Nenda pale kwa Tesha lete hapo bia kreti 10 na soda kreti 6Moshi ni pagumu kuanza biashara. Ila watu wakiisha kufahamu na ukaunda urafiki nao biashara inakuwa ni nzuri. Watu wanajenga mazoea ya kununua kitu kwa fulani. Hivyo mpaka ujenge jina na kuaminika. Na utasikia watu wakimtaja mtu zaidi kuliko jina la biashara yake.
Hivyo kama ndio unaanza inabidi uwe mvumilivu na utoe huduma ya uhakika kufikia kuaminiwa na kutambulika.
Kisha pita kwa Mrosso chukua sabuni box 3, halafu wakati unarudi utapita mashine kwa mama Oiso utachukua pumba na mashudu gunià 4.
Kwa mazingira hayo unafikiri mgeni utatoboa?