktk viwanda ktk mkoa wa kilimanjaro.