jamii ya kitanzania imeporoka kimaadili kwa kiasi kikubwa si wanaume wala wanawake wote hali mbaya....kifupi wenye mamlaka wameshindwa kuishape jamii isiathirike na maendeleo ya dunia....Ulaya na America kwa kiasi kikubwa wameishape jamii iweze kuishi sambamba na kasi ya ulimwengu bila kuathirika.
Tumetoea uhuru sana kwa wasanii wa muziki, filamu kuiharibu jamii kwa aina ya maisha yao kuwa ndio habari kuu kila mahala...umalaya na uchafu wote wa wasanii vinapewa covarage kubwa kwenye mitandano na kuonekana kama sehemu ya maisha ya kawaida...
Leo hii ujinga wa Hamornize, Kajala, Paula, Diamond, Rayvan nk ndio habari kuu kwenye jamii na kutangazwa na social medias kama sehemu ya maisha ya kawaida wakati ni ujinga uliopitiliza..
Mama zetu, Dada zetu wamepokea vibaya suala zima la haki sawa na kuwafanya wawe busy na dunia ili nao wawe na uchumi...hali hii imefanya wengi kukimbia jukumu la msingi la malezi kwa watoto na mwisho wake watoto kulelewa na akina baba au mabibi... Hali hii ya utafutaji wa maisha na hela kwa akina mama kunawafanya wengi kufanya mambo ya ajabu maana wengi wao wanalimitations kwenye huu utafutaji tofauti na wanaume.....( zipo kazi akinamama hawaziwezi na wanaume wanaziweza, hakuna kazi ya mwanamke mwanamume asiiwezi) .
Ni wakati wa jamii kuhimiza sana watu kuoa na kuolewa pia jamii ielimishwe uthamani wa utu na ubinadamu....Jamii ifundishwe kutothamini sana hela na kuweka mbele kuliko maisha na utu..